TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nimeandika nikafuta
Nikaandika nikafuta
Nimeogopa kuitwa mc.......i
Ngoja niseme kidogo tu make inakera.
Kama mnania ya kutatua kero zote za umeme .narudia tena
Kama mnania ya kutatua kero zote za umeme.
Mruhusu kuwepo na makampuni binafsi ya kutoa Huduma ya umeme. Kama zilivo kampuni za simu.
Mtakuwa mnakagua nyumba inayojengwa ili kuomba mtoe Huduma ya umeme.
Huduma zitakuwa nzuri kwan kampuni ikizingua MTU anahamia kampuni nyingine no kubembelezana.
Leo hii MTU akiweka umeme anatangaza utadhani kapata ajira.
Kuhusu Huduma ni mbovu sema tu hamna jinsi.
Ndugu mpendwa mteja fursa ipo wazi kwa mujibu wa sheria hivyo kama wapo wafate taratibu kwa kuzingatia sheria ya umeme ya mwaka 2008 na kanuni zake
 
Naomba kuuliza, hivi rimoti ya kuingizia umeme ikiharibika au kupotea unaweza kupata nyingine na kwa utaratibu gani? Nimekuja nimekuta mpangaji wangu kahama na rimoti haionekani na alikohamia sijui sasa nafanyaje kuingiza umeme?
Fika ofisi ya eneo lako na loss report kutoka polisi na barua yako ili kulipia na kupatiwa nyingine. Kama ikiharibika yenyewe unapatiwa bure lakini wataalamu wetu wanaikagua kwanza
 
Fika ofisi ya eneo lako na loss report kutoka polisi na barua yako ili kulipia na kupatiwa nyingine. Kama ikiharibika yenyewe unapatiwa bure lakini wataalamu wetu wanaikagua kwanza
Asante sana!
 
Huku Goba Tegeta A umeme ni mdogo ( Voltage)..
Yaani simu ya kuchaji masaa 2
Unachaji usiku kucha
Na asubuhi inakuwa haijajaa tofauti na hapo awali
Hebu ongezeni transformer..
Maana toka 2010 mpaka leo transformer ni hizohizo
Na zikizidiwa zinajibu (zinabutuka).....
Na wakazi wanaongezeka sana pamoja shughuli za kibinadamu km viwanda vidogo
Tanesco Kimara (Mbezi Mwisho) hebu chukueni hatua...
 
Ndugu mpendwa mteja fursa ipo wazi kwa mujibu wa sheria hivyo kama wapo wafate taratibu kwa kuzingatia sheria ya umeme ya mwaka 2008 na kanuni zake
Point ya msingi boresheni Huduma zenu.kwan MTU nguzo iko mbele ya nyumba unakaa mwaka hujapata Umeme .
 
Habari yako afisa wa Tanesco unayetuhudumia kupitia hii platform. I hope you are fine.

Siku ya leo (jumapili) mchana nilikuwa nimewasha TV, baada ya muda umeme ukakatika. baada ya umeme kurudi TV haitoi mwanga tena japokuwa taa ya power button inaonesha TV ipo on.

Nimejiuliza maswali kadhaa, mojawapo ni hili: nani yupo responsible wa uharibifu huu? Ni mimi niliyewasha Tv au walipkata umeme? Na je ninyi Tanesco mna utaratibu gani endapo matatizo ya kukatika umeme yameleta madhara kwa wateja?

Nimeuliza hivyo kwa sababu; kwa wiki kadhaa hapo nyuma umeme wenu ulikuwa unakosa nguvu hivyo vitu yangu vyote ambavyo vipo vulnerable to power instability nilivi switch off including hii TV iliyopata damage. Nimeanza tena kuvitumia baada ya kuona hali imetengamaa lakini matokeo yake ndo hayo.

Sasa naomba kujibiwa maswali yangu ili nijue tunafanya nini kuhusu hili. Asante
 
Habari yako afisa wa Tanesco unayetuhudumia kupitia hii platform. I hope you are fine.
Siku ya leo (jumapili) mchana nilikuwa nimewasha TV, baada ya muda umeme ukakatika. baada ya umeme kurudi TV haitoi mwanga tena japokuwa taa ya power button inaonesha TV ipo on.
Nimejiuliza maswali kadhaa, mojawapo ni hili: nani yupo responsible wa uharibifu huu? Ni mimi niliyewasha Tv au walipkata umeme? Na je ninyi Tanesco mna utaratibu gani endapo matatizo ya kukatika umeme yameleta madhara kwa wateja?
Nimeuliza hivyo kwa sababu; kwa wiki kadhaa hapo nyuma umeme wenu ulikuwa unakosa nguvu hivyo vitu yangu vyote ambavyo vipo vulnerable to power instability nilivi switch off including hii TV iliyopata damage. Nimeanza tena kuvitumia baada ya kuona hali imetengamaa lakini matokeo yake ndo hayo. Sasa naomba kujibiwa maswali yangu ili nijue tunafanya nini kuhusu hili. Asante
Tafadhali wasilisha taarifa yako kwa maandishi uchunguzi utafanyika na kutoa taarifa itakayosaidia kufanya maamuzi
 
Tafadhali wasilisha taarifa yako kwa maandishi uchunguzi utafanyika na kutoa taarifa itakayosaidia kufanya maamuzi
Taarifa nawasilisha wapi? Naomba address. Naishi Dsm
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU KWENYE LAINI YA ILALA KURASINI

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Temeke inapenda kuwajulisha wateja wa mkoa huo kuwa kumetokea hitilafu kwenye laini ya kurasini kufuatia tatizo la under frequency

Mafundi wako kwenye eneo la Tukio kurekebisha hali hiyo

MAENEO YANAYOATHIRIKA:

kurasini,malawi cargo,transcargo, gate no 3, nhif, unifreight, trh,baraza la maaskofu,uhamiaji, baadhi ya maeneo ya Mbagalana maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Kwa mawasiliano

Dawati la Dharura Temeke: 0712052720, 0758880155, 0732997361

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
 
Yaani jinsi ya kuomba kama unatumia unit chini ya 70 wanakupa form unajaza wanakupa zile vocha unajaza unakaa hata zaid ya mwez umeme hujaisha unafanyaje...
 
TAARIFA : Kuna nguzo imeinama na Nyaya za umeme zipo chini sana usawa wa kichwa cha mtu mfupi na ni hatari kwa jamii. Eneo lenyewe ni Tegeta karibu na Ladi Hoteli.
 
TAARIFA : Kuna nguzo imeinama na Nyaya za umeme zipo chini sana usawa wa kichwa cha mtu mfupi na ni hatari kwa jamii. Eneo lenyewe ni Tegeta karibu na Ladi Hoteli.
Tegeta eneo gani na namba yako ya simu mpendwa mteja
 
Kutokea Tegeta kwa Ndevu unashuka na barabara kupitia kituo cha polisi then uliza Ladi Hoteli then trace ile sehemu ya tatizo from Ladi Hotel. My nr. 0766805757. Actully mimi ni mpitanjia na siyo mteja. Na kwa vile nimeiona hiyo hatari nikaona ni busara kutoa taarifa Tanesco.
 
Mbezi Kimara, Msuguri, Saranga, Malamba kwa nini hatuna huduma ya umeme tokea saa 6 mchana?! Ni sababu gani hasa mnapenda kutukatia umeme takriban kila siku?
 
Back
Top Bottom