gspain
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,920
- 6,081
Hili wazo mbona linatekelezeka tu tena kirahisi bila shida. Hapa nitatoa mfano hai;Umeangalia kwa mtazamo mmoja. Kwa wenye nyumba tu lakn haujaangalia kwa wapangaji. Mtu amepanga fremu au nyumba nzima. Siku anakaribia kuondoka anakopa umeme wa 20,000. Na halipi deni.
Hiyo hela atalipa nani? Siyo rahisi kama unavyofikiria ndiyo maana hauajatoa maelezo yaliyojitosheleza na njia zake ndiyo maana umekimbilia kukopesha.
Hii italeta migogoro sana, na siafiki suala hili la kukopa umeme hata kwa 100%
Kipindi tunaanza masomo form 1 kulikuwa na fedha ya tahadhari unalipa na fedha hii hurudishwa pindi unapohitimu form 4 baada ya kusainiwa clearance form na kubainika hakuna deni/hasara/uharibifu uliofanya katika kipindi chote cha masomo.
Kwa namna hii hii TANESCO wanaweza kwa kushirikiana na serikali za mitaa kuwaelekeza wamiliki wote wa nyumba za kupanga ku-introduce pesa ya tahadhari kwenye kodi ya pango ambayo inalingana na kiwango ambacho Tanesco wanakopesha.
Kwa namna hiyo, dhamana ya deni inabaki kwa mwenye nyumba na endapo mpangaji/wapangaji wanahama bila kuwa na deni pesa ile (ya tahadhari) inarejeshwa kwa muhusika.
Kama wapangaji wako zaidi ya mmoja, fedha ile inagawanya mf. wako watano na kiwango cha kukopa ni 25,000/= basi kila mpangaji kwenye kodi yake ya mwanzo ataongeza elfu 5 kama hela ya tahadhari na siku akiwa anahama na hakuna deni anarejeshewa pesa yake.
Nadhani ni good idea kwa zama hizi kwa Tanesco na hata mamlaka zingine za serikali, itawaongezea wigo wa mapato kupitia riba.
Mbali na hii pia wanaweza kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha wateja gharama za kuunganisha huduma na kuweka interest pia, hii itasaidia kupunguza hasara na utegemezi wa ruzuku kwenye uendeshaji wa hizi mamlaka.