Umelipia lini? Jina? Wilaya namba ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umelipia lini? Jina? Wilaya namba ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijalipia, ni baada ya kupimiwa na kuambiwa tusubiri nguzo. Sasa nguzo hizo tunasubiri hadi lini? Allocation No 531520 -01318 KOROGWE TANGA -NORTH ZONE; nilishaweka no, ila majibu ni ya siasa tu, coz mwisho wa majibu naambiwa nguzo ni tatizo, Ndio maana nauliza mbona kauli hizi ni tofauti na kauli za Waziri husika?
 
Umeme unakatika sana pongwe Tanga kila siku tangu mwezi nne umeanza pongwe umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi Jioni saa kumi na moja, hatujui nini shida.

Inakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umelipia lini? Jina? Wilaya namba ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nina ndogo wangu yupo Kange Tanga. Wakati anamalizia kujenga nyumba nguzo ya umeme iliwekwa nje kwake kabisa lakini alipokuwa anahamia na ameanza kufuatilia umeme chakushangaza Tanesco walikwenda wakaondoa nguzo badala ya kumuunganishia umeme. Huu ni mwezi wa tatu toka wameondoa nguzo nje kwake.

Sasa kweli hatujui intention ya TANESCO KUONDOA nguzo badala ya kumuunganishia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmetukatia umeme chang'ombe bora toka jana saa nane mchana mkawa mnafanya matengenezo saa moja usiku mkamaliza ila umeme ukarudi baadhi ya nyumba tukatoa taarifa tanesco kurasini na tatizo kupewa no 7125 lakini mafundi hawajafika matokeo tumelala giza bila sababu mnafanya hivi kwa kuwa hamna washindani au kwa kuwa mishahara yenu inaingia kila mwisho wa mwezi
 
Kukatika katika umeme Ni changamoto kubwa Sana ndg zangu TANESCO.Hali inakuwa mvaya Zaid hasa katika kipindi hichi Cha Janga hatari la covi 19.

Tumetangaziwa na serikali kubaki majumbani Kama hauna ulazima wa kutoka ikiwa Kama Tahadhari ya janga Hili. Kwahiyo tupo nyumbani tunaendelea kufuatilia taarifa za habari kuhusu janga Hili na elimu inayotolewa ya kujinga na corona. Lkn umeme Ni shida unakatika katika Sana, katka masaa kumi na mbili ya mchana umeme unawaka masaa matano kwa nyakati tofauti tofauti. Yaan washa Zima washa zima,ukijumlisha inakuwa masaa matano umeme unawaka ndani ya Masaa kumi na Mbili.

Lkn pia wizara ya elimu baada ya kuona watoto wanafunxi shule zimefunga na ili waendelee kujisomea wameanzisha utaratibu wa vipindi vya darasani kwenye Tv, lkn hays yote wanayakosa watoto wetu.

Kwahiyo Ni waaombe Tanesco natambua kazi mnayofanya Ni ngumu na changamoto za kiufundi Ni nyingi lkn jitahidin hasa katka kipindi hiki kigumu.

Sisi mtwara huku vijiijini Hadi watoto wameshakariri masaa ya kukatika umeme na kuwaka. Hatar Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo gani haswa? Wilaya na namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je amelipia kwa jina gani? Tarehe ngapi na namba yake ya simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeme umekatika toka jana saa nne maeneo ya mtoni kwa aziz ally, lakini ulirudi saa moja usiku lakini baadhi ya maeneo huku nyuma ya sabasaba haujarudi hadi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO Dodoma huu ni uzembe au uhuni? Tatueni tatizo la umeme eneo kisasa mtaa wa palanjo, mtaa huu umekua kero kubwa kwenye swala la umeme umekua ukikatika Kila wiki mala mbili na ukikatika swala la kurudishiwa ni ndani ya masaa matano mpaka nane. Hamtoi taalifa yeyeto wananchi hawaelewi tatizo haswa ninini? Tunaomba lekebisheni tatizo hili kwa haraka Sana vinginevyo tutakwenda kwa mh: Rais ili tumweleze Jambo hili na ikiwezekana tumwombe awaite mkajieleze kwake kwanini Jambo hili linajirudiarudia Kila wakati pasipo kulekebishaka. TANESCO mnamwangusha sana Mh Rais ktk kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni watu gani wanaosimamia huu mradi wa Umeme wa REA, maana huku kwetu toka mwezi wa 8 nguzo wamesimamisha na wananchi bado hawajapata umeme, wamefunga Trasfoma tu nakuondoka wanadai nyaya hazipo
Kama ni ishu ya serikali ni bora mkawaambia wananchi ukweli kuliko kuzungukazunguka, hizi form tumepeleka toka mwezi wa 8 2019 tunasubiri umeme lakini hadi leo mwezi wa 5 2020
Ebu tupeni majibu hapo tujue kama ni uzembe wenu au ni uzembe wa serikali.
 
Tafadhali tusaidie namba yako ya simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wilaya gani tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Hello! Mwaka Jana September 2019 nilijaza fomu, kisha mwezi wa 12 wakaja kupima eneo husika ( na kusema nguzo 3 zitahitajika). Sasa huu ni mwezi may, kila nikienda ofisi ya Tanesco iliyopo Makongolosi Chunya Mbeya wanasema tuendelee kusubiri nguzo. Je, habari za Kusubiria nguzo ni LA kitaifa?
 
Tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo gani haswa? Wilaya na namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Maeneo ya njia ya libobe Hadi kitere. Wiki hii yote kila saa kumi na mbili jioni unakatika unarudi saa nne au tano usiku. Hata Leo tarehe 2/5/2020 umeme umekatika saa saa 3 asbh, umerudi saa saa 5, umekaa nusu saa ukakata Tena, ukarudi saa Saba. Hapo umeme umewaka lisaa limoja tu Hadi saa Hadi saa nane, ukakatka Tena umekuja kuwaka saa kumi na mbili.umewaka lisaa limoja na nusu, saa mbili kasoro Umekata Tena na cjui unarudi saa ngapi. Kwahiyo muda huu umeme haupo saa 2.15 usiku sahiv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunategemea umeme wenzenu katika vibiashara vyetu tunavyofanya ili kujikimu. Kwahiyo unapokatika masaa matatu haujarudi au masaa 12 tunalala njaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtawara vijijini hasa laini ya vijiji vya mpapura,libobe Hadi kitere.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…