TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Habari,Leo mafundi wa Tanesco wamefanikiwa kuja na kutengeneza meter yetu lakini Imebakia clear tamper codes za kuweza kumalizia tatizo...wamesema tuwasiliane na makao makuu ili mtupatie codes za kuclear tameper....Naomba mtusaidie kwa hili jamani.Tumekaa bila umeme kwa muda mrefu luku number Ni 37164698759
 
TANESCO MAKAO Makuu hamlioni lalamiko langu kwa Tanesco Kigamboni au tatizo liko kwenu kwa kushindwa kupeleka vifaa kazi; kupeleka magari pamoja ukarabatii wa magari yaliopo ili kuboresha huduma maana Tanesco Kigamboni wanna visababu vyao eti magari Ni machache na mabovu.
Tanesco Makao Makuu mnakaa kimya inamaana mmeshindwa kunisaidia!!? Au ndiyo hivyo mko kwa wale wenye mamlaka na uwezo wa kipesa. Tuka lalamikie wapi. Ngoja niadike barua EWURA CC labda watanisaidia.
 
Tanesco (Rea) mnatutenga watu wa zingiziwa chanika Dsm, yani tumekuwa kama kisiwa umeme hamtuleti ila mnapeleka maeneo ya mvuti na dondwe wakati mliwaambia wananchi wakate mazao yao.
 
Kuna nguzo ya Umeme karibu na shule ya msingi Ludete Kata ya Katoro wilaya Geita imekatika karibu kabisa na uwanja wa shule. Ni zaidi ya mwezi mmoja mimi kama mwananchi nilipiga simu kutoa taarifa nikaambiwa kuna watu wengine wameshatoa taarifa. Kuna watumishi nina namba zao nilipiga picha nikawatumia lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa. Najiuliza inasubiriwa ianguke watoto washike nyaya ndiyo majanga yawalete au kinasubiriwa kitu gani?
 
Tunaomba namba yako ya simu.mpendwa.mteja wetu
 
Habari,Leo mafundi wa Tanesco wamefanikiwa kuja na kutengeneza meter yetu lakini Imebakia clear tamper codes za kuweza kumalizia tatizo...wamesema tuwasiliane na makao makuu ili mtupatie codes za kuclear tameper....Naomba mtusaidie kwa hili jamani.Tumekaa bila umeme kwa muda mrefu luku number Ni 37164698759
Wilaya

Eneo

Namba ya simu tafadhali
 
Ifahamike wazi kwamba TANESCO walitoa tangazo kwamba umeme utakatwa mikoa ya kitanesco ya ukonga na temeke kila Jumanne na Jumatano kuanzia mwezi wa tisa hadi tarehe 7/11/2018. Lakini kinyume na tangazo lao, leo tena umeme umekatika ikionekana ni muendelezo wa utaratibu wao wa kukata kila siku za J4 na J5.

Ni vema TANESCO mkawa wazi mseme kuna mgao wa umeme ili wananchi tujiandae kisaikologia. Kwani mgao wa umeme si jambo geni

#Repost #Repost #Repost
TAARIFA KUHUSU HALI YA UMEME ENEO LINALOLALAMIKIWA*

Ndugu wapendwa wateja wetu

Tunapenda kuwajulisha kuwa hakuna mgawo unaoendelea Ila kuna Uboreshaji wa upatikanaji wa umeme kwenye kituo chetu cha Kipawa.Kazi hii inahusisha uvutaji wa njia nyingine ya umeme ya Msongo wa 132kv kutoka ubungo kwenda kipawa.Zoezi hili lilianza tarehe 18/9/2018 na litaisha 7/11/2018.

Matangazo yaliyotolewa kwa wateja wetu.Tunajitahidi wakati mwingine kupata njia mbadala wakati mwingine ili wateja waweze kupata umeme wakati wa mchana ambapo inatulazimu kurejesha katika hali ya kawaida wakati wa usiku.

Tunawaomba radhi sana wapendwa wateja wetu kwani kazi hii imelenga kuboresha upatikanaji na ubora wa umeme.

*TANESCO*
 
*TAARIFA KUHUSU HALI YA UMEME ENEO LINALOLALAMIKIWA*

Tunapenda kuwajulisha kuwa hakuna mgawo unaoendelea Ila kuna Uboreshaji wa upatikanaji wa umeme kwenye kituo chetu cha Kipawa.Kazi hii inahusisha uvutaji wa njia nyingine ya umeme ya Msongo wa 132kv kutoka ubungo kwenda kipawa.Zoezi hili lilianza tarehe 18/9/2018 na litaisha 7/11/2018.

.

*TANESCO*
Tanesco mlisema mwisho ni tarehe 7/11/2018 sasa mbona na leo mmekata kama kawaida
 
*TAARIFA KWA WATEJA WA WILAYA ZA KITANESCO KIBAMBA NA KIMARA*

TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini umeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kufungua ofisi mpya ya *WILAYA YA KIBAMBA* eneo la Kibamba kituo cha *KIBAMBA SHULE* kufuatia hilo baadhi ya wateja waliokuwa wanahudumiwa na Wilaya ya Kimara sasa watahudumia na wilaya hiyo mpya kama ifuatavyo:

*ENEO LA WILAYA YA KIBAMBA*
[emoji841] HONDOGO, KIBAMBA, KIBWEREGE, KING'AZI, KWEMBE, NJIA YA KWENDA MAKABE UPANDE WA KUSHOTO ,NJIA YA KWENDA MARAMBA MAWILI UPANDE WA KUSHOTO , MBEZI KAMA UNAENDA GOBA UPANDE WA KUSHOTO NA MSIGANI MPAKA MSUMI

*ENEO LA WILAYA YA KIMARA*

[emoji841] UBUNGO MSEWE, KIBO KWA GWAJIMA, KIMARA YOTE, BARABARA YA MALAMBA UKITOKEA MBEZI STAND KAMA UNAENDA KIFURU UPANDE WA KUSHOTO KIMARA NA KUTOKA MBEZI STAND KWENDA MSUMI KWA DALADALA UPANDE WA KULIA KIMARA

Hivyo basi hata kwenye group letu la WhatsApp tutagawanyika ambapo wateja wanahudumiwa na wilaya ya Kimara watabaki kwenye group hili la siku zote na wateja

wanaohudumiwa na wilaya ya Kibamba watafata link ifuatayo kujiunga WhatsApp group ya eneo la Kibamba kisha wajitoe kwenye group la Kimara ili kuwapa nafasi wateja wengine

*Gonga hapo kwenye link kujiunga*

TANESCO HUDUMA KIBAMBA

Kwa mawasiliano:
*Wilaya ya Kimara*:0717379696/0788379696

*Wilaya ya Kibamba*
0677111102/0699111103

*Magomeni/Mkoani*
0784271461/0222171759

*Endelea kufurahia huduma zetu*

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano na huduma kwa wateja

TANESCO Kinondoni Kusini
10/11/2018
IMG-20181113-WA0003.jpeg
 
Lini Umeme wa REA utafika ktk vijiji vya Kibamba na Sunguvuni wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani
 
Back
Top Bottom