TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nina mambo mawili

1. Kimara mwisho njia hii ya kwenda bonyokwa kila siku umeme unakatika na sio unakatika kwa muda mfupi no. Unakatika muda mrefu bila matangazo bila samahani bila chochote tunaomba kujua hili tatizo litakwisha linii????Maana imekuwa ni kawaida sio siku moja mbili wala tatu ni almost kila siku umeme lazima ukatike hapa muda huu saa moja na robo usiku umeme umekatika kwa mara ya tatu rupo gizani naomba kujua tatizo hapa ni nini na kama linajulikana nini kinashindikana kulitatua mara moja lisijirudie?nina mashaka sana kama mna wataalamu wanaojua kazi yao maana kama wapo basi ingekuwa tatizo likitatuliwa halijirudii.tuliaminishwa bomba la gesi likikamilika hakuna kukatika kwa umeme sasa nimejiridhisha issue sio umeme kidogo issue ni wataalamu wetu kutatua matatizo yaliyopo

2.naomba kujulishwa uhusiano wa mvua kunyesha na umeme kukatika hapa kimara hakuna siku ya mvua umeme lazima ukatike embu tanesco tuambieni kitaalamu uhusiano uliopo wa mvua na kukatika kwa umeme maana ni aibu kwa nchi hii ya viwanda na janga la umeme,shame on you
Tafadhali tusaidie namba yako ya simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa na viambatanisho vyako vyote andika barua ya cover letter kwa ajili ya kuomba mkoa huska kupata ridhaa ya kufanya ukandarasi kwa wateja wapya wa TANESCO na utajibiwa
naomba kujua ni jinsi gani naweza kufanya ili kampuni yangu iingizwe kwenye list ya contractors wanaotambuliwa na Tanesco wa kutandaza nyaya kwenye majengo na kuchora ramani ,ili niweze kuhudumia wananchi,
natanguliza shukrani zangu




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Pole sana ndugu mteja, tunaomba kujua ni sehemu gani hapo. Mteja wetu anatakiwa kupata umeme wenye ubora na uwakika
Mkipost nyie mnaandika vitu vya msingi kweli utazani watu. majuzi hapa mtaani kulitokea shida ya low voltage nawapigia najibiwa eti bora huko kuna low voltage kuna pengine umeme umezima kabisa, nikajiuliza kumbe hata low voltage ni huduma ya TANESCO. afu mda ule nawaeleza tatizo wananiambia wana taarifa tangu juzi, ha haaaa.




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Kwema humu ndani?

Nawaza kwa hili joto la sasa wakikata umeme itakuaje

Tanesco tafadhalini msifikirie kukata please tutakwisha haki vile

Kuna siku umeme ulikatika mchana na siku hiyo nilikua zangu getto kwangu ilibidi nikatembee tu maana joto la humo ndani ilikua ni balaa asikwambie mtu

Sahiz hadi feni zimegoma zinapuliza moto tu sahz

Unapambana vipi na joto kwako?Tanesco wasikate maana tutakwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom