Tamko la wazee Chadema: Mbowe ndiye kiongozi pekee barani Afrika asiyelipwa posho wala malipo yoyote na chama chake, anajitolea!

Tamko la wazee Chadema: Mbowe ndiye kiongozi pekee barani Afrika asiyelipwa posho wala malipo yoyote na chama chake, anajitolea!

Kuna pesa alikuwa anawakata wabunge wake na pesa za ruzuku

Zikikuwa zunaingia kwenye account ya familia yake
Tukumbushane, hiyo bilioni nane kaichukua wapia na kwa staili gani?
 
Kuna pesa alikuwa anawakata wabunge wake na pesa za ruzuku

Zikikuwa zunaingia kwenye account ya familia yake
Too cheap to buy my friend, hakuna mbunge hata mmoja aliwahi kukatwa pesa na mbowe. Katiba ya chama chao inabainisha suala la wabunge kuchangia chama. Kama kuna mbunge kakaa na ubunge miaka mitano na hajui katiba ya chama chake,basi huyo hata udiwani hafai. Na hakunapesa iliwahi kukatwa na kuingi akwenya akaunti ya familia. Hizi ni story za kumjenga Mbowe zaidi ya kumbomoa. yatupasa kuja na hoja zenye mashiko ili kumbomoa huyu jamaa. he is very strategic na wengi wetu tumekuwa tukisakama kwa maneno ambayo kwa akili yetu tunafikilia yatammaliza kumbe ndio tunamjenga kisiasa.
 
Safi sana, huyu ndiye mfano wa kuigwa...Mtu anajitolea tu lakini yupo tayari kupambana na yeyote anayetishia nafasi yake hiyo ya kujitolea kwa jamii.
 
Mkuu Mbowe alikuwa anawakata wabunge zaidi ya milion anaenda kula bata na mukya dubai
Too cheap to buy my friend, hakuna mbunge hata mmoja aliwahi kukatwa pesa na mbowe. Katiba ya chama chao inabainisha suala la wabunge kuchangia chama. Kama kuna mbunge kakaa na ubunge miaka mitano na hajui katiba ya chama chake,basi huyo hata udiwani hafai. Na hakunapesa iliwahi kukatwa na kuingi akwenya akaunti ya familia. Hizi ni story za kumjenga Mbowe zaidi ya kumbomoa. yatupasa kuja na hoja zenye mashiko ili kumbomoa huyu jamaa. he is very strategic na wengi wetu tumekuwa tukisakama kwa maneno ambayo kwa akili yetu tunafikilia yatammaliza kumbe ndio tunamjenga kisiasa.
 
Kuna haja ya TAKUKURU kupeleleza ukwasi waliokua nao
Mzee Mwinyi
Mzee Mkapa
Mzee Kikwete
Hii itaongeza uwajibikaji sana
 
Baraza la wazee wa Chadema limetoa tamko lake la kumtetea Mwenyekiti wa chama hicho dhidi ya njama ovu zinazotekelezwa na wabunge waliohamia CCM wakimtumia Mwita Waitara aliyewahi kuwa mlinzi wa Mbowe.

Katika tamko lake baraza la wazee limetaja sifa kuu 3 za Mbowe:

Mosi Mbowe ni mwenyekiti pekee wa chama cha siasa barani Afrika ambaye hapokei posho wala malipo yoyote kutoka kwenye chama chake anaitumikia Chadema kwa kujitolea.

Pili, Mbowe ndiye Mwenyekiti pekee wa chama cha siasa nchini anayeaminiwa na chama pamoja na wanachama ambao wameamchagua mara zote na amedumu katika uongozi kwa takribani miaka 25.

Tatu, Mbowe ndiye kiongozi pekee nchini aliyeingia katika uongozi akiwa tajiri na serikali kumfanyia figisu hadi anafilisika bila kuogopa wala kukata tamaa tofauti na wenyeviti wa CCM mzee Mwinyi, mzee Mkapa na mzee Kikwete ambao waliingia wakiwa maskini na kuondoka wakiwa matajiri.

Mwisho wazee hao wamemtaka Mwita Waitara kama ni mzalendo na siyo mnafiki anayejipendekeza, aanze kuhoji ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM.

Source: Ayo TV

Maendeleo hayana vyama

Ujinga ni kipaji pia
 
Tunataka TAKUKURU ifanye uchunguzi kwa ccm na viongozi wake,hofu yao ya uchaguzi isiwe kigezo cha kutumia vyombo vya dola kuhujumu vyama vingine. Kama takukuru ina nia ya dhati kusimamia fedha za vyama vya siasa Basi isioneshe upendelea wenye nia hasi, cuf tuliambiwa walitoa fedha kwenye akaunti ya chama na kuweka kwenye akaunti binafsi lkn hatukusikia takukuru wakifuatilia,ccm kumeibuliwa madudu hatukuona wakifuatilia, na hata serikalini pia iweje Leo iwe kwa chadema? Kuna mpango gani?
Unajua kuna watu wamezoea kuzani Watanzania ni wajinga, na hivyo bado wanaishi nao kwa mazoea! Ni TAKUKURU hukohuko ilipelekwa hadi flash iliyokuwa na sauti za viongozi wa CCM mkoa wa Arusha waliokuwa wakipanga njama za kuwahonga na kuwanunua madiwani wa CHADEMA, lakini hatujawahi kusikia hatua zozote zikichukuliwa! Si hivyo tu, mwaka 2016 Mwenyekit wa CCM aliunda tume ya kuchunguza mali za chama hicho nchi nzima, baada ya uchunguzi tume ile iliyokuwa chini ya Dk Bashiru Ally, iligundua ubadhirifu mkubwa sana wa mali za chama karibu Tanzania nzima, lakini hatujawahisikia TAKUKURU imejitosa kuita watu kuhojiwa! Je hapa tuamini nini? Tunaomba TAKUKURU wabishe hodi kwenye vyama vyote kama kweli wana nia njema!
 
Kwa sababu ni wazee sina haja ya kushangaa. Ni sahihi kabisa kama mwenyekiti wa Chama halipwi, lakini by Position hiyo anaingiza pesa. Ana malipo na maslahi kama Mbunge, pia kama KUB. Muhimu zaidi kama mwenyekiti chama chake kina muhudumia safari, makazi na issue zake zote kwa ujumla as a Chairman.
 
Wazee wa chadema kwenye kikao wakimsafisha MBOWE na tuhuma
FB_IMG_15906896585392420.jpg
 
Ama kweli ukizeeka na akili za kudanganya zinazeeka eti anajitolea miaka 20 bila posho wala malipoo!!!
Uzee mwingine sio dawa ni ujinga
 
Back
Top Bottom