Kwa hiyo gharama hizi ni sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO wilaya ya kinondoni, tunaomba tujue kama kuna mgao au la! Hivi na jote lote hili la dar mnaanzaje kukata umeme. Wiki hii ilioisha na kurudi nyuma dar kulikuwa na joto la hatari halafu mnakata umeme, manata watu waishije, watoto wadogo wasiojua hata kuongea wanahangaika na joto, mtu mmoja hapo ofisini kakaa na kikatia umeme. Okay mchana mtu unaweza ukatoka ukaitafuta hewa ya Mwenyezi Mungu, je usiku wa manane mtu uende wapi, kwanini mnatesa watu lakini nie TANESCO, unakataje umeme usiku wa manane nauliza
 
Hivi kumbe umeme ukikatika ni mtu anaamua tu kwa mapenzi yake kwenda kukata umeme!
Ahsante kwa kutufahamisha
 
Hapo Liwiti si ndio wana Ofisi zao za Tabata?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa bhana yaani ukilipa hela ya connection yq umeme ile 321000 lakini cha ajabu mafundi wakija site lazima wakugasi tena wanataka hela kabla ya connection yaani ni kero sio mara moja wala mara ya pili...TUMEWACHOKA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli tanesco, mbona bado hamtaki kubadirika kabisa, kwenye huduma kwa wateja?!! Nina tatizo langu, juu ya nguzo imeegamia bati,,

nimetoa taarifa hadi nimechoka muda wote simu ziko busy, hapa hapa kupitia jukwaa hili, mkasema niwatumie namba yangu ya simu nimefanya hivyo, sasa ni karibia mwezi,

hakuna kitu chochote kimefanyika?!? Basi acha nitafute sehemu nyingine ninapoweza pata msaada wa haraka!!
 
Wewe ndugu TANESCO mie na wewe tupo sana tu humu yaani!
Nakukumbusha tu mvua hizoo zinakuja,sitaki ugomvi na wewe, waambie marufuku kukata umeme Dar es salaam.Ningekuwa mimi ndio wewe ningefanya operesheni ya kukagua na kuweka sawa miundombinu yote korofi kabla mvua hazijachanganya ili zikija zisilete shida,mie nakupa madini tu hapa,sasa ole wako mvua zije unikatie umeme Kimara,utaninunia humu nakwambia TANESCO na hilo koti lako la kijani hapo.

Wiki hii hujanikatia umeme nimeshangaa,hongera bhana!...aargh,nimekumbuka jana usiku saa tisa ulikata ukawahi kurudisha kabla sijaamka!bahati yako nililala ila nilihisi tu usingizini umeukata na kweli ulikata,yaani hunidanganyi jinsi nnavyopenda umemei!🤒
 
Kuna mtumishi wenu yupo Kabuku Tanga, kwa jina la Sadiki, nikikwazo sana, naomba mumfatilie anakatisha sana wateja tamaa
 
Fomu yangu tangu mwezi was nane mwaka Jana imeandikwa nisubiri nguzo za mradi. Ila kuna wateja wapya wanatokea nyuma yangu wanawekewa tu sa sijui wanatoa rushwa maana ukiwauliza wateja hawajalipia. Mi nikienda TANESCO naambiwa nisubiri nguzo za mradi toka mwaka jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nicho ona Voda ongozi wa Tanesco muangalie na kufuatilia kwa makini kero znazotolewa humu, maana wanaochafua taswira ya Tanesco ni baadhi ya watumishi sio wote,mfano unakuta unaenda Tanesco lkn kitendo cha kutatua tatizo linachukua muda mrefu sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ndg yangu nasumbuliwa na kupata nguzo , Kabuku Tanga kwenye hili sijapata majibu sahihi toka kwa wahusika, nimetoa mpaka jina la mtumishi
 
Mkuu TANESCO Nimebambikiwa deni la umeme la milioni tatu. Kila nikinunua umeme nakatwa asilimia 50%, tatizo limeanza wiki mbili zilizopita. Baada ya kupiga simu nikapewa taarifa ya hilo deni kuwa ni kabla ya mfumo wa Luku. Nimekuwa mlipaji mzuri wa bili za umeme Tanesco kabla ya Luku.

Hivyo nimetembelea ofisi za Tanesco lakini nazungushwa kila siku, leo wakinambia system ya madeni haifanyi kazi, kesho yake wanasema Manager hayupo. Nahitaji msaada kwa sababu nina hakika sina hilo deni. Nimeanza kutumia luku miaka mingi iliyopita iweje wanibambikizie deni kipindi hiki.
 
TANESCO hebu rudisheni umeme Kimara.
Hii ni haki ya mwananchi amelipa kodi serikalini kupata huduma kama hizi,iwe jua iwe mvua.
Kwanini mnakuwa hivi nyinyi watu mfanywe nini?
Sisi wananchi wa leo hatupendi power disruptions sababu shughuli zetu za kiuchumi zinategemea sana umeme,hasa maeneo ya mijini kama Dar.
Ni aibu hadi leo hii mvua ikinyesha mnakata umeme,huu ni ujima wa hali ya juu.
Tunataka umeme wa uhakika Dar.
Rudisheni umeme mda huu mlikokata kote,including Ubungo,Kimara,Mbezi.
Mvua ndo muda wake huu kila mwaka,ni nature,you cant fight or wait for it to pass,it is there to stay forever.So siwaelewi mnapositisha huduma kwa hitilafu zitokanazo na mvua za kawaida kama hizi hapa Dar wakati kuna maeneo huko mikoani yana mvua na radi kali zaidi ya hizi na umeme uko stable,which means miundombinu yenu hapa Dar mibovu,ndio sababu mnatusumbua sana wananchi,tena bila aibu katika mahali ambapo ndipo mnapata pesa nyingi kuliko pengine Tanzania.You are not serious na biashara yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…