TANESCO mjitathimini uendeshaji wenu wa shirika kwani ni miaka na miaka sasa imepita tatizo la kukatika umeme imekuwa kero utadhani ndo SERA YA TAIFA.
Ifike wakati tuache mazoea,umeme ndo kila kitu katika ukuaji wa uchumi wa nchi nyingi dunia kwan big investment zinategemea sana umeme lakini pia hata watu wa kawaida wanategemea umeme kuingiza kipato na kipato kinavyoingia kwa mtu mmoja mmoja ndio uchumi unakuwa lakini pia stability ya umeme inavutia wawekezaji.
Naomba niwakumbushe Rais wetu alisema hii ni Tz ya viwanda je na nyinyi mnalijua hili?? Ukizungumzia kiwanda unazungumzia na umeme.
Kwa kuhitimisha tuache mazoea kazini,tuwe wabunifu and tutumie elimu zetu kwa ndugu zetu wa Tz kwa mustakabali wa taifa hili linaloendelea.
*SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME*
*1. Utangulizi*
Kwa muda mrefu kumekuwa na uelewa kutoka kwa wateja wetu kuwa kila umeme unapokatika TANESCO WAMEKATA. Tumeona ni vyema tukatoa
Maelezo kwa ufupi ili wateja wetu waelewe sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi, zilizo ndani ya uwezo wa TANESCO na zisizo ndani ya uwezo wa TANESCO.
*2. Sababu za TANESCO Kukata Umeme*
TANESCO itakata tu umeme endapo kuna sababu zifuatazo *BILA* kuwataarifu wateja:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura _emergencies_ (imeelezwa hapo chini namba 4)
*3. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - _Planned Interruptions_ endapo:-*
a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu _Planned Preventive Maintanance_ (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara _Routine Maintanance_ (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV
*4. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura _Emergency cases_* nyingi ni Unplanned Interruptions
a) Za kiasilia _Natural Calamities_ (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.
b) Hujuma za kibinadamu _Sarbotage_
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.
Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, Umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.
*5. Hitimisho*
Tunajua jukumu la TANESCO ni kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika, pia ni ukweli kuwa mifumo mingi ya TANESCO ni ya muda mrefu hivyo inahitaji ukaratabati wa mara kwa mara na uwekezaji mkubwa ambao sote tumeona jitihada zinazofanywa na Serikali ili TANZANIA iwe na umeme wa uhakika.
Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa kama viongozi tunaamini hakuna mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu tena wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme. Kama yupo na anafahamika ( _Kama baadhi ya wateja wetu wanavyotuhumu_) tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kumshughulikia kwa taratibu za kisheria na tutakuwa tumelisaidia Shirika na serikali kwa ujumla.
TANESCO
_*Tunayaangaza Maisha Yako*_