TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco mnajitahidi kadiri ya uwezo wenu, ila bado nauliza hivi km kuna shida ya umeme mnapungukiwa nini kutoa taarifa kwa wateja wenu?

Tangu saa tatu asubuh mamboleo, moshi vijijini, mkoa wa Kilimanjaro hakuna umeme!

Hivi mkitoa taarifa,, ndugu wateja wetu kutakuwa na tatizo la umeme kesho muda flani hadi flani...mtapungukiwa nini?

Nawaambia hivi mkurugenzi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro usipoondolewa mwaka huu ntshangaa sana!

Mnafanya kazi kwa mazoea, customer care ndo wapuuzi haswa wanahisi wao tu ndo wanakazi za maana wengine hatuna! Mngejua kuwa wateja ndo tunawalipa msingekuwa na majibu ya hovyo!

Tanesco badilikeni soor hamtakuwa monopoly tenaa! HAYA
 
Mimi sijaelewa juu ya mradi wa rea!
magawa kwa wananchi mpendavyo ninyii, au mnagawa kwa yeyote anaye hitaji alimradi ametimiza yanayotakiwa?!
 
Niliuliza Hapa Kwenye Thread Hii
Nimefungiwa Umeme Tarehe 27.12.2016 Hadi 27.12.2017 Nimetumia Units 205

Sasa Kwa Matumizi Hayo Nakuwa Kwenye Kundi Gani La Matumizi Ya Umeme Wa Tanesco
Ulinielekeza Kuwa Nifike Ofisini Nijaze Form

Week Moja Iliyopita Nilifika Ofisi Ya Tanesco Mkoa Wa Morogoro Nikawaelezea Suala Hili Wakaniambia Nirudi Siku Inayofuata Kwaajili Ya Kujaza Form


Leo Sasa Nimepata Nafasi Tarehe 15. 01.2018
Nimekwenda Ofisini Nilichojibiwa Ni Kuwa Hayo Ni Matumizi Ya Kawaida Niondoke.

Kuna Wakati Hawa Watumishi Wa Mikoani Wana Majibu Yasiyoridhisha Sana Kama Hili Nililopewa
Najiuliza Uliposema Niende Ofisini Kujaza Form Hii Huduma Ipo Ama Kuna Tanesco Mbili?

Naomba Sasa Iwapo Ufumbuzi Wa Tatizo Hili (Huduma Hii ) Naweza Kuipata Hapa Hapa Kwenye Forum Hii Nisaidiwe Yaani Mahitaji Gani?
Yanahitaji

Tanesco Mkoa Nimejibiwa Dry Kama
Meter Number Ni 24 2147 01716
 
TANESCO nimefanya wiring...wamekuja surveyors wakaniambia nahitaji kulipia nguzo moja....na gharama nyingine....nimelipa vyote November mwaka jana...., baada ya mwezi mmoja...(katikati ya December ) wakaja kusimika nguzo TU kisha wakaondoka.

Hadi leo hii sina umeme...ipo nguzo tu ambayo imesimama haina nyaya.. malipo yote nimekamilisha..., majirani wote walonizunguka wana umeme.

ni Mateso kwakweli...mimi sielewi shida ni nini hasa ....yani sielewi.
 
hivi: hii page ni yao Tanesco kweli au MTU tu anatuenjoy!? naona km sioni majibu yao!
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;

LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.
Luku zenu za waison zina sumbua sana hasa muda wa jion kuanzia saa moja jion mpaka saa tatu na nusu usiku zinazima mara kwa mara. ni kero kwa kweli kama kuna utaratibu wa kubadilishiwa hiyo luku naomba nijulishwe.
 
Luku zenu za waison zina sumbua sana hasa muda wa jion kuanzia saa moja jion mpaka saa tatu na nusu usiku zinazima mara kwa mara. ni kero kwa kweli kama kuna utaratibu wa kubadilishiwa hiyo luku naomba nijulishwe.
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
Kutakuwa na umeme mdogo eneo hilo tunaomba hizo taarifa mkuu
 
sijawaelewa. natuma jina langu na namba yangu na eneo nitokalo humu ndani!?
 
Kinondoni sehemu gani, mkwajuni hapo kwenye mafuriko? Kama ni hapo mnatakiaa kuhama.

Umeme upo labda umeishiwa Luku.
 
Back
Top Bottom