TANESCO imeisamehe Zanzibar deni la umeme la bilioni 60

Kama nikweli imewezekana kufuta deni la umeme Zanzibar, wanashindwa nini kuzifutia dei taasisi za serikali huku bara?.

Mambo kama hayo yana umiza mioyoyetu sana,hilodeni siku mimi nikiwa rais nitalihuisha na kuamuru lilipwe, sitakubali huumpango wa ubaguzi kama huu.
 
Sasa ni nini kifanyike?
Katiba Mpya itamke wazi, Tanzania kuna Muungano, wenye serikali moja.

Ngoja nikupe habari: Ule mchakato wa Katiba Mpya uliofanyika chini ya Marehemu Sitta, na Samia akiwa Naibu wake; ni hawa hawa akina Samia waliokwamisha sababu ya Muundo wa Muungano.
Sasa yeye ndiye rais, na unaona anavyozungukazunguka na swala la Katiba Mpya akitafuta jinsi atakavyookoa jahazi kwenye swala hilo la Muungano.
Huku urais wa nchi anao yeye, na kule akiwa analinda maswala ya Zanzibar iendelee kunufaika zaidi ya kiasi kinachostahiki katika Muungano.

Serikali ni Moja tu, chini ya rais mmoja wa muungano.
Haya mengine ya kulembalemba achaneni nayo.

Kuhusu Muungano kuvunjika, hilo sahau. Zanzibar ni sehemu isiyotenganishwa na Tanganyika.
 
Hussein Mwinyi Anafanya nini kule na ikulu yake na bunge lake?
 
Ni mara ya pili zanzibar wanafutiwa madeni ya umeme na tanesco huku wabara wanakamuliwa. Na juzi huyu maharage eti anasema sio busara kushusha bei ya umeme wakati ni kubwa zikiongoza duniani. Mfano wakati kwa unit marekani na ulaya wanalipa $0.02 tanzania tunalipa $0.22. Magufuli akija na ujenzi wa bwawa la nyerere aliapiza kushusha bei ili kuchagiza maendeleo ya viwanda na matumizi kwa wingi ya wananchi.
Wahuni sio watu wema. Wanataka faida ya uwekezaji wa umma wafaidi kwa mishahara na marupurupu manono vigogo bila raia kufaidika wala kuona faida yoyote.
 
Bi tozo sehemu za strategia zote kaweka vichwa boga wake. Angalia fedha kaweka kichwa bingiri kazi kuchekacheka na kuvusha pesa, tanesco ndo kaua kabisa kapeleka kipara kipya , huyu anajiona first born kabisa, muungano ndo kamchimbia mpiga diri wa msoga. Ingekuwa hawa watoto wa kambo tungeshalimia meno ila midanganyika ni nyumbu tu
 
Sasa wafungiwe Luku kuu basi kwenye waya kuu inayoingiza umeme kisiwani.
 
Kwani nani aliwatuma mtuvamie?
 
Katika kosa kubwa ambalo sintakaa nimsamehe Nyerere labda lirekebishwe ni kule kuipa hadhi ya utawala wa ndani Zanzibar. Hili ni kosa kubwa la kihistoria na linatakiwa apatikane mtu wa kulirekebisha. Kama walivyofanya India kule Kashmir. Ilitakiwa Zanzibar Leo hii iwe mkoa tu hiz kelele hazitaisha wasipofanya maamuz magumu.
 
Endelea kuota
 
Binadamu huonyesha yake anapokosa usimamizi makini!!

Sisi tuna dola inayolea ujinga lazima mtu ataonyesha ujinga wake!!!

Mimi nitalia na Dola siku ZOTE!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…