Naomba kujua ukisharipoti kunatatizo la nguzo mbovu huwa inachukua muda gani kubadilishiwa
 
Habari TANESCO
Kwenye eneo langu ule waya unaotoka juu ya nguzo kwenda ardhini(Guy Wire) umewekwa kwenye eneo langu. Nataka kutumia eneo langu kwa ujenzi. Nafanyaje ili mje mhamishe?
 
Habari TANESCO
Kwenye eneo langu ule waya unaotoka juu ya nguzo kwenda ardhini(Guy Wire) umewekwa kwenye eneo langu. Nataka kutumia eneo langu kwa ujenzi. Nafanyaje ili mje mhamishe?
Tafadhali fika ofisi ya eneo lako
 
Tafadhali fika ofisi ya eneo lako
Naomba kuuliza:

Kuna wateja tuliomba kuunganishiwa umeme tukaambiwa nguzo zimeisha tusubiri mwaka mwingine wa fedha ambao tumeisha uanza 2020/2021. Je bajeti hiyo imeisha anza kufanya kazi tuende tena Tanesco kufuatilia ili tuwekewe umeme ama bado?

Natokea wilaya ya chemba mkoa wa Dodoma.
 
Je wewe ulichukua form kwa jina gani

Wilaya gani

Namba ya simu tafadhali
 
Habari wanajamvi....?
Hii ni habari njema kwa wafanya biashara wenye maduka makubwa,kati na madogo yenye uhitaji,,,,
Kampuni yetu pendwa ya NEXIS tunapenda kuwataarifu kuwa tunawakaribisha ili muweze kununua software system kwa gharama rafiki ambayo itaweza kukusaidia kufanya record ya mahesabu kwenye mauzo ya duka lako pasipo na usumbufu na kuweza kukupa mahesabu sahihi ya stock yako iliyopo kwenye duka lako ,yaani itakusaidia kujua total ya mauzo yaliyofanyika kwa siku na pia inakuwezesha kujua stock iliyobakia kupitia computer yako iliyopo ofisini vile vile tunaweza kukuunganisha direct kupitia smart phone yako...
PoS system ni program yenye ubora zaidi na ni program rafiki kwa mfanya biashara kujua stock ya biashara yako kwa ujumla ..

nachukua fursa hii kuwakaribisha sana
kwa mawasiliamo zaidi piga 0692449416
 
Je wewe ulichukua form kwa jina gani

Wilaya gani

Namba ya simu tafadhali
Jina Alphonce Clement Chilimo.

Wilaya ya Chemba (Dodoma)

Simu yangu 0620 639923 / 0683 537644 .

Fomu nilijaza tangu mwezi wa nane 2019.
 
Je wewe ulichukua form kwa jina gani

Wilaya gani

Namba ya simu tafadhali
TANESCO mita yangu inanyeshewa na mvua sehemu mliyoweka. Je naweza kuhamisha bila kufika ofisini? Inaniletea shoti isije ikaniletea maafa.

Je kuna gharama kuhamisha?
 
TANESCO mita yangu inanyeshewa na mvua sehemu mliyoweka. Je naweza kuhamisha bila kufika ofisini? Inaniletea shoti isije ikaniletea maafa.

Je kuna gharama kuhamisha?
Tafadhali fika ofisi ya eneo lako
 
TANESCO mbona mmekata umeme Bunju kuna tatizo gani? Mnafanya viwanda vyetu visifanye kazi mnahujumu juhudi za raisi za kumaintain uchumi wa kati.
 
TANESCO mbona mmekata umeme Bunju kuna tatizo gani? Mnafanya viwanda vyetu visifanye kazi mnahujumu juhudi za raisi za kumaintain uchumi wa kati.
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANZANIA)*

*25/08/2020*

* KUKUMBUSHIA KATIZO LA UMEME MKOA WA KINONDONI KASKAZINI*

Shirika la Umeme Tanzania *TANESCO* Mkoa wa Kinondoni Kaskazini wilaya ya Tegeta linawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la umeme kwenye sehemu ya line ya Tg3 kama ifuatavyo;

*Siku* Leo Jumanne Tarehe 25-08-2020

*Muda* Kuanzia Saa 3 Asubuhi hadi 9 Mchana

*Sababu* Maboresho ya miundombinu ya umeme ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme .

