Tanesco mnajitahidi kadiri ya uwezo wenu, ila bado nauliza hivi km kuna shida ya umeme mnapungukiwa nini kutoa taarifa kwa wateja wenu?

Tangu saa tatu asubuh mamboleo, moshi vijijini, mkoa wa Kilimanjaro hakuna umeme!

Hivi mkitoa taarifa,, ndugu wateja wetu kutakuwa na tatizo la umeme kesho muda flani hadi flani...mtapungukiwa nini?

Nawaambia hivi mkurugenzi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro usipoondolewa mwaka huu ntshangaa sana!

Mnafanya kazi kwa mazoea, customer care ndo wapuuzi haswa wanahisi wao tu ndo wanakazi za maana wengine hatuna! Mngejua kuwa wateja ndo tunawalipa msingekuwa na majibu ya hovyo!

Tanesco badilikeni soor hamtakuwa monopoly tenaa! HAYA
 
Mimi sijaelewa juu ya mradi wa rea!
magawa kwa wananchi mpendavyo ninyii, au mnagawa kwa yeyote anaye hitaji alimradi ametimiza yanayotakiwa?!
 
Niliuliza Hapa Kwenye Thread Hii
Nimefungiwa Umeme Tarehe 27.12.2016 Hadi 27.12.2017 Nimetumia Units 205

Sasa Kwa Matumizi Hayo Nakuwa Kwenye Kundi Gani La Matumizi Ya Umeme Wa Tanesco
Ulinielekeza Kuwa Nifike Ofisini Nijaze Form

Week Moja Iliyopita Nilifika Ofisi Ya Tanesco Mkoa Wa Morogoro Nikawaelezea Suala Hili Wakaniambia Nirudi Siku Inayofuata Kwaajili Ya Kujaza Form


Leo Sasa Nimepata Nafasi Tarehe 15. 01.2018
Nimekwenda Ofisini Nilichojibiwa Ni Kuwa Hayo Ni Matumizi Ya Kawaida Niondoke.

Kuna Wakati Hawa Watumishi Wa Mikoani Wana Majibu Yasiyoridhisha Sana Kama Hili Nililopewa
Najiuliza Uliposema Niende Ofisini Kujaza Form Hii Huduma Ipo Ama Kuna Tanesco Mbili?

Naomba Sasa Iwapo Ufumbuzi Wa Tatizo Hili (Huduma Hii ) Naweza Kuipata Hapa Hapa Kwenye Forum Hii Nisaidiwe Yaani Mahitaji Gani?
Yanahitaji

Tanesco Mkoa Nimejibiwa Dry Kama
Meter Number Ni 24 2147 01716
 
TANESCO nimefanya wiring...wamekuja surveyors wakaniambia nahitaji kulipia nguzo moja....na gharama nyingine....nimelipa vyote November mwaka jana...., baada ya mwezi mmoja...(katikati ya December ) wakaja kusimika nguzo TU kisha wakaondoka.

Hadi leo hii sina umeme...ipo nguzo tu ambayo imesimama haina nyaya.. malipo yote nimekamilisha..., majirani wote walonizunguka wana umeme.

ni Mateso kwakweli...mimi sielewi shida ni nini hasa ....yani sielewi.
 
hivi: hii page ni yao Tanesco kweli au MTU tu anatuenjoy!? naona km sioni majibu yao!
 
Luku zenu za waison zina sumbua sana hasa muda wa jion kuanzia saa moja jion mpaka saa tatu na nusu usiku zinazima mara kwa mara. ni kero kwa kweli kama kuna utaratibu wa kubadilishiwa hiyo luku naomba nijulishwe.
 
Luku zenu za waison zina sumbua sana hasa muda wa jion kuanzia saa moja jion mpaka saa tatu na nusu usiku zinazima mara kwa mara. ni kero kwa kweli kama kuna utaratibu wa kubadilishiwa hiyo luku naomba nijulishwe.
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO/UNACHOHITAJI....................

10.NAMBA YA TAARIFA ULIYOPEWA.................


"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Kutakuwa na umeme mdogo eneo hilo tunaomba hizo taarifa mkuu
 
sijawaelewa. natuma jina langu na namba yangu na eneo nitokalo humu ndani!?
 
Kinondoni sehemu gani, mkwajuni hapo kwenye mafuriko? Kama ni hapo mnatakiaa kuhama.

Umeme upo labda umeishiwa Luku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…