Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,968
- 8,139
WATUMIAJI WA UMEME WA LUKU CHUKUENI TAHADHARI MAPEMATumepokea taarifa kwa hatua zaidi
Wakuu natumaini mmeshinda salama.
Kwa habari nilizozipata leo ni kuws mkataba kati ya Tanesco na Maxcom (MaxMalipo) wa kuuza token za umeme (LUKU) utakwisha mwisho wa wezi huu na hakuna dalili kwamba wataongeza mkataba siku za karibuni.Ikumbukwe kuwa Maxcom ndio wenye mkataba wa kuuza umeme kwa wateja wa Tanesco na hivyo wao pia wameingia ubia na makampuni ya simu kama Tigo, Voda n.k na hivyo kuisha kwa mkataba wa Maxcom ina maana hutaweza pia kununua kwenye simu.
Hii ina maana kuwa, baada ya tarehe 31 March ukitaka umeme lazima uende katika office ya Tanesco ili kupata huduma hii. Hata wale vendors maarufu wa Tanesco waliopo mitaani hawatakuwa na uwezo wa kuuza umeme. Hivyo wakuu naomba kuwapa tahadhari kwa wale wenye sehemu za biashara wanaotumia LUKU na watumiaji wote wa LUKU hata wa majumbani mchukue tahadhari mapema kabla hali ya taharuki haijazuka ukizingatia sikukuu hii ya pasaka inakuja hakuna ambae angependa kukaa giza siku kadhaa kisa ameshindwa kununua LUKU.
Mpaka sasa hakuna suluhisho lililofikiwa zaidi ya kuwa LUKU itauzwa katika ofisi ya Tanesco na hivyo nawaasa ndugu zangu mnunue kuanzia leo na kesho umeme wa kutosha hata week kadhaa maana kuna kadhia inakuja hapa mbeleni.
Ukiupata ujumbe huu tafadhali usiwe mchoyo mshtue na jirani yako.
Mtag rafiki yako ili ajue asije kukuwekea jam nyumbani kwako kucharge simu au kupiga pasi.
Asanteni
Hii taarifa hapo juu ina ukweli? Tuambieni ukweli ili tuchukue tahadhari mapema
TANESCO