TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Zile nyimbo na ngonjera za 'miundo mbinu chakavu' zimeshachuja na hazina mashiko tena katika zama hizi za Magufuli. Sina shaka Kigamboni ndio inayoongoza kwa ukatikaji wa umeme hovyo hovyo katika jiji la Dar, kwa wiki umeme unakatika mara tatu hadi nne kutegemea na siku hiyo wameamkaje; shida ni nini, mbona ni Kigamboni tu? Nani awajibishwe?
 
Wewe jamaa kwa kulalamika balaa. Ni muda mrefu sasa sija-experience umeme kukatika huku Kigamboni, unakatika mara chache na kurudi baada ya dakika chache.
Acha masikhara, we upo sehemu gani? Kuanzia Maweni mpaka Kibugumo tunaadhibiwa kila siku, hapa yenyewe tupo gizani, upo wapi wewe?
 
Back
Top Bottom