*MAENEO YATAKAYOATHIRIKA*
Bunju A, Bunju B yote, Kinondo kati, Mabwepande yote na maeneo ya jirani.

*Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.*

*Tahadhari*
Usikanyage wala kugusa waya uliokatika au kulala chini.

Wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo:

Dawati la dharura Wilaya ya Tegeta
0688650878/0717650878

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

Imetolewa na:
*OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA- KINONDONI KASKAZINI*
 
Naomba msaada enyi TANESCO tafadhali.Mimi ni mkazi nipo mkoa wa songwe.IPO hivi mwezi wa july mwaka huu tulijichangachanga fedha ili tupate huduma ya umeme kwani bado kama nguzo mbili kutufikia.tukachanga zikafika lakinne,.miongoni mwetu tukampa ili azilipe.kabla ya kulipa miongoni mwetu akasema ana namba ya ofisa wa tanesco hivyo ni vema wawasiliane ili atueleze utaratibu wa kulipa.walipowasiliana na yule ofisa yule ofisa akasema,kunanguzo zipo za ziada naweza kuwaletea leteni hizo fedha .ni kweli afisa yule akapewa fedha.
Baada ya wiki moja alileta waya pamoja na nguzo.
KIMBEMBE KILIPOANZIA.
Yule afisa akaleta vibarua wakachimba mashimo nakusimika nguzo na kufunga waya.tulimwita mtumishi mmoja anayehusika kupima aligoma kupima,akadai hizo nguzo hazikuja kihalali mazingira hayo,hivyo ili atupimie ni shart tulipie upya hizo nguzo.
Ilitushtua sana habari hiyo kwani hatukutegemea habari kama hizo.tukajua labda anamambo yake.tukampigia mpimaji mwingine naye kaongea vivyohivyo.
Tukaenda kwa ofisa mmoja pale wilayani tukamwelekeza habari yote akatutishia kutwitia security na takukuru.tumejaribu mala kadhaa kumpigia afisa aliyetuletea hizo nguzo mwanzoni alionesha kuwajia juu wale wapimaji,lkn alipoona wamemkazia naye kaingia mitini na hapokei simu yetu hasa akigundua ni sisi tunampigia
TUNATAKA MSAADA GANI?
Msaada tunaotaka je huyu ofisa tumfanye nini?
Je hili swala ni rushwa?
Je hili swala mwishowe uwe nn?
Tunajiuliza Je tukienda kwa meneja hatatuitiwa security na takukuru?
Kunawakati nilisikia waziri anasema nguzo ni bure mbona wanasema tulipe?
Kama ni bure kwa nn wasitupatie mita ?.tunaomba msaada please
 
Tunasikitika kukujulisha kuwa malipo yote ya TANESCO yanalipwa kupitia bank na mteja anapatiwa control number. Kwa malipo yeyote uliyofanya kwa mtu au mtumishi ni kinyume na taratibu zetu.

Hivyo tujulishe ulilpatia nani

Jina lake

Namba ya simu

Lini

Kiasi gani

Na namba yako ya simu kwa uchunguzi na ufatiliaji zaidi
 
Nashukuru,naomba unipatie dakika chache niandae documents
 
Ninailalamikia ofisi ya tanesco sengerema ni miezi 8 sasa toka nimewasilisha fomu ya kuomba umeme imechukua takribani miezi saba kuja kufanya survey na ikaonekana nipo mbali kidogo kiasi cha kuhitaji nguzo mbili ,lakini hadi leo sijapata mrejesho wao pengine mniambie ni ofisi gani naweza pata msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…