SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

MABORESHO YA MIUNDOMBINU MKOA WA TEMEKE

Tunawataarifu Wateja wetu wa Mkoa wa Temeke kuwa, kutakuwa na maboresho ya miundombinu ya umeme kwa kufanya kazi za Kuhamisha njia ya umeme ya msongo mkubwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya daraja la Mwalimu Nyerere, kubadilisha nguzo zilizooza, kuimalisha viunguo vya umeme na kukata miti iliyopita kwenye njia za msongo mkubwa wa umeme wa kilovolti 33, siku ya Alhamisi, Decemba 07, 2017 kuanzia saa 02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni. Kutokana na maboresho hayo maeneo ya Vijibweni, Tungi, Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji Pemba Mnazi, baadhi yamaeneo ya Toangoma na maeneo ya jirani yatakosa umeme

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo

Toa taarifa Dawati la dharura Mkoa waTemeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au Kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768 985 100.

Tovuti:
www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

Desemba 05, 2017
 
Kwani mnaona shida gani kutangaza kuna mgao rasmi? Kama ndio hali halisi tutangaziwe. TANESCO
 
Kinachoshangaza ni kwamba kila siku wanaboresha lakini matatizo hayaishi, huko viwandani tunaenda kwa kukatakata umeme hovyo hovyo.

Wekeni LUKU kwenye ofisi zote za serikali muweze kujiendesha. wakopaji wakiwa wengi tena wa mabilioni mtawezaje kuendesha shirika kwa pesa za walalahoi sisi.
 
Mie naomba kujuzwa umeme single phase one km haufiki mana mie nmepimiwa ndo jibu nililopewa hilo, nmewaambia wanipe gharama nikaambiwa gharama ni kubwa zinaweza fika Mil 50 mara ninunue Transforma wafunge ndo umeme ufike. haikuniingia akilini kwa kwelii
 
Nimebadilishiwa tariff kwenda tariff 4 lkn namba nilizopewa kuongiza kabla ya token mita haikubali. Nifanyeje?

Vv
 
Jina
Mkoa
Eneo
Namba ya simu
Tatizo
 
Habari zenu tanesco
Jamani mi toka jana naaingiza unit inasearch tu vile vimishale mwisho inaandika ERROR 17 sijui tatizo nini mnisaidie leo siku ya pili niko gizani.
 
Habari zenu tanesco
Jamani mi toka jana naaingiza unit inasearch tu vile vimishale mwisho inaandika ERROR 17 sijui tatizo nini mnisaidie leo siku ya pili niko gizani.
Tunaomba namba ya mita na namba ya simu
 
Namba ya mita na token ulizopewa tafadhali
Mita yake ni namba 24214169096
Namba alizopewa aingize ili ahamishwe tariff ni 4058 8557 7619 6863 2390 0157 2600 7881 3528 0953 .

Mita nyingine ni namba 24214169104. Namba zinazogoma ili aingizwe kwenye tariff nyingine ni 4041 4371 6933 6919 7977 6033 6564 4609 9654 9881.

Akiingiza hizo namba mita haisomi/hairespond, Akiingiza token baada ya kuwa ameingiza hizo namba bado mita haisomi
 
hanaga majibu kupitia ukurasa huu...........!!!
 
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Tunatizo la mita Tunaomb msada umeme wa elf 5 tunapata unit 14 wakat mwenye nyumba anapata unit 45 had hamsin
Mtakuwa mpo kundi la matumizi tofauti tunaomba namba yakomya mita tafadhali
 
Hongera kwa kujitahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…