Mbona mwanzo ulivyoambiwa ulikataa??*TAARIFA KWA UMMA*
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wote wanao tumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, 2018 TANESCO itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa Taasisi za Serikali.
TANESCO ikiwa miongoni mwa Taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, Kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki.
Serikali kwa kushirikiana na Wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike kwamba, TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa Taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio, baadhi ya Taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji.
TANESCO inapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka.
TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’
Kwa mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook Tanesco Yetu
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
MACHI 27, 2018
*TAARIFA KWA UMMA*

Nami pia ningependa kujua hili...Tunashukuru kwa taarifa.......je hii ina impact gan kwa Maxcom na Selcom vendors.
Kwahiyo mnatuhakikishia sie wauzaji wa luku kupitia mashine za selcom na Maxmalipo hakutakua na mabadiliko?Huduma zitaendelea kuwepo kama kawaida, swala la impact kwa washirika wetu ni la ndani ni lanahusu wao na sisi
Sijasema sio taarifa kamili,Hio ni taarifa kamili, toka TANESCO
Mteja huyu alete taarifa kwa maandishi uchunguzi utafanyika kisha taarifa itatolewa na maamuzi kama ni tanesco au yeye.mara kadhaa ikitokea shoti tunadhani ni tanesco kumbe wakati mwingine ni tatizo na kwa mteja kuweka matumizi zaidi ya alichoombaTanesco kuna matatizo makubwa ya kupungua kwa umeme maeneo ya DSM. Juzi kuna mango maarufu meneo ya salasal ameunguliwa na duka kubwa LA jumla likiwa n Mali za thamani kubwa. Hebu tuelezeni mini kinaendelea
Ndugu hiyo kauli ya "umeme ndani ya siku saba" hata mie ilinihadaa na nikahadaika. Nimelipia nasubiri umeme badala ya siku saba sasa inaelekea " siku saba mara sabini".TANESCO Makao makuu wafuatilie mwenendo wa maofisa wao walioko kwenye tawi lao la Mbezi, kutokana na huduma zisizodhirisha za ofisi hiyo.
Kuna wateja ambao wameshalipia kuwekewa umeme kwa zaidi ya miezi sita lakini hata survey haijafanyika. Kila wanapofuatilia kufanyiwa survey wanaambiwa kuwa hakuna usafiri. Kuna ambao walikuwa tayari kutumia usafiri wao, na wengine hata kukodi magari, lakini wakajibiwa kuwa hairuhusiwi kutumia usafiri binafsi. Sasa wateja hawa waende kwa nani ? Nakumbuka Waziri wa nishati alisema siku kadhaa zilizopita kuwa mtu anayekamilisha malipo ya kuwekewa umeme awe amewekewa ndani ya siku saba.
Maofisa hawa wanafanya makusudi ili serikali ichukiwe na wananchi. Tafadhali suala hili lifuatiliwe, la sivyo tutaliwasilisa kwa Mheshimia Reais wa Jamhurimya Muungano wa Tanzania baada ya sikukuu ya Pasaka.