Naomba kujua taratibu za kuongeza mita kwenye Nyumba yenye mita mfano Mimi MPANGAJI nahitaji mita kwenye Chumba changu
Taratibu ni zote kama ambavyo ukifungiwa mita ya kwanza sharti isiwe na deni na kama sio yako upate idhini na mmiliki
 
Waambie nyumba inataka kuwaka moto ndo utawaona hapo la sivyo utasubiri sana.
 
Panda kwa manager wao, natumaini utapata huduma haraka.... bado kuna tatizo la uzembe kazini maana kama tatizo lipo nje ya uwezo wao walitakiwa wakupe taarifa na pia watafute njia mbadala.
 
Sitoi no kila siku mnachukuwa namba zangu na hakuna la maana linalofanyika leo imebidi nikafanye kazi zangu Dar.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]


Mkuu.... Naona hawa jamaa wamekuvuruga sana
 
Hao jamaa ni kuungana na kuing'oa nguzo kisha kuwapelekea ofisini kwao.
 
Mimi ni naishi Tunduru mkoa wa Ruvuma. Ushauri wangu kwenu juu ya KULIPIA UMEME KWA MWEZI NA SIO KWA UNIT KAMA MNAVYO FANYA.

Sababu ya kufanya hivyo ni kwakua umeme mnaozalisha hamuwezi kuuhifadhi kama wanavyo hifadhi maji, gesi au mafuta hivyo hamna sababu yakuweka mita wakati mteja asipotumia huwezi kuuhifadhi wala hakuwapunguzii gharama zakuzalisha.
Hilo likiwashinda fikirieni kuwahamasisha watu watumie umeme zaidi kwa kugeuza utaratibu wenu wasasa.

Namaanisha wale wanaotumia umeme zaidi ndio wawe wanauziwa bei ndogo kwa kumaanisha wanaotumia chini ya unit 75 ndio wananunua bei kubwa kuliko wanotumia zaidi ya unit 150
Ikiwafaa nitafuteni 0756200115 kwamajadiliano zaidi
 
Mkoa wa morogoro
Wilaya ya kilombero
Tarafa ya mlimba
Kata ya utengule

Kuna transforma limeharibika tangu mwaka jana watu wa kijiji hicho hawapati umeme msaada wenu tanesco
 
Mkoa wa morogoro
Wilaya ya kilombero
Tarafa ya mlimba
Kata ya utengule

Kuna transforma limeharibika tangu mwaka jana watu wa kijiji hicho hawapati umeme msaada wenu tanesco
Tunaomba namba yako ya simu mkuu
 

Hayo majibu umekaririshwa? Mteja anakuuliza sababu yao kulipishwa gharama ya nguzo wakati kimsingi nguzo inamilikiwa na Tanesco wewe unajibu kama umekunywa! Toa maelezo ya kina sababu

Mtu anataka umeme wewe unamlipisha nguzo! Inaingia akilini or it would make sense akawa amewakopesha fedha za hiyo nguzo halafu akaweza kulipwa hiyo gharama kwa kupewa units za umeme kidogo kidogo kwa muda mtakaokubaliana lakini kulipia full cost ili hali nguzo ni mali ya Tanesco ni wizi wa mchana! Ujinga na kukosa kujua haki za msingi za Raia ndio mtaji wa Tanesco and it’s totally unfair and nobody from Tanesco or the Ministry of Energy has moral legitimacy to clarify this abnormality.
 
Tunashukuru kwa lugha hiyo uliyotumia. Nguzo ni moja ya kifaa kinachphitajika kumfungia umeme,waliopo ndani ya mita 30 hawalipii nguzo bali waliozidi hapo wanachangia nguzo,lau kama ungelukuwa unazingatia gharama za uwekezaji kwenye nishati nadhani ungetuelewa mapema
 
Tanesco tafadhar nipo Iringa Mufindi kinegembasi nina shida ya umeme tangu mwezi wa 10 mwaka jana mita ilikufa nimejaribu sanaaaa kufatilia ila adi naandika apa leo jibu ni kua mradi wa Umeme vijijini Upo chini ya REA kwaio hao jamaa hawana mita tangu mwaka jana adi leo asa kweli au si kweli sielewi na Transifoma yao ndio iliua mita zetu sasa angalia hili pia
 

Usijifiche kwenye lugha jibu swali hata hiyo gharama ya service line ya kawaida ndani ya mita 30 toa maelezo kwa nini wateja walipie kwa sababu ni mali ya Tanesco pamoja na mita.

Mteja hawezi kulipishwa gharama na bado inakuwa ni mali ya Tanesco inaingia kwenye akili kweli ? Mteja anapaswa alipie umeme ambao ndio anatumia tu . Lazima mtoa huduma afikishe kwa mteja pasipo kumlaszimisha achangie hiyo kuchangia it’s not on the basis of willing buyer and willing seller ila tu kwa sababu ya monopoly you simply dictate the terms which are not negotiable.

Katika uhalisia Tanesco walipaswa kuunganisha wateja wanajitokeza na hizo gharama should have been part of the cost of service. In fact gharama umeme wa Tanesco does not reflect the cost of service and that is the problem the cost is politically determined huku mkijidanganya kutoa huduma nzuri at a low cost hiyo kitu hakuna duniani.

Hayo maswali usiyajibu kwa mihemko ya kutokujua jiongeze na jipange kutoa majibu yenye mashiko. Shirikisha Economists na wataalam wengine. You should take on board diversity of the readers na wala lugha isiwe issue hapa! Zamani before the advent of Luku wateja walikuwa wanalipia meter deposit and it was actually calculated as three months billing basing on the projected customer load sasa hii ya kulipia service ya kibaguzi sijui REA 27,000 na wengine 177,000 kwa vijijini what is the justification ligicaly?

Elimu yahitajika and this is the forum!
 
Tunashukuru sana kwa mapendekezo yako, haya yote tunayokueleza yapo kwenye kanununi za umeme pamoja na sheria ya umeme ya mwaka 2008 hivyo unaweza ukajiuliza swali dogo kabisa je umeme tunaopeleka maeneo mbalimbali ikiwewa vijijini kwa gharama kubwa ya uwekezaji kwa lengo la kuamsha uchumi wa maeneo hayo ingekuwa kampuni binafsi ingeweza? Shirika hili la Uma linalenga zaidi kuleta maendelea kupitia miradi yake pamoja na gharama kidogo tunazowatoza wananchi,

Kumbuka kazi ya Tanesco ni kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme hivyo nguzo ni kifaa kimpjawapo kinachpweza kisambaza umeme na mteja anapswa kuchangia mpaka nguzo mbili zikizidi hapo anahiyari ya kusubiri mradi umfikie au kulipa mwenyewe na baadaye wengine wakifungiwe kupitia nguzo hizo atapewa fidia hii ni kwa mujibu wa electricity regulations
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…