Tutakufungia umeme hauna haja ya kuwa na hofu wala kudhani tunahitaji chochote.hii ni haki yako na sisi ni wajibu wetu.upo kwenye orodha yetu
Hii namba ya Eng.Muyanja mkuu wa kanda ya Pwani na Dar.
0784277953 mpigie ueleze shida yako maana hawa ni wasumbufu wanataka rushwa tu.
 
Ulilipa kwa jina gani ,namba ya simu na tarehe ngapi tafadhali
 
Kigoma mjini ni takribani wiki 3 sasa umeme unakatika kila siku kwa msaa 3 hadi 5. Kwanini hamtangazi kuna mgao ili watu wapange shughuli zao?
 
 
Wakuu naomba mnisaidie nakuwa kama niko kisiwani. Hata humu ndani mafundi washacheki hakuna tatizo la kiufundi. Shida ni nini? Nishaenda zaidi ya mara tatu Tanesco wansema umeme mdogo. Naona ni assumptions maana mimi naona majirani unawaka!!
Why kwangu tu? Na hapa nipo gizani!!!
 
NDUGU ZETU TANESCO KILIMANJARO HASA HAPA HIMO KUNA MABADILIKO MAKUBWA YAMETOKEA HASA KWA WENYEWE MITA ZA LUKU YAAN UNIT SASA ZINATOLEWA CHACHE SANAA PUNGUFU MARA 2 YA KAWAIDA.... WANANCHI WA KAWAIDA TUNAUMIA SANA...... NIMEJARIBU KUWAULIZA OFFICE YA TANESCO HAPA NAAMBIWA KUNA UKAGUZI WA MITA ZA LUKU......... NAOMBA KUJUA HILI ZOEZ NI KWEL AU KUNA UKIRITIMBA HAPA HIMO......


UFAFANUZI PLEASE!?!
 
Naombeni msaada, nilikua nimezoea umeme kutokuisha kabisa kwenye luku maana kwa tariff 4 shiling 7500 tu zilikua zinanipatia umeme wa kutosheleza. Sasa kwa haya mabadiliko mliyotuletea huku Kilimanjaro ni tabu tupu, umeme umeisha jana mchana sikuwaza kama Jioni nikirudi kuweka mwingine ingenisumbua. Kila nilipotaka kuweka ninaambiwa error 77 nimewapigia mkanipa namna ya kuondoa hiyo error ila hakuna kilichofanikiwa nipo gizani na baadhi ya mambo kukwama, namba ya mita ni 24212097125
 
*JINSI YA KUONDOA ERROR 77 KWENYE MITA ZINAZOANZA NA NAMBA 2421...*

*ERROR 77*

Hii ni error ambayo inapatikana kwenye mita tengano maarufu kama mita za rimoti au CIU ambazo zinafungwa juu ya nguzo na zinaanza na namba ya mita 2421.....

*NINI KINASABABISHA ERROR 77*

*Error 77* inamaanisha kuwa mita yako ya kwenye nguzo na rimoti yako hazina mawasiliano hivyo umeme hauwezi kuingia. Mara nyingi inatokea unapotaka kuweka umeme baada ya kuisha unit.

*JINSI YA KUTATUA ENDAPO ITATOKEA*

Unatakiwa kuhakikisha kuwa umeme kwenye mtaa wako upo na kama nyumba yako haina umeme yaani unit zimeisha weka betri zenye nguvu kwenye rimoti yako na kisha fata taratibu zifuatazo

[emoji841]Zima switch zote za nyumba yako, *hakikisha zote zimezimwa*

[emoji841]Washa switch moja tu ya ukutani na chomeka hiyo rimoti kisha bonyeza zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako alafu tena zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako kisha bonyeza ok au enter..

*Mfano mita namba yako ni 241234567 Utafanya ifuatavyo *024212345670241234567ENTER*

[emoji841]Baada ya kubonyeza ok itaakuandikia *GOOD* apo sasa weka umeme wako kama kawaida na utapata umeme.

*ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA ZA TANESCO*

*RUKSA KUSHARE NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI*
 
Kuna uhakiki wa wateja unaendelea hivyo wateja wote wanawekwa makundi yanayoendana na matumizi yao
 
Wilaya

Eneo

Namba ya simu

Namba ya mita

Tatizo
 
Wilaya kinondoni

Eneo kawe mlalakuwa,karibu na golf course ya JWTZ

Namba ya simu 0699784611

Namba ya mita

Tatizo tunapata tatzo la under voltage mara kwa mara na nilishareport tanesco na technician wakaja warecommend phase balance ya nyumba lkn still bado tatizo lipooo halishii bado nna video nimerecord zA jinsi tatizo lilivyo ika hapa zimegoma maaana file ni kubwa sanaaa
 
Ndugu zangu Tanesco Yetu,

Salaam.

