hili joto ni kiyamaaa.
 
Tanesco wamekusikia,, hakikisha units hazipungui... umeme hawatakata
 
Mbona
 
Watu wameomba umeme tatizo inakua nguzo . Yani ni changamoto kwa kweli, mm nimepimiwa na ikaonekana kwangu kinahitajika nguzo mbili, hadi leo sijapata jibu la uhakika, naomba majibu ya kuleta matumaini
 
Nina masikitiko makubwa sana, hii namba 0768985100 ipo kwenye website yao kuwa ukiwa na tatizo uwapigie, nimepiga zaidi ya mara 4, simu inaita tu, kibaya zaidi, kumbe inakata salio la vocha, simu haipokelewi lakini salio la vocha linaisha, huu ni wizi mkubwa sana, kilio changu nakipeleka kwa waziri tafadhali shughulikia huu wizi.
Mhe: waziri, angalia salio salio lako, kisha piga hiyo namba(ambayo haitapokelewa) halafu angalia salio lako, ni wizi mtupu, kwanini wakate salio ilhali wanajua hiyo line haina response ??
 
Taasisi za serikali ni muda sasa wa kuwa na Toll numbers ili waweze kufikiwa haraka na wateja
 
Salaam, kwenu Tanesco. Nawashukuru na kuwapongeza kwa baadhi ya hatua mnazozichukua lkn pia nawaomba mjitahidi zaidi na zaidi.

1- Nilituma mtu kunichukulia form za kuungiwa umeme.

Akakataliwa mpaka niende mm mwenyewe, nikaomba ruhusa kazini na kwenda Mkuranga na nikapewa huduma Bora kabisa.( Japo umuhimu wa mm kwenda huko ulikuwa hauna maana.)

2- baada ya kukamilisha ujazaji form nilizirejesha na kuambiwa surveyor atafika baada ya wiki 3 sikufurahishwa na muda huo kuwa mrefu.

3- Ndani ya wiki moja, surveyor alifika kwangu na kutoa maelekezo na mengine anayoyajua kitaalamu. Nilipofanya mawasiliano naye akanijulisha kuwa ameisha kamilisha sehemu yake nifike ofisini kwao kwa ajili kuandaliwa malipo.

4- Nilifika ofisini Mkuranga na kuulizia juu ya hatua zangu nikajulishwa kuwa HAKUNA NETWORK hivyo haiwezekani lolote kuendelea. Nisubiri.

5- Nilisubiri kwa muda wa saa moja, Khali ikawa Ile Ile, ilibidi niage niendelee na majukumu mengine nikapewa namba ya simu ili niwe nafanya mawasiliano kuona Kama NETWORK imerudi .

6- Kila wakati nimekuwa naulizia Network jibu ni Bado.

7- Nilidhani suala la NETWORK ni la muda tu, lkn baada ya kuliongelea kwa wengine, jibu wanalonipa ni KERO iliyopo MKURANGA TANESCO. Kila siku NETWORK HAKUNA.

8- tupo katika maisha ya kawaida tunaomba huduma ifanyike haraka changamoto hii iondolewe TUNAPOJICHANGA CHANGA tumalize majukumu Mara moja.


9- TANESCO NYINYI NI MUHIMU UCHUMI MWINGINE UENDELEE.
 
Tunashukuru kwa taarifa mpendwa mteja wetu

Je umeshapatiwa huduma? Kama bado tusaidie namba yako ya simu

Kuhusu kutakiwa ufike mwenyewe huu ndio utaratibu nchi nzima kwani mteja anapoenda mara ya kwanza mwenye inatusaidia kupata taarifa zake kamili pia inasaidia kuzuia watu wasiowaaminifu kulaghai wateja ( yametokea mara kadhaa) hivyo mteja anawajibika kufika ofisini mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…