Kwa mteja mdogo wastani ni unit 75 kwa manunuzi yake. Hivyo tunakushauri sana nunua unit kwa matumizi kama neno LUKU ( Lipia Umeme Kadro Utumiavyo) kulimbikiza unit hakuna tatizo lakni inaweza tokea kuwa mita yako ikaaribika na kupoteza kumbukumbu zake, endapo utataka kupata unit zako za awali ambazo hazionekani inaweza kuleta shida.

Tumia umeme ambao utakutosha kabsa kwa matumizi yako.




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Huu ni wakati wa Coronavirus inabidi huduma ya umeme isiwe na matatizo ya kukatika mara kwa mara. Na ikitokea tatizo lishughulikiwe haraka. Kwasababu baadhi yetu tunahifadhi vyakula vya familia ili kupunguza safari za sokoni kuepuka Coronavirus.
Lakini kwa bahati mbaya hapa Tanesco Tabata kuna dalili za kufanya mambo kwa mazoea.
Umeme ulikatika leo 08/04/20 saa 3.00 usiku huu kwa dakika chache ukarudi kwa nguvu sana. Majirani zangu umewaka bila shida, ila kwangu tu haujarudi na nimepiga simu Tanesco Tabata saa 3.21 kuripoti nikaambiwa mafundi watakuja.
Saa 5.42 nimewapigia tena. Jibu ni kama kawaida: Fundi yuko njiani atakuja.
Nikaomba wanipe namba ya report file wakasema siku hizi hawatoi namba kwasababu "mtandao mbovu".
Sasa ni saa 00:15 bado nasubiri.
Kwa mwendo huu hatma ya familia zetu sisi ambao tunanunua vyakula na kuvihifadhi katika fridge halafu umeme unakatika vyakula vyetu vikioza tutaishije?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuko kwenye changamoto ya Corona virus na watu wanatakiwa kukaa nyumbani. Lakini kama huna chakula au akiba yako imeharibika kutokana na umeme kukatika utakaaje nyumbani?

Umeme ulikatika saa 3:00 usiku 08/04/20 ukarudi kwa nguvu sana kwa bahati mbaya hapa kwangu ukaleta shoti. Eneo lote majirani zangu umewaka bila shida ila kwangu tu haujarudi na nimeripoti TANESCO Tabata tangu saa 3:20 usiku lakini hadi muda huu 02:15 hawajafika kurudisha umeme.

Jana nilimtumia fedha nyingi kununua chakula pamoja na mboga kwa familia ili kupunguza safari za sokoni kuepuka Coronavirus. Nikahifadhi katika fridge. Sasa kutokana na umeme kukatika hivi vyakula vitaoza. Niatawezaje kuhimili changamoto ya Coronavirus?

Serikali isiache mambo kama haya yaendelee kama inataka tukae nyumbani. Utakaaje nyumbani kama huna chakula?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha vioze, kwanini ulimbikize chakula ilihali ukijua tabia hiyo inapandisha juu bei za vyakula? Inamaana wewe umejifungia ndani na hutoki nje kwenda kufanya kazi? Ukitoka kazini huwezi kupitia mahitaji ukarudi nayo?
 
Wacha vioze, kwanini ulimbikize chakula ilihali ukijua tabia hiyo inapandisha juu bei za vyakula? Inamaana wewe umejifungia ndani na hutoki nje kwenda kufanya kazi? Ukitoka kazini huwezi kupitia mahitaji ukarudi nayo?
Sikubaliani na wewe lakini sitakujibu kwasababu akili yako imefikia ukomo. Hutaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shirika letu pekee la umeme Tanzania mnafurahisha Sana. Maagizo ya Waziri na mnayoyafanya ni vitu viwili tofauti.

Waziri alitoa maagizo KUUNGANISHA UMEME nchi nzima kwa gharama na bei za REA nadhani.

Mimi nipo umbali wa mita 25 toka ilipo nguzo ya umeme na nimepewa quotation ya Tsh. 536,000.


Je, Tanesco mnatenda kazi kinyume na maagizo ya Waziri pamoja na Wizara ya nishati?

Tatizo lenu hasa Nini. Hivi ukimfungia mtu umeme SI ananunua luku na nyie mnapata mapato na Serikali pia inapata?

Kwa usawa huu, kea mlalahoi hamuoni kuwa laki tano Ni ndefh Sana?

Je, hamuoni mnakuwa kikwazo kwa MALENGO ya Mheshimiwa Rais?

Tafadhali Sana naomba mnijibu kero yangu.
 
Tunafuatilia ndugu mteja. TANESCO hatuuzi nguzo. Mteja anaunganishiwa umeme kwa umbali (mita)




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
Tutashukuru kama mnafuatilia. Maana tusije kuingia kwenye rushwa adui wa haki na hela zenyewe hakuna. MTU anajenga nyumba mpya anawekewa umeme sisi was zamani fomu zetu zimeandikwa zinasubiri nguzo za mradi mwaka mzima hakuna hizo nguzo wakati nguzo zipo ofisini zinaoza na mchwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijiji Cha losokonoi,kata ya lendanai,wilaya ya simanjiro mkoa wa manyara ambako mradi wa REA ulivuka kaya zaidi ya 300 bila kupata umeme mwaka 2019 Tanesco imefuatilia chanzo Cha Hilo tatizo? Tumeandika Hadi tumechoka hakuna ufuatiliaji hadi leo
 
Me ninalalamiko, hususan hapa wilaya ya bunda mkoa wa mara jimbo la mwibara ambayo ni halimasahauri mpya kibara, kijij cha mchigondo kilichopo kata ya igundu sisi tunatatizo la umeme wiki na sehemu imepita umeme hauwaki tukipiga cm tanesco kibara hawaji ebu tunaomba mtusaidie ni hili jmn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini hapa kwetu Ifakara kukatika umeme ni kila siku hasa tunapo anza kusikiliza taarifa ya saa 2 usiku ? jambo hili ni gumu kiasi gani kubadilika ? mbona imekuwa ni kawaida sasa ? hamuoni kama mnawakera watumiaji wa umeme ?
 
Kuna kukatika umeme kwa uhalisi kwa matatizo ya kiufundi. Pia kuna kukatika kwa kimkakati. Mafundi wanazusha matengenezo na hasa mwisho wa wiki na sikukuu ili kupata overtime. Wabane maintance engineers wako, piga chini over time zisizo na miguu , hutaona matengenezo ya kijinga yanajitokeza, hutaona kukatwa umeme. Awali Tanesco walikuwa wanazima mitambo ya mtera kisingizio maji. Tegeta iptl nao kuzalisha mpaka serikali inunue mafuta. Wakipewa hela wanawasha siku mbili tatu wanazima na kuwasha mtera, mpaka serikali ilipo washtukia.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mimi nataka kujua kwanini tanesco mnauza nguzo huku Waziri akisema nguzo ni bure?Ina maana Kalemani anatudanganya?Mimi kwangu kuna nguzo ipo chini miaka haijatumika ila nikiomba kuunganishiwa umeme mmataka pesa laki mbili na ushee kwa ajili ya nguzo tu,Naomba majibu maana malalamiko haya nina mpango kuyapeleka wizara ya nishati endapo sitapata msaada


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwanangu tuungane kupeleka malalamiko huko wizarani. Hata wilaya ya chemba mambo no hayo hayo nguzo zinaliwa na mchwa afu unaambiwa nguzo hamna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…