TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Hili wazo mbona linatekelezeka tu tena kirahisi bila shida. Hapa nitatoa mfano hai;

Kipindi tunaanza masomo form 1 kulikuwa na fedha ya tahadhari unalipa na fedha hii hurudishwa pindi unapohitimu form 4 baada ya kusainiwa clearance form na kubainika hakuna deni/hasara/uharibifu uliofanya katika kipindi chote cha masomo.

Kwa namna hii hii TANESCO wanaweza kwa kushirikiana na serikali za mitaa kuwaelekeza wamiliki wote wa nyumba za kupanga ku-introduce pesa ya tahadhari kwenye kodi ya pango ambayo inalingana na kiwango ambacho Tanesco wanakopesha.

Kwa namna hiyo, dhamana ya deni inabaki kwa mwenye nyumba na endapo mpangaji/wapangaji wanahama bila kuwa na deni pesa ile (ya tahadhari) inarejeshwa kwa muhusika.

Kama wapangaji wako zaidi ya mmoja, fedha ile inagawanya mf. wako watano na kiwango cha kukopa ni 25,000/= basi kila mpangaji kwenye kodi yake ya mwanzo ataongeza elfu 5 kama hela ya tahadhari na siku akiwa anahama na hakuna deni anarejeshewa pesa yake.

Nadhani ni good idea kwa zama hizi kwa Tanesco na hata mamlaka zingine za serikali, itawaongezea wigo wa mapato kupitia riba.

Mbali na hii pia wanaweza kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha wateja gharama za kuunganisha huduma na kuweka interest pia, hii itasaidia kupunguza hasara na utegemezi wa ruzuku kwenye uendeshaji wa hizi mamlaka.
 
Zanzibar (TUKUZA) upo umeme wa mkopo. Mkopo huo ni wa units kadhaa tu, ambapo ni rahisi kwa mkopaji kuresha pasi usumbufu.
 
Tumepokea ushauri tunashukuru sana mpendwa mteja wetu

TANESCO , Makao Makuu
Na kingine kwanini msiwe mnawakopesha kuwaunganisha wateja umeme then kwenye kununua umeme muwe mnawakata kidogo kidogo mpaka watakapo maliza deni liwe kama zile unit za kuanzia???
 
Ndio maana niko "addicted" na JF na hasa GT, wengine tulipepesa macho huko kwa Wakoloni wetu, ni jambo la kawaida sana, fikiria umeme wakatika saa saba usiku na huna chochote kwenye mobile wallet wala ile mikopo yao?!
Brilliant idea ila kama uwajuavyo TANESCO wako kama DAWASA, wagumu kufikiria, hawafikiri nje ya boksi wala ku "brain storm" zile "grey cells" zao kichwani!
Tuombe watausoma huu uzi na kutafakari...
 
Salary advance🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…