TANESCO hali mbaya, Serikali yasuasua kununua mita na nyaya za kuunganishia umeme

Nenda Iringa kaulize bei ya nguzo, au kama ni mbali nenda hata Mwenge kaulize. Narudia tena, tusifanye siasa. Kwamba 321,000 bado watu walikuwa wanasota is irrelevant, issue ni kwamba kuunganisha umeme kwa 27,000 ni siasa. Hakuna kitu cha bure, kama vipi kila mtu apewe specifications akanunue kwa 27,000 yake tuone.
Unatetea ujinga
 
Naona unajiongelea mwenyewe... jisikilize mwenyewe utajua ujinga wa kukataa ukweli
Watu tuliwahi kulipia nguzo moja kwa laki 8 ukijumlisha na sevice line 321,000 ni milioni moja na laki 1 na bado tulisota nusu mwaka kuwekewa umeme alafu wewe unatetea nini?

Au unafikiri wote bado tunatumia luku za nyumbani kwa wazazi wetu?
 
Hilo la kuishi kwa wazazi siwezi kulijibu kwa sababu ni kauli ya kitoto.

Again, ulilipa tsh ngapi is irrelevant. The point is umeme kwa 27,000 ni siasa; prove otherwise kama unaweza. Nimekuuliza ukilipa 27,000 nani analipia gharama nyingine, unaishi kusema "natumia luku" ya mzazi wangu.
 
Tatizo siasa kwenye mambo ya kitaalamu...

Mtu anaunganishiwaje umeme kwa 27,000?

Hakuna cha bure duniani, gharama halisi sio 27,000... nani analipia hiyo tofauti? Kama serikali imeamua kweli kuunganisha watu umeme kwa bei nafuu;
1. Mwananchi afanye application
2. Apewe control number yenye gharama halisi
3. Akampe Mwigulu alipe.
Duh kweli fikra zetu zinatofautina Hizo Nguzo na Mita ni mali ya nani ?

Umeme sio kama maji yaani unafungua kulingana na mahitaji, uzalishaji ukiwa mwingi watumiaji wachache ni hasara..., sasa kama watu wengi hawajaunganishwa unadhani hizo Mega Watts 2100 zitakazokuja zitakwenda wapi ?

Ukimuunganisha mtu leo (Kumbuka mita na Nguzo ni za Tanesco) ni kwamba utakula Pesa ya Huduma to infinity.., ni kama wewe umejenga nyumba ya kupanga rent ya mwaka ni milioni mbili useme pesa hio sio halisi kwa nyumba yangu niliyojenga kwa milioni mia mbili kwahio sijengi..., ila kumbe ukiwa na wapangaji 10 baada ya miaka 10, hao hao wapangaji ndio watakujengea nyumba ya 11.....
 
Mkuu shida sio hiyo.... shida ni rasilimali.

Ni kweli watu wengi wakiunganishwa, ni faida kwa Tanesco; lakini sio faida ya leo, ni faida ya kesho.

Tanesco haitengenezi mita, waya au nguzo. Sasa wakiamua kuwaunganisha watu bure au kwa gharama ambazo sio realistic, nani atalipia mita, wire na nguzo? Unadhani kuna supplier ambae atakubali kuambiwa na Tanesco, "nipe vifaa, nitakulipa mteja akianza kutumia umeme", tuwe wakweli, nani atakayetoa nguzo Iringa kwenda Bukoba bure?

Ujamaa umetuharibu sana. Watu tunapenda tu vitu viwe cheap au bure, lakini hakuna anayetaka kujua nani analipa. Leo wanaongelea bima ya afya ya bure, lakini analysis ya NHIF inaonyesha wana hali mbaya sana. Wameongeza umri wa tegemezi kutoka 18 kwenda 21, huo ni mzigo mpya kwa NHIF, nani anaubeba.

Tutulize vichwa kidogo, serikali na yenyewe inatafuta pesa kama mimi na wewe, wategemezi wakizidi itashindwa tu.
 
Hivi unajua kwa Kampuni kama Tanesco kutengeneza faida ni nyongeza hata ikipewa ruzuku ni sawa..., Kitu cha maana kuliko vyote ni watu wengi kupata umeme wa uhakika na nafuu.

Nishati ni muhimu sana kwenye kila jamii kukiwa na nishati ya uhakika mambo mengi ya uzalishaji yatafanikiwa huenda kwa Tanesco kutoa nafuu ya gharama kwa unit.., hata yule mama kijijini aneyesaga unga wake wa mahindi atapata huduma ya bei rahisi kuliko vinginevyo (hii knock on effect ingawa Tanesco huenda isipate faida direct ila huduma inayotoa kwa jamii ndio inabidi ipimwe)

Kodi Ruzuku, kila mwananchi akinunua luku anakatwa na kuna pesa inapelekwa huko pia kutoka kwenye vyanzo tofauti, sio mbaya ku-invest leo kwa future gains..., au kila siku watakuwa wanaunganisha watu ? Au kuunganishwa kukishamalizika tutaanza kuongelea maintenance..., pia katika suala la generation Tanesco ina bahati sana hii nchi kuna vyanzo vingi sana ambavyo vinaweza kutumika katika Power Generation..., Tatizo la Tanesco sio watu sources of funds bali ni ufujaji na Shirika kuendeshwa bila uadilifu na kwa mikataba ya upigaji.

