Nimeripoti tatizo la nguzo kutaka kuanguka watu wa emergency wakaja kuona na kuthibitisha kweli nguzo imeshikiliwa na waya mmoja wa umeme unaoingia kwenye moja ya nyumba zilizo chukulia umeme kwenye hiyo nguzo. Mafundi walikuja kuona wakasema wanaenda kufuata nguzo Ila hii ni wiki ya tatu hajarudi. Nimepiga simu customer care wanasema hamna nguzo wakati wiki hii niliona mafundi wenu walikuja kucheki transformer wakiwa na nguzo, nimeambiwa kuwa hizo nguzo ni za wateja wapya kwahiyo Sisi wa zamani hatuna thamani.
Mnataka kutuunguzia nyumba aisee maana hii nguzo muda wowote itaanguka.
Hili tatizo lipo kinondoni mkwajuni, sasa iweje watu wanalipia umeme halafu msema nguzo hamna na hamjui lini zitawasili na bila shaka sidhani hata kama mnaweka rekodi ya sehemu zote zinazo hitaji nguzo ili zikija mkaweke
Mwisho waambieni customer care representatives wenu wajifunze kwa customer care wa mitandao ya simu. Yani wana huduma mbovu mbovu hamna mfano. Mtu unapiga simu anaongea na wewe Kama hataki, Tena ukipiga usiku ndio kabisaaa mwingine anakuwa busy kupiga stori na mwenzake