Ingalikuwa ni enzi za zamani zile za msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Ili kukabiliana na uhaba huu wa maji, wananchi wangalihimizwa kufunga na kusali na kuomba kwa siku tatu kupitia imani zao, ili Mola wao akapate kuwasaidia.
Naamini kwa imani hii ya hali ya juu ingaliweza kufanya kazi kwa 100% vile kama ilivyokuwa dhidi ya tishio la UVIKO 19. Natambua JPM alizingatia nukuu ifuatayo kutoka katika maandiko matakatifu;
Mathayo 7:7-9
“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa. Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa. Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe?