TANESCO isifiche kuhusu mgao wa umeme

TANESCO isifiche kuhusu mgao wa umeme

litamgalimu sana niemongea na watu kule kwenye bwawa la nyerere wanasema winchi lipo na iyo milango ipo January anahujumu taifa
Inampasa kuelewa kuna tofauti kubwa kati ya JPM kama mtu binafsi, na JPM kama kiongozi wa taasisi nyeti ya urais aliyoiongoza. Ni lazima azingatie na kufuata miradi ya kimkakati ambayo JPM alitembea nayo katika kipindi alipokuwa madarakani.

Kama ana hoja kinzani ni vyema angeipenyeza kupitia marafiki zake waliopo vyama vya upinzani na wala si wale waliopo ndani CCM na kuonekana waliathiriwa katika utawala uliopita. Ukiangalia kwa jicho la tatu, utaona kabisa hata timu ya wateule wake, wengi wao ni wale waliowekwa kando ktk awamu ya JPM.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hapo ndio utaona hata kwa mbali umuhimu wa Magufuli. Alikuwa anawafanya hawa mabwege wawatii wananchi. Angalau walikuwa na hofu. Utendaji kama huu wa mazoea ulipungua kwa kiwango kikubwa...
Wakati wa enzi za utawala wa JPM, wengi wetu tulimpa majina mabaya kwa kuangalia tu upande mmoja wa shilingi. Haijapita hata mwaka mmoja toka aage dunia, ndipo pengo lake linaanza kujidhihirisha wazi kabisa kwa kumlinganisha na utawala wa sasa.

JPM alikuwa ni mfuatiliaji wa mambo, na alijitahidi mno na kuhakikisha miradi inayogusa maslahi ya watu wengi kuwa ndiyo kipaumbele chake.

Alikuwa mkali na hakuvumilia uzembe kwa watumishi wa umma. Kauli ya waziri mwenye dhamana ya nishati kuwa TANESCO hawakuthubutu kukata umeme kwa kuwa walimuogopa, basi atambue kuwa hiyo ndiyo mojawapo ya "strengths" zake.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Wakati wa enzi za utawala wa JPM, wengi wetu tulimpa majina mabaya kwa kuangalia tu upande mmoja wa shilingi. Haijapita hata mwaka mmoja toka aage dunia, ndipo pengo lake linaanza kujidhihirisha wazi kabisa kwa kumlinganisha na utawala wa sasa...
Mimi binafsi nimemkumbuka MAGUFULI kwa mambo mengi tu. Siku hizi ofisi nyingi za umma zimerudi kimazoea kizamani,hakuna utendaji. Magufuli aliwajua sana watendaji ofisini. Vile vitisho vyake alianza kwa utumbuaji,uliwarudisha kwenye uwajibikaji kwa kasi. Vingi alirejesha mahala panapotakiwa.

Binafsi aliharibu tu kuwafanya tra wawe mungu mtu. Wakaanza kuwanyang'anya watu,kuwatisha na kuwaibia kwa njia zisizo halali, wakajineemesha kwa njia hiyo. Hiyo hali hawajaiacha,bado wanaendelea nayo kwa chini chini. Ksbb tayari walishaonja
 
Wakati wa enzi za utawala wa JPM, wengi wetu tulimpa majina mabaya kwa kuangalia tu upande mmoja wa shilingi. Haijapita hata mwaka mmoja toka aage dunia, ndipo pengo lake linaanza kujidhihirisha wazi kabisa kwa kumlinganisha na utawala wa sasa...
Halafu usalama wa taifa wapo tu wanaangalia taifa linahujumiwa badae akija rais mkali watampa repoti ya uhuni uliokuwa unafanyika tanesco kama kipindi cha ngereja yani hakukuwa na tatizo lakini alikua anatoa amri umeme ukatwe
 
Muda huu kuna maeneo mengi katika jiji la Dar es Salaam umeme umekatika hebu tupeane taarifa hali ilipo mtaani au kazini kwako ili tujue ukubwa wa tatizo na Tanesco waje kutupa mrejesho wa hali ilivyo na viongozi waone hali halisi iliyopo.Ni vizuri kutaja umekatika muda gani.
Karibuni
 
Toa kwa haraka taarifa TANESCO kwa ukatikaji huo wa umeme. TANESCO ipo kwa ajili ya kukuhudumia kwa viwango vya hali ya juu kwa ubora. TANESCO shirika la wananchi wote.
 
Nimeona ratiba ya umeme kwa maeneo ya oysterbay na Mbezi huko mitandaoni, je mgao umeanza au ni mambo ya kiufundi tu?

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
 
Na utazidi kuwa mkali zaidi kutokana na vyanzo vyake kupungua maji,jua kali,ndani joto umeme hakuna pesa ngumu kwanini tusiwe vichaa.
 
Nimeona ratiba ya umeme kwa maeneo ya oysterbay na Mbezi huko mitandaoni, je mgao umeanza au ni mambo ya kiufundi tu?

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
hili swali tuwaulize nyie makada wa CCM maana nyie ndiyo mmekabidhiwa wajibu huu.
 
Back
Top Bottom