Nina concern mbili.
1. Kuhusu upatikanaji wa Luku statement
Nimeenda Tanesco Wilaya ya Kigamboni pale Kisiwani kuhitaji kupata Luku statement ili niweze kufuatilia malipo yangu. Kwani Nimeona Kuna tatizo katika ununuzi wa Luku. Ninalipa Hela nyingi kununua umeme wakati matumizi yangu ni madogo sana. Kwa Mwezi mzima situmii unit 60.

Cha ajabu ni Kuwa na kilichonishangaza ni kuambiwa siwezi kupata statement hadi niandike barua ya kuomba hitaji langu kwa meneja. Hii Ilinishangaza Kidogo. Je huu ndio utaratibu wenu kwa Wilaya hii ya Kigamboni? Au ni utaratibu wa Nchi nzima? Na Kwanini mteja nilazimike kuandika barua ya maombi? Kwanini isiwe mkaiga Mfumo wa mabank kutoa statement bila usumbufu. Naomba ufafanuzi.

2. Pili ni Kuwa Tanesco Yetu mna utaratibu wa kumpandishia mtu kutoka matumizi madogo kwenda makubwa automatically akiwa anatumia umeme zaidi ya unit 75 kwa Mwezi bila hata kumjulisha. Lakini wakati huo huo mtu anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa Mwezi hamshushi kutoka juu kuleta chini. Hapo mnahitaji mteja alalamike na kuandika kuomba kupelekwa matumizi madogo. Swali langu Kwanini inakuwa ngumu kwenu kufanya hivyo? Hamuoni kama mnawanyonya Wateja ambao matumizi yao ni madogo na nyie mnamlipisha kiwango cha daraja la juu.

Naomba kupata ufafanuzi wa mambo hayo mawili.
 
Habari ndugu.

Pole sana kwa changamoto hio. Ndugu mteja unaweza kupata statement yako. Je tunaweza kujua unataka kuona manunuzi pamoja na kitu gani zaid mfano. Njia ya manunuzi iliotumika na muda na tarehe.

Je unataka kuona kwa kipindi gani hio statement (kuanzia lini hadi lini). Kutokana na ukubwa statement unaweza kututumia barua pepe yako na kesho mapena tutakutumia...

2. Tanesco hatupandishi matumizi wala manunuzi ya mteja..
 
Yapo mazingira yanayaoweza kupelekea mteja abadilishwe kundi la matumizi.tunaomba namba yako ya mita na ya simu tukupatie ufafanuzi zaidi
 
Mpunguze kutukatia umeme uku mbagala bana
 
Pia ili kuweza kupelekwa kuwa mteja mdogo ni lazma uombe ili kudhibitisha kuwa ni kweli unataka huduma hii kwa sababu endapo utakiuka masharti na vigezo Tanesco tunakupiga faini ya kuvunja makubaliano na baada ya muda mfumo wetu unakuondoa kwenye mteja mdogo
 
Mimi ni wakala wa airtel money,
Nimemnunulia mteja umeme bahati mbaya ikakosewa namba ya simu token zikaenda kwa mtu mwingine.
Nimewapigia Airtel wakasema mpaka niwasiliane na tanesco
Hebu mnisaidie maana
 
Nashukuru kwa prompt response.

Nahitaji kuona njia ya manunuzi, jumla ya units zangu ninazonunua. Muda na tarehe kuanzia August 2017 hadi October 2018.

Msingi wa hoja ya Pili ambayo nadhani hukuielewa ni Kuwa mteja kama alikuwa anamatumizi madogo, halafu akawa anatumia umeme miezi mitatu mfululizo kuzidi units 75 automatically anapandishwa juu. Mfano, shilingi 5000/= hutoa unit 41 kwa mteja mwenye matumizi ya chini na unit 14 tu kwa mteja mwenye matumizi makubwa. Swali langu likawa Kwanini huyu anapokuwa anatumia matumizi madogo asishushwe automatically bila kuhitaji kuomba kwenu?

Asante. Email Nitakutumia na mita namba.
 
Mradi Wa Umeme vijijini ( REA) Eneo Mkokozi wilaya Mkuranga , tarehe 25/7/2018 niliipia mita 2 kwa majina ya Annastazia Bajagae.

Kwa makosa ninayoamini ni ya kibinadamu nilifungiwa mita 1, nikaelezwa kuwa wao wamepewa mita 1 na Hata hizo risiti 2 nilizonazo hawajui ni IPI iliyopewa mita hivyo wakanishauri nirudi TANESCO Mkuranga kutoa taarifa.

Nilifanya hivyo, na kuahidiwa tatizo langu kushughulikiwa kwa maana ya kufungiwa mita ya 2, nimevumilia nimepewa namba ya Simu lkn kila ukipiga jibu TUNASHUGHULIKIA. ( Kweli)

Hivi hata hili , mpaka nguvu ya ziada ( ziara za viongozi)
 
Contact.centre@tanesco.co.tz tuma hapo na namba yako ya simu tutakupatia ufafanuzi yote hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…