TANESCO, naomba muimlike Mbeya Jiji na Usumbufu na Kutojali kwa Watu wenu!
Sasa hivi ni mwezi wa 3 tangu nafuatilia Kuunganishiwa Umeme ninachokutana nacho ni kama siyo Mtanzania Vile na kama naomba Msaada!
Kwanza Form ya Mkandarasi ilikaa Ofisini kama miezi miwili bila kuja Kupima Watu wa Planning, nilikomaa nao, wakaja baada ya hiyo miezi miwili!
Haya limekuja Swala la Kulipia, hawataki kunitumia Ujumbe kuwa inatakiwa nikalipia kiasi gani, hiyo nimefuatilia zaidi ya mwezi sasa hakuna lolote linaloendelea! Na Ukiangalia eneo langu hata Nguzo haihitajiki!
Sasa Tanesco mnataka nini toka kwa Wananchi wanyonge. Ujinga zaidi hawataki niiingie nikaonane na Meneja wa Mkoa nimueleze shida yangu!
Nini Kimetokea mpaka mnatudharau hivi, mbona kipindi cha Mhongo Utiifu kidogo ulikuwepo?
Nimewapa Wiki hiii tu, Upumbavu huu Ukiendelea najua nitakako kwenda Kureport mwenyewe, this is too much.
 
Naomba no ya Tanesco makao makuu nina shida tangu jana umeme hauingii kweny mita tafafhali naomba msaada
 
Nipo Vwawa Mbozi Songwe. natumia unit chini ya 70 kwa mwezi nataka Tariff zero chenga ni nyingi mpaka nimekata tamaa naomba mwongozo please au nipe namba ya waziri naona kama yupo serious sana anaweza kunisaidia.
 
Mkuu hata mimi imefika kipindi nahitaji namba ya waziri,maana tanesco ni uozo mtupu
 
Ulasimu ni mwingi mnno hasa tanesco Kigamboni. Kisingizio ni nguzo. Zikiwepo huuziwa kwa wenye pesa tu. Ninyi mlio lipia pasipo toa cha juu kwa meneja utasubili sanaa..
 
Ulasimu ni mwingi mnno hasa tanesco Kigamboni. Kisingizio ni nguzo. Zikiwepo huuziwa kwa wenye pesa tu. Ninyi mlio lipia pasipo toa cha juu kwa meneja utasubili sanaa..
Aisee haya Matatizo ni Nchi Nzima. Mimi ni Mbeya hapa, Ujinga na Ukiritimba mwendo mmoja!
 
Aiseee na nunua umeme ina goma wana nambia nahitaji kupata key change sasa sijui wana maanisha nini
 
Mkowa Wa kagera wilaya ya Karagwe Umeme unasumbuwa sana, yani afadhali ya mikowa mengine.
 
Ulipewa Account ya bank au ya kwao?
 
Baada ya kulipia ni muda gani huunganishiwa umeme ninapoishi hakuna haja ya nguzo mpya kuna nguzo ya jirani hapa?
 
Sitaacha kuwashukuru kwa kazi mnayoifanya maana ni ngumu na changamoto kibao japo bado Niko njia panda. Niliwahi kuuliza humu suala nikajibiwa vizuri sana na hadi simu nikapigiwa lakini ukweli hadi sasa sioni dalili. Swali ni hivi; Kijiji cha MABUYE kata KASSAMBYA Wilaya ya MISSENYI Mkoani KAGERA ni lini kitapatiwa umeme wa REA maana vijiji vilivyo kizunguka karibia vina umeme ila chenyewe na vitongoji vyake vya KIJUKA, MABUYE, RUHAMA na ITALA vimebaki katikati tu bila umeme. Naomba kujulishwa juu ya hili. Hivyo naomba kujulishwa kama kimo au hakimo, na kama kimo ni lini kutapatiwa? Nitashukuru kujibiwa.
 
Kitongoji cha Kemambo Kijiji cha kewanja Nyamongo Tarime mnaweka lini umeme.
 
Ulipewa Account ya bank au ya kwao?
Walinipa account wao wenyewe nika deposit pesa. Baada ya hapo nilirejesha bank slip hapo TANESCO ndipo nikaambiwa nisiende tena mpaka nitakapopigiwa simu. Ila kwa dokezo tu niliambiwa kuna "fast track" nadhani umenielewa
 
Kuna uvumi unaendelea mtaani kuwa Tanesco wanaplan kuwarudisha watu wrote kwenye tarrif 1. Hili lina ukweli?
 
Walinipa account wao wenyewe nika deposit pesa. Baada ya hapo nilirejesha bank slip hapo TANESCO ndipo nikaambiwa nisiende tena mpaka nitakapopigiwa simu. Ila kwa dokezo tu niliambiwa kuna "fast track" nadhani umenielewa
Fast track ndyo nini?
 
Kuunganishiwa huduma ya umeme, malipo yalifanyika Juni 2016, mahitaji ni pomoja na nguzo moja. Hivi hadi miezi minne au zaidi ndo nipate huduma? Nipo Iringa manispaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…