Unaongelea Ujamaa ? Unaongelea Bure...., Hivi hujui hata wewe hapo kodi zako zinachangia Tanesco ?, Nani kasema bure ? kuna bure na kuna affordable hivi ni vitu viwili tofauti sana...

By the way unaongelea BIMA hivi Sweden na United Kingdom healthcare yao ipoje ? Hao nao ni Wajamaa ? Insurance ni mchezo wa Volumes kukiwa na Bima ya Afya kwa Wote hata wengine wakipewa through ruzuku na wengine kuchangiwa kutoka kwenye Kodi zetu Bima lazima itafanikiwa.., KWANINI UTAULIZA...., ukiwa na watu 1,000,000 haiwezekani nusu yote wakaugua ila ukiwa na watu wawili mmoja akiugua hio ni 50% na lazima utafeli tu...
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Maneno matupu, TANESCO ni ile ile, poor services.
 
You make good points.... but shida ile ile, too theoretical, hautaki kusema "huu uwekezaji" nani ataulipia sasa hivi? Maana huo ndio ukweli, ni kama elimu bure; ni uwekezaji; na serikali inalipa. Huu uwekezaji wa mita, wire na nguzo za bei sawa na bure nani ataulipia? Halafu hiuo ruzuku unayoisema inatoka wapi? Umeona wanavyohangaika kuchukua hela zetu kila kona? Kweli unataka hizo hela zinaweke mita kwenye frame za watu huko Madale? Tatizo liko hapo, mara ya kwanza ilikuwa strictly vijijini tu, na fedha ilikuwa inatoka REA. Sasa hii expansion nani anaenda kuilipia? Affordable is relative, kama kitu bei yake ni 1,000,000 halafu ukauziwa 27,000 hiyo ni sawa na bure.

Hayo makato unayoongelea bado hayatoshi hata kuendesha shirika vizuri.

Kabla hujatoa mfano wa healthcare za Norway na UK toa pia takwimu zao za kodi. Unadhani wamefika hapo kwa bahati mbaya? Tax to GDP ratio ya Norway ni 38% na ya UK ni 33% wakati Tanzania ni 11%, tungefikia angalau ukusanyaji wa Kenya (18%) tungekuwa mbali lakini hapa hakuna serikali hapa yenye uwezo wa kufanya hivyo. Tuambiane ukweli, hizi siasa hazitatufikisha kaanani
 
Nguzo na vifaa vyote vya kuunganisha umeme ni mali ya TANESCO, katika hali halisi,huduma ya kuwekewa umeme ilipaswa kutolewa bure,mteja ulipie matumizi ya umeme.
Kwa miaka mingi walipa kodi wa Tanzania, kupitia serikali yao wamekuwa wanatoa ruzuku ya uendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania.
Miaka 5 iliyopita watumiaji wa umeme wamekuwa wakichangia au kulipia asilimia 3 kwenye mfuko wa REA,(kwa maana nyingine watumiaji wa umeme wamechangia mabillioni ya fedha kwenye mfuko wa REA).
Ninadhani,ni kwa muktadha huu serikali imeamua wananchi kulipia shs27,000 (kwa Waombaji wapya),hii siyo fadhila,ni wajibu wa serikali kwa wananchi wake na ni haki ya wananchi kupata huduma ya umeme kwa gharama nafuu.

Ushauri
(1). TANESCO kitengo Cha huduma kwa wateja badala ya kuwataka wateja kujaza taarifa zilizoainishwa, kwenye fomu zao,waagize kila kituo waweke utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya pending applications za wateja wapya (TANESCO Mkoa/Kanda/Makao Makuu ) kila siku/week/mwezi/quarter/mwaka na hatua mbalimbali zilizofikiwa na changamoto.
(2). Aidha kitengo Cha huduma kwa wateja wanaweza kuingia kwenye mitandao wakaona (kwa mfano kituo Cha Nyakato au Chanika) Kuna pending applications ngapi.
(3).Kwa kuwa asilimia 3 ya REA inakusanywa na TANESCO,na kupelekwa kwenye mfuko au taasisi husika.
-Ni vema jukumu la usambazaji umeme(transmission-nguzo na vifaa vya umeme),likahamishiwa REA,na
-TANESCO,ikabakiwa na jukumu la uzalishaji (Generation-Vyanzo vya umeme) na utoaji huduma kwa wateja (ukusanyaji maduhuli nk).
Mawazo mazuri sana chief

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Karibia vifaa vyote nguzo, nyaya, mita, vikombe n.k vinanunuliwa kutoka nje ya nchi, na malipo ya nje ni fedha za kigeni.Inawezekana fedha za manunuzi ni changamoto
 
Back
Top Bottom