Mara baada ya kusimika nguzo kwa wateja hicho ndio kinafata.kuhusu mita tunaendana na mabadiliko ya technolojia huku tukozingatia ubora na usalama mita zetu
 
Mara baada ya kusimika nguzo kwa wateja hicho ndio kinafata.kuhusu mita tunaendana na mabadiliko ya technolojia huku tukozingatia ubora na usalama mita zetu
Sorry niulize tena nilisikia hizo meter za remote luku ikiisha unatakiwa uingeze token ndani ya meter 10 sasa kwa tuliojenga huku kibamba nyumba moja na nyingi ni zaid ya mita mpk 30 umeme ukiisha kuna njia mbadala??? pia nashukuru kwa jibu letu la kwanza
 
Baada ya kusubiri siku 30 za umeme kuunganishiwa zikapita, je!hatua zipi nifuate?
 
Kwanza Tunashukuru kwa kutuwekea platform ya kueleza kero zetu. Kuna huu umeme wa REA ambao unasambazwa vijijini. Kijijini kwetu Nyakunguru kata ya kibasuka wilaya ya tarime umeme uliletwa hadi centre ya kijijij ilipo shule ya msingi Nyakunguru ,ambapo ni katikati ya kijiji na kuishia hapo bila kufikia nusu nyingine ya kijiji eneo ambalo lina nyumba za kisasa. Wakazi wa hili sehemu ambayo haikupata umeme walipohoji waliambiwa ni eneo la Mgodi. JAMBO AMBALO SIYO KWELI.Kwani eneo hilo mgodi wenyewe umechimbia wakazi wake visima kadhaa vya maji na unaendelea kuvihudumia na hawajawahi kueleza wakazi hao kuwa hilo ni eneo lao. Eneo hilo lina shule ya msingi inaitwa Nyamichale ipo kitongoji cha Nyamichale.Naomba kujua kama kweli kuna zuio la Mgodi wakidai eneo ambalo tunamiliki kihalali ni lao au mna sababu zenu za kiutendaji za kutopeleka umeme eneo hilo
 
Tumepokea swala lako kwa ufatiliaji mpendwa mteja
 
Unaweza kuweka betri na kuingiza umeme wako
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;
 
Tumepokea swala lako kwa ufatiliaji mpendwa mteja
Kwasasa kwenye REA III tunataraji kufikisha umeme kitongoji cha Itandula kijijini hapo Nyakunguru. Na utaratibu huu utaendelea hadi vitongoji vyote vipate umeme
 
Walau Leo nimeridhika na majibu yenu kuhusu usambazaji Wa nguzo.
Kikawaida yaweza chukua muda gani mpaka kiwekewa wire?
 
No. 4 JINSI YA KUFIKIA MAKAZI YA MTEJA;

USHAURI.

Kwa kuwa wateja wengi wa mijini wako kwenye maeneo yaliyopimwa na Serikali; ila mitaa haina majina, na nyumba hazina namba; tunawashauri mpate nakala ya ramani kutoka mamlaka husika, ili mteja anapowahitaji mfike kwenye makazi yake, awatajie 'Eneo, Block number na Plot number':

.... ambayo kimsingi mnazo kwani alizionyesha wakati anaomba kuunganishwa.

Mtakomboa wakati wenu na rasilimali zenu kuwafikia, hasa usiku, kwani mitaa mingi haina hata street lights.

[emoji120] [emoji120]
 
Ndugu mpendwa mteja zipo hatua tunazochukua kumuwezesha mteja kujisajili na kutoa au kupata taarifa moja kwa moja kwetu.kitu kipya kipo njiani stay tune
 
Npo Iringa Mafinga nina miezi minne tangu nilipie hadi leo sijawekewa umeme
 
Kibugumo Kigamboni umeme umekatika, nimetoa tu taarifa. Na kila umeme ukikatika nitakujulisha, ili uone kama hiyo ni hali ya kawaida umeme kukatika so frequently and hapharzadly
 
Kwasasa kwenye REA III tunataraji kufikisha umeme kitongoji cha Itandula kijijini hapo Nyakunguru. Na utaratibu huu utaendelea hadi vitongoji vyote vipate umeme
Ninashukuru kwa kuonyesha mnajali angalau kwa ufuatiliaji na kutoa feedback. Tunaomba wakati umeme unaenda itandula, kwenye mikakati yenu mtusaidie tu wakazi wa eneo linaloitwa nyakato ambako ni junction ya kuelekea itandula muwawekee huduma ya umeme hapo kwani ni eneo ambalo watu walposikia umeme unakuja wakajenga nyumba nzuri nzuri na wanasubiria umeme na kwa kuwa ni njiani kwenda itandula naamini mtaridhia ombi lao. Na hii itasadia kwani hapo kuna mashine za kusaga nafaka ambako watu wanalazimika kutumia diesel kuhudumia hizo mashine za kusaga na hii inasababisha running cost kuwa kubwa na kufanya wawekezaji wapya kutaka kuhamishia miradi yao nyakunguru centre.Nashukuru kwa kusikiliza kilio chetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…