Tamko la Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kumtaka Freeman Mbowe kuomba radhi

unapokatisha matangazo wakati unahutubia unasababisha focus ihame badala ya kujadili maudhui ya mkutano wanafocus kuzungumzia kukatwa kwa matangazo hongera kwa Mbowe kwa uamuzi wa busara aliyoyachukua amalizie tu kumfukuza na millardayo kupunguza longolongo.
 
Wapeleke upuuzi huko.

Hakuna mtu atawaomba radhi hao wazee wa bahasha za kaki, hizo njaa zao wazipeleke huko CCM.
Haki ya nani hii ni laana kwa wanachedema. Kila jambo mnatanguliza matusi tu, matusi hayajawahi kuwa suruhisho la jambo lolote.
 
kama Gwajima kafanya matusi hadhari lakini leo hii ni mgombea wa CCM unadhani kuna mataga anaweza kutupa husia wowote tukamsikiliza??
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Mh. Mbowe akifanya kitendo Cha ujasiri na sahihi kabisa kwa sababu TBC haikwenda kwenye mkutano ule kwa nia njema kama ilivyo kawaidà yao waliokwenda kwa ajili ya CCM na mgombea wake. Yeyote aliyekuwa anafuatilia mkutano ule kwenye TV aliweza kuona nia mbaya ya TBC na kuchukizwa sana wala hatujutii kutoona live kilichokuja kinaengelea. Mpiga kura mwenye akili anakuwa amejua ni kiongozi gani atampa kura yake miaka mingi kabla ya siku ya Uchagusi bila kumwona wala kumsikia. Waandishi hao wa Habari wanatafuta ajira Serikalini kwa sababu wengi wameajiriwa kwa kutumia njia hiyo ya kuimba sifa za wenye mamlaka.
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
TBC ni serikali
Si wakafungue jalada polisi!
Ni vema TBC isijifiche nyuma ya vyama ambavyo waal havijulikani.
Ni ajabu TBC kulalalama kwani kwa muda mrefu hawana sifa ya kuwa na a balanced reporting katika matukio yao karibu yote.
Kiuhakika TBC anavuna kile walichopanda muda mrefu!
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
KUOMBA RADHI UTAKUWA NI UJINGA MKUBWA
 
Back
Top Bottom