Naomba nipate kujua tatizo ni nini kwani tangu tarehe 24 Januari 2020 ,walifanya survey kwa ajili ya kupewa bili ya kulipia umeme,lakini mpaka leo sijapewa hiyo bili ili nilipie ,ninaitwa bupe john namba yangu simu ni 0753 26 34 52 ,eneo lilipo ni Isyesye Mbeya. Tafadhali naomba kujulishwa kama kuna tatizo: natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
From Arusha kwa kweli kwa sasa huduma zenu kwa jiji letu zinaridhisha kabisa


GOD IS GOOD
 
HABARINI WAKUU NILIPELEKE FOMUYA KUUNGANISHWA NA UMEME KATIKA KITUO CHENU CHA TEGETA DAR...NA BAADA YA KUKABIDHI NIKAONDOKA KUSUBIRI KUPIGIWA SIMU NA SURVEYOR KWA AJILI YA UKAGUZI....SIKU MOJA JIONI SAA 12 NIKAPIGIWA SIMU NA MTU ALIYEJITAMBULISHA KAMA NI SURVEYOR AKITAKA NIMUELEKEZE SITE ILIPO NLIMWAMBIA NIKO MBALI WAKAT HUO MM NPO POSTA YEYE. YUKO MADALE NIKAOMBA APPOINTMENT YA SIKU NYINGINE.ALIKUBALI LAKIN BAADA YA HAPO KIMYA HADI LEO NILIENDA OFISIN PALE TEGETA WAKASEMA FOMU ZIMEPOTEA NIANZE UPYA...NAOMBENI MSAADA WENU PICHA YA FOMU NILIZOPLEKEKA NNAZO


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco ukerewe ni tatizo kubwa
Katika tembea tembea yangu maeneo mbalimbali Tanzania nafikiri sijaona sehemu yenye matatizo makubwa ya umeme kama ukerewe
Kukosa umeme siku tatu au nne katika wiki ni jambo la kawaida sijui tanesco wanafanya nini

Viongozi wote wa serikali akiwamo mbunge wa eneo husika wanafumbia macho tu uozo huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco Katavi wanajitahidi sana kutatua kero zetu. Ukiwapigia kwa simu ya dharura wanarespond chap, wanakupa namba ya huduma vijana wanafika fasta. Waendelee vivyohivyo.

Tatizo kubwa ni hii issue yakubadilisha matumizi kuja yakawaida(madogo) baada yakuingiza umeme kwa marayakwanza. Wanasema wanasubiri mwongozo sijui maelekezo eti utaratibu imebadilika.

Hebu tusaidieni basi. Wanyonge sisi kuendelea kununua 350 @unit tunaumia. Kwanini lakini jamani?

Hebu tusaidieni basi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nawaita TANESCO huku
 
Tafadhali unapotoa lalamiko au kuuliza weka taarifa kamili ya vijiji husika na namba yako ya simi kwa taarifa zaidi kutoka TANESCO

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba kutoa lalamiko langu kwa Tanesco ndg yangu ameomba umeme sasa ni mwezi wa tatu hakuna jibu lolote, ameishia kupimiwa saiti yake Kabuku Tanga, kila akifatilia Tanesco Korogwe anaambiwa nguzo hakuna asubiri, tatizo hili linaisha lini? No yake 0625543419. Wahusika mnaomvwa muwe na majibu ya kueleweka
 
Imekuwa kawaida sasa Kimara kukosa umeme every weekend.
Hii nahesabu jumamosi ya nne ndani ya wiki tano umeme unakatwa Kimara asubuhi hadi jioni.
Huu ni mgao?
Kama ni matengenezo ni kwanini myaschedule weekend?
Maeneo ya nje ya mji kama Kimara umeme unatumika zaidi weekend sababu watu wako nyumbani wanapumzika,nyinyi ndio mnaona ni wakati sahihi kukatia watu umeme sio?
Au ndio yale mambo ya kutafuta overtime kama alivyosema mmoja wetu humu ndio mnalazimisha kazi zenu zifanyike weekend?

Serikali hebu fuatilieni hili shirika na kila kitu inalofanya.
 
Habari TANESCO. Kwa nini fomu za maombi ya awali hamjaziweka kwenye mtandao? Mtu ajiprintie ajaze na kuwarejeshea. Au vema zaidi, mtu anajaza huko moja kwa moja. Halafu viambatisho anavipelekea afisi jirani / husika ya TANESCO au navyo anaviambatisha mtandaoni. Control Number si/ni ndio habari ya sasa? Nini tatizo?
 
Hatujaweka kwenye mtandao kwa kuwa utafiti wetu umeonyesha kuwa zinatumiwa vibaya na baadhi ya watu wasio na nia njema lakini zipo taratibu zinaendelea kuruhus wateja kufanya online application

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo Kimara eneo gani? Namba yako ya simu yenye whatsApp tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa taarifa tunaifanyia kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu yetu ya wataalamu ipo eneo hilo kutatua tatizo tunawaomba uvumilivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jina lako uliloombea umeme ni lipi? Namba yako ya simi tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…