TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA.

NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)


TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO
 
Ivi umeelewa nilichoandika hapo,? Nimekuambia bagamoyo mkoa wa pwani maeneo ya mapinga hadi kerege, sasa namba yangu na jina langu la nn?
 
Tafadhalini TANESCO hapa Tandale Chama Transformer yenu linamwaga miali ya moto siku ya tano leo.Tumewapigia Magomeni lakini hakuna lolote walilofanya mpaka sasa
Muda si mrefu hii nguo yenu itaungua na kuchoma nyumba za jirani.

Magari yenu ya emergency yanapita hapa kila baada ya nusu saa lakini hawaoni tatizo lililo wazi kabisa
 
TANESCO Naomba kujua mtakuja kunifungia umeme kwangu Kimara Saranga lini maana nimelipia tokea December mwaka jana mwanzoni, mlinambia itachukua miez miwili ndo imeshaisha hivyo!mwenzenu nateseka sana vitu vyangu vya umeme vinaharibika tu najuta kuwafahamu maana hata kupasi nguo nishasahau, na pesa nimeshalipa 515618.

Alafu cha ajabu mliniambia nikishalipa nisirudi ofisin kuulizia ati mtakuja wenyewe!Mbona hamji jamani khaa..
 
nenda kwenye kituo chako cha karibu cha tanesco, mi mwenyewe niliwekwa tariff 1, nilibadilishiwa cery simple na sikuhonga hatta senti moja.
Naona Tanesco kigamboni bado kuna urasimu nimeandika barua ya maombi wameniambia nijaze fomu halafu baada ya wiki mbili ndio watanirekebishia na wanasema lazima waje nyumbani.

sasa sijui maana ya system wakati rekodi zote zinaonekana kwao.
naomba muliangalie hili
 
Hiyo ndio taratibu mkuu lazima tuje tukukagua maana wapo wanaoiba umeme halafu wanaomba kuwa tarif 4 ili kuhalalisha hilo
 
Ulilipa kwa jina gani na namba yako ya simu?kwa kiasi ulicholipa bado upo ndani ya muda wa mkataba wa huduma kwa wateja
 
Tunaomba namba yako ya simu mkuu tufike eneo husika
 
Lalamiko la eneo husika linaweza kutumwa hata pm
Kwani ikiambiwa umeme magomeni mtaa fulani umekatika hamuwezi kushughulikia? Mnaweka urasimu hadi kwenye njia za kutoa taarifa?
 
Hata mimi nishawaandikia barua kimya, nilikwenda ofisini kwao jamaa mikwara mingi yaani unamuona jinsi inavyomuuma wewe kubadilishiwa tarrif
 
Hata mimi nishawaandikia barua kimya, nilikwenda ofisini kwao jamaa mikwara mingi yaani unamuona jinsi inavyomuuma wewe kubadilishiwa tarrif
ahhhh yaani inabidi tuwe wapole ,mimi wameniambia nisubiri labda baada ya mwezi.
 
Naomba kujua taratibu za kuongeza mita kwenye Nyumba yenye mita mfano Mimi MPANGAJI nahitaji mita kwenye Chumba changu
 
Hiyo ndio taratibu mkuu lazima tuje tukukagua maana wapo wanaoiba umeme halafu wanaomba kuwa tarif 4 ili kuhalalisha hilo
sawa pamoja ndio utaratibu lakini ndio naambiwa labda baada ya mwezi ndio watakuja;kweli ndio Tanzania ya Viwanda hii
 
Mtu unalipoti tatizo kwa haraka zaidi kuepuka madhara unayoweza yapata kutokana na hitirafu ya umeme lakini cha kushangaza siku ya nne Leo tatizo bado lipo palepale,unaenda ofisini kwao wanakuambia mafundi watakuja lakini wapi ,unapiga emergence stori ni zilezile siku ya nne Leo sina umeme da aisee is so painful,Hivi hawa Tanesco wa maeneo mengine wapo kama hawa wa Songea au huko kungine kuna unafuu kidogo?
 
Hivi tanzania ya viwanda tutafika kweli kama umeme wa kuwasha taa tu ni mtihani viwanda sindiohatari
 
pole sana wanaleta za kujuana sana hawa jamaa Kaleman afik na huko..
Yaani ni shida sana mkuu unapiga simu anapokea mdada kwa bashasha utafikiri fasta tatizo litaisha lakini wapi ,Leo nimeshindwa kwenda hata kanisani maana siwezi nyosha nguo,inasikitisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…