Kwanini TANESCO-KISARAWE huwa ni wagumu sana kutoa huduma ya umeme kwa wateja? Inaboa sana.
 
Ok nitashukuru Sana mkinifanyia kwa wepesi kwasababu ni sehemu ya biashara. Ni wiki mbili Sasa sifanyi chochote
Tunashukuru kwa taarifa mpendwa mteja wetu tunaifanyia kazi
 
Habari tena jamani ,nimeshalipia sasa wiki ya pili kwenda ya tatu je umeme unawekwa kwa muda gani ukishalipia
 
Umeme umekatika siku ya pili leo tatizo la meter ime stack huwezi kuingiza token.... Tatizo linajitudia mara kwa mara. Tusaidieni maana ni la muda sasa, maeneo ni Tabata Dar es salaam

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo jingine ni urasimu wa huduma zenu, mfano hii meter mlipendekeza ibadilishwe lakini danadana ni nyingi sana, au labda ndo bila kunyoosha mkono hupati huduma? Kingine ni gharama ya marekebisho, majuzi alikuja fundi kuirekebisha ila akasema gharama zake ni shilingi elfu 30 lakini hata wiki haijakaa tatizo limejirudia lilelile, je akija tena kuirekebisha tutoe kiasi hicho tena? Na akirekebisha itakaa muda gani! Mtatufirisi jamani. Tusaidieni

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
Tafadhali onyesha

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Namba ya taarifa
 
Nipo Kijijini wilayani korogwe,kuna nyumba tatu nalipia umeme, nyumba moja elf kumi napata unit 28, ila hizi nyingine kwa elf kumi napata unit nyingi zaidi,tatizo nini?
 
Utaratibu wa mteja mwenye matumizi madogo kumpeleka kwenye tariff zero upoje? Maana tunaambia mpaka fundi apite kila nyumba akague ndiyo upelekwe. Naomba ufafanuzi. Maana kama kuunganishwa nilishaunganishwa toka mwaka 2019 Novemba. Na fomu ya kuomba imejazwa toka mwezi wa nne 2020 lakini bado kimyaaaaaaa kabisa hakuna mrejesho wowote. Ukiuliza hakuna majibu yanayoeleweka.
 
Tafadhali onyesha namba ya mita eneo wilaya simu
 
Nipo Kijijini wilayani korogwe,kuna nyumba tatu nalipia umeme, nyumba moja elf kumi napata unit 28, ila hizi nyingine kwa elf kumi napata unit nyingi zaidi,tatizo nini?
Hii inatokana na kutofautiana kwa matumizi
 
Tanesco mpo, hivi dar kuna mgawo wa umeme ? Siku hizi haueleweki kama jana na leo daa kutwa unakatwa vipi!
 
Ivi jamani Tanesco huwa mnatatua changamoto kweli?
Maana mi nimeandika tatizo hapa lakini mpaka sasa hizi nimeandika maelezo zaidi ya mara mbili na hakuna simu yoyote!

Tatizo rejea comment #8218.

Tuko gizani jamani

Sent from my Nokia 2.2 using JamiiForums mobile app
 
Narudi tena na nasisitiza; mm ni mtumishi wa umma.

Nimekopa kwenye banks nimejenga nyumba 2 ndogo kwa ajili ya upangaji ili nikidhi kidogo mahitaji yangu.

Tanesco kwangu nawaona mna roho mbaya.

Nimeleta malalamiko hapa , lkn jibu lenu halina matumaini ya kweli .

Nimepiga simu Tanesco Mkuranga jibu ni lenye kuleta matumaini yasiyo ya kweli.

Kwa kumbukumbu zenu;

Nimelipa umeme tarehe 27/3/2020

Mmeleta nguzo kwangu tarehe 09/7/2020 kisha kunipigia simu na kunieleza eti hamtachukua siku nyingi kuniunganishia umeme.


Nijulisheni inachikua muda gani kuweka nguzo na kuunganisha umeme?
 
Je umelipa kwa jina gani

Namba ya simu tafadhali
 
Je umelipa kwa jina gani

Namba ya simu tafadhali
Nawaomba sana sana , kuweni serious kwa kweli, nimeandika humu, mmeniomba hayo mnayoomba mara 2 nimewapa na hii sasa ni mara 3 .

Nawaombeni sana fanyeni kazi kwa kujituma nimewaambia kwa kuwakumbusha tu ,

Naendelea kusubiria mtakapofurahi nyie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…