Tumepokea kwa hatua zaidi
Wanachagua wa kuwajibu mkuu, nimepost zaidi ya mara nne. Jana nimevizia wakiwa hewani, lakini hawanijibu. Ukitaka ujibiwe haraka weka post zinazilosrma, "Nanjilinji mtaleta lini umeme." Yaani maswali ya ujumla tu, sio matatizo yanayolenga ofisi.
 
TANESCO IMEGOMA KUTULETEA UMEME SHULE YA SECONDARY MAGUBIKE?

MIMI NI MKAZ WA KIJIJI CHA MAGUBIKE NAPATA SHIDA SANA KUELEZA AMBAPO KIJIJI CHA MAGUBIKE KATA YA MAGUBIKE WILAYA KILOSA BARABARA YA DODOMA.SHULE HAINA UMEME MWAKA WA NNE KIJIJI KINA UMEME ILA SHULE HAINA UMEME EBU TEMBELEEN HAPO MUONE WANAFUNZ NA WAFANYAKAZ WANAVYOPA ADHA YA KUKOSA HUDUMA HIYO NYETI KWA AJILI YA KUONGEZA UFAULU WA SHULE HIYO.
HII POST YA 2 HAIJAJIBIWA.
 
TANESCO
Mimi nataka nifungiwe ile tarif ya watumiaji wadogo wa umeme, wanaotumia umeme chini ya Unit 75 kwa mwezi.

Je nikifika TANESCO, niseme nataka niwekewe Tarif Ipi ?

[emoji117] Naomba jibu tafadhari.
 
Mpendwa mteja wetu kama ambavyo tumewahi kuwlezea swala hili ni kwamba ili mtu,tasisi au kikundi kipate umeme kinapaswa kuhakikisha wiring imekamilila kisha kufanya maombi ya umeme kwa eneo ambalo miundombinu ya umeme imefika.je ninyi mliomba umeme?tunaomba jina na namba ya simu ya msimamizi
 
Je umeshafungiwa umeme?zipo kanuni na taratibu za kuwaweka wateja kwenye makundi mbalimbali ya utumiaji wa umeme hivyo unapofungiwa tu unakaa kundi sahihi
TANESCO
Mimi nataka nifungiwe ile tarif ya watumiaji wadogo wa umeme, wanaotumia umeme chini ya Unit 75 kwa mwezi.

Je nikifika TANESCO, niseme nataka niwekewe Tarif Ipi ?

[emoji117] Naomba jibu tafadhari.
 
Je umeshafungiwa umeme?zipo kanuni na taratibu za kuwaweka wateja kwenye makundi mbalimbali ya utumiaji wa umeme hivyo unapofungiwa tu unakaa kundi sahihi
Sawa.
Mimi nataka nifungiwe umeme kwenye nyumba mpya inayowekewa umeme kwa mara ya kwanza.
Ikikamilika nitawajulisha TANESCO kuwa nahitaji ule wa matumizi madogo.
 
Sawa.
Mimi nataka nifungiwe umeme kwenye nyumba mpya inayowekewa umeme kwa mara ya kwanza.
Ikikamilika nitawajulisha TANESCO kuwa nahitaji ule wa matumizi madogo.
Mkuu hapo ni lazima kwanza ukae kwenye kundi la tariff 1 baada ya miezi 3 au 6 ndiyo watakuweka katika kundi la tariff 4 kama utakuwa unasifa za kuwa katika kundi hilo
Na sasa hivi wanachofanya nikuwatoa wateja wote kwenye tariff 4 na kuwarudisha kwenye tariff 1
 
Sawa Mkuu
 
eneo husika ni moja ya maeneo yatakayopatiwa umeme kupitia mradi wa ujazilishi (Densification) kwa mkoa wa Morogoro. Magubike ipo wilaya ya kilosa lkn kwa Tanesco inahudumiwa na wilaya ya Mvomero (Turiani)

Tunawashauri wasubiri utekelezaji wa mradi. Lkn pia mzee wa magumashi washauri uongozi wa shule walete maombi rasmi ya kutaka umeme ili tuwajibu
 
Naomba kujua namba za kuulizia bili
*PATA ELIMU KUTOKA TANESCO*

*JE UNATAKA KUJUA BILI YAKO YA MWEZI NA NAMBA YA KUMBUKUMBU YA KULIPIA ?*

*HII NI KWA WATEJA WENYE MITA ZA KUSOMA TU SIO LUKU*

*BASI FATA MAELEZO YAFUATAYO*

[emoji841]fungua sehemu ya ujumbe (meseji) kwenye simu yako

[emoji841]Andika neno
*TANESCO* acha nafasi,

[emoji841] Andika neno *BILL* AU *BILI* acha nafasi

[emoji841]Andika namba yako ya utambulisho ya mteja (ipo kwenye bili yako imeandikwa *cust ref*)

[emoji841]Tuma ujumbe huo kwenda 15200


[emoji841]Utapata ujumbe wa kiasi cha bili unachopaswa kulipa na *Control number* itakayoruhusu kulipa kupitia mfumo wa Serikali (GePG)

*Mfano*

TANESCO BILL CUST REF

*KWA KINGEREZA*

TANESCO BILL 85011403

*KWA KISWAHILI*

TANESCO BILI 85011403

Tuma kwenda
*15200*

*TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO*
 
Nipo arusha kimandolu tindigani.

Kila ikifika jioni mida ya kwanzia saa mbili hivi umeme huwa unakatakata. Na tatizo hili limeanza tokea nifungiwe luku mwaka huu. Kabla ya hapo hakukuwa na hii hali. Tatizo ni nini?
 
Nipo arusha kimandolu tindigani.

Kila ikifika jioni mida ya kwanzia saa mbili hivi umeme huwa unakatakata. Na tatizo hili limeanza tokea nifungiwe luku mwaka huu. Kabla ya hapo hakukuwa na hii hali. Tatizo ni nini?
Simu yako,namba ya mita na namba ya taarifa fafadhali
 
Hivi tanesco hili suala la kuhamishwa tariff halipo ndani ya uwezo wenu?mbona hamjibu sasa twende wapi kushtaki?
 
Maswali yenyewe hamjibu
 
Kazi yenu ni nzur sana but karagwe Tanesco imekuwa ya shida sana

Kila wakati ni umeme umekatika,bila ata taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…