Ndugu mpendwa mtejaTatizo la umeme Bagamoyo ni kama mgonjwa wa ngiri jumanne asubuhi saa 11 ulikatika baada ya mvua kunyesha kidogo jumatano asubuhi saa 11:45 ukakatika tena uliondoka na tshirt kwenda kazini jana alhamisi saa 12 asubuhi umekatika tena ukarudi saa 2, leo tena siku ya mapinduzi saa 12h asubuhi mpaka hivi sasa hakuna umeme hii ni aibu hivi kweli hivyo viwnada vitajegwa kwa style hii hatutafika kwakweli.
Huyu jamaa muwakilishi wao hapa jf yeye ni kutoa tu taratibu za malalamiko wakati wanapokata umeme hawana utaratibu.
Ingekuwa waeja wanashindwa kulipia umeme hapo sawa lakini watu wapo tayari kulipia lakini huduma ni mbovu sana
Sitoi no kila siku mnachukuwa namba zangu na hakuna la maana linalofanyika leo imebidi nikafanye kazi zangu Dar.Ndugu mpendwa mteja
Tunaomba namba yako ya simu na eneo ulilopo Bagamayo
[emoji23][emoji23][emoji23]Sitoi no kila siku mnachukuwa namba zangu na hakuna la maana linalofanyika leo imebidi nikafanye kazi zangu Dar.
Tunaomba taarifa kamili eneo lako, simu, nini kimetokea, mkoa na wilaya yako, je ulifika ofisiniMimi shida yangu ni namna nilivyoachwa solemba kwenye mradi wa rea mtaani kwetu! tulihamasishwa kufanya wiring nyumba zetu, tukaacha na mambo mengine kwa ajili ya kutaka tupate umeme, cha ajabu mlichonifanyia sijawaelewa hadi leo. nimeachwa mwenyewe, wiring nimefanya, nikatiwa moyo kuwa napata umeme hadi leo hakuna kitu kinaendelea! nilipowafuata naambiwa mradi umeisha nilipie kwa bei ya ajabu!
kwa maonezi Yale, Mungu anawaona!
Tunaomba namba yako ya taarifa na namba ya simu tafadhaliNimeripoti tatizo la nguzo kutaka kuanguka watu wa emergency wakaja kuona na kuthibitisha kweli nguzo imeshikiliwa na waya mmoja wa umeme unaoingia kwenye moja ya nyumba zilizo chukulia umeme kwenye hiyo nguzo. Mafundi walikuja kuona wakasema wanaenda kufuata nguzo Ila hii ni wiki ya tatu hajarudi. Nimepiga simu customer care wanasema hamna nguzo wakati wiki hii niliona mafundi wenu walikuja kucheki transformer wakiwa na nguzo, nimeambiwa kuwa hizo nguzo ni za wateja wapya kwahiyo Sisi wa zamani hatuna thamani.
Mnataka kutuunguzia nyumba aisee maana hii nguzo muda wowote itaanguka.
Hili tatizo lipo kinondoni mkwajuni, sasa iweje watu wanalipia umeme halafu msema nguzo hamna na hamjui lini zitawasili na bila shaka sidhani hata kama mnaweka rekodi ya sehemu zote zinazo hitaji nguzo ili zikija mkaweke
Mwisho waambieni customer care representatives wenu wajifunze kwa customer care wa mitandao ya simu. Yani wana huduma mbovu mbovu hamna mfano. Mtu unapiga simu anaongea na wewe Kama hataki, Tena ukipiga usiku ndio kabisaaa mwingine anakuwa busy kupiga stori na mwenzake
Tunaomba namba yako ya taarifa na namba ya simu tafadhali