TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
NINI TOFAUTI KATI YA UMEME WA REA NA UMEME WA TANESCO??
NAHIS MKANGANYIKO
Umeme wote ni wa TANESCO, REA ni Wakala wa umeme vijijini wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini ikishakamilika inakabidhiwa TANESCO
 
Umeme wote ni wa TANESCO, REA ni Wakala wa umeme vijijini wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini ikishakamilika inakabidhiwa TANESCO
KAMA NI WOTE WA TANESCO KWA NN
WAKALA GHARAMA ZIWR NDOGO KUINGIZA UMEME KULIKO TANESCO YENYE UMEME WAKE?
 
Karibu sana
Kumbuka pia kuwa nina restrictions ambazo zinanifanya nisitumie chakula kutoka mazingira ya nje ya nyumbani kwangu. Kitendo cha Microwave kuwa haifanyi kazi kutokan na tatizo la umeme, kunanilazimisha kuvunja utaratibu huu wa kutokutumia chakula kutoka mazingira ya nje. Tafadhali naomba sana msaada wenu
 
Tafadhali onyesha namba ya simu na wilaya husika

Saccoss - Mabwepande ipo Wilaya ya Kinondoni ,imepakana na Viwanja vya KMC(Kinondoni Municipal Council) Block 14 karibu na Tumaini Girls Boarding School Shule ya Serikali.

Nadhani Mabwepande ipo Mkoa wa Tegeta wa Tanesco maana ndipo tulipoenda kutaka kuchukua form ndipo walipotujibu mradi bado haujakamilika....Mradi mwaka mzima? Nguzo tayari ,nyaya tayari ,transformer nalo kupachika miezi mitatu imepita wameweka tu nguzo na chuma za kukalia transformer.

Namba ya simu ya kwangu au ya Tanesco wilaya? Kama namba ya kwangu ya nini wakati issue sio individual ni ya wakazi wote wa saccos-Mabwepande? Kama wewe ni ofisa mawasiliano ukiwasiliana na tegeta tanesco wanajua huo mradi ,sisi tunataka kujua nini kinachelewesha kutuwekea transformer na kupata umeme?
 
TANESCO kama kuna mgao ni afadhari mtangaze, yani huku bunju mnakatakata umeme. Kila siku juzi mlikata, usiku wakuamkia jana mlikata, sasa hivi mmekata. wiki iliyopita nako mmekata kama mara tatu. Mnakera mnasema nchi uchumi wa kati huo uchumi wa kati tunauendesha kwa kuni au?
 
TANESCO kama kuna mgao ni afadhari mtangaze, yani huku bunju mnakatakata umeme. Kila siku juzi mlikata, usiku wakuamkia jana mlikata, sasa hivi mmekata. wiki iliyopita nako mmekata kama mara tatu. Mnakera mnasema nchi uchumi wa kati huo uchumi wa kati tunauendesha kwa kuni au?
tunashukuru kwa taarifa tunaifatilia kwa hatua zaidi
 
Kama Kuna mgao baridi wa kumsindikiza Gwajima mseme. Mnakata hivyo umeme bila taarifa Mbezi.

Mtamkwamisha my raisi na waziri wa nishati huu ni wakati wa kuomba kura nyie mnakata umeme.
 
Tunakuelewa mpendwa mteja wetu ndio maana zipo hatua kadhaa zilizochukuliwa kuendelea kuboresha upatinaji w umeme eneo husika.Sisi hatukati umeme wala kupenda umeme ukatika
leo jumamosi nyingine umeme hamna kimara.unataka kuniambia hiyo mitambo yenu iko systematic kuamua kusumbua siku za weekend tu?hii ni purposely mnakata umeme.Mnatuumiza sana wakubwa.
Nilishawahi kuwaambia huku nje ya mji weekend kuanzia alhamisi hadi jpili ndio kunachangamka sababu watu wanakuwa nyumbani.Kama mna dharura za mara moja moja ni heri kufanya matengenezo yenu siku za jnne au jtano.Unakata umeme kila weekend,kweli?hujaona kabisa siku ya kufanya kazi ila weekend?Why do you prefer weekends?
We soma post zangu kila weekend lazima nije kulalamika humu.
Mimi sikati tamaa ntaendelea kukupigia kelele mpaka Kimara tupate umeme wa uhakika from Monday to monday.Kwa sasa mnatuzingua sana Kimara Mwisho.Huu ni mwezi wa tatu sasa kila wiki lazima tuna siku mbili au tatu za kukaa giza,especially weekends.This is not fair TANESCO
 
leo jumamosi nyingine umeme hamna kimara.unataka kuniambia hiyo mitambo yenu iko systematic kuamua kusumbua siku za weekend tu?hii ni purposely mnakata umeme.Mnatuumiza sana wakubwa.
Nilishawahi kuwaambia huku nje ya mji weekend kuanzia alhamisi hadi jpili ndio kunachangamka sababu watu wanakuwa nyumbani.Kama mna dharura za mara moja moja ni heri kufanya matengenezo yenu siku za jnne au jtano.Unakata umeme kila weekend,kweli?hujaona kabisa siku ya kufanya kazi ila weekend?Why do you prefer weekends?
We soma post zangu kila weekend lazima nije kulalamika humu.
Mimi sikati tamaa ntaendelea kukupigia kelele mpaka Kimara tupate umeme wa uhakika from Monday to monday.Kwa sasa mnatuzingua sana Kimara Mwisho.Huu ni mwezi wa tatu sasa kila wiki lazima tuna siku mbili au tatu za kukaa giza,especially weekends.This is not fair TANESCO
Tafadhali onyesha namba yakonya simu yenye whatsApp kwa taarifa zaidi za eneo lako
 
Tafadhali onyesha namba yakonya simu yenye whatsApp kwa taarifa zaidi za eneo lako
eneo ni Kimara mwisho Mavurunza,Dawasco,Matangini,Polisi,Sokoni,Catholic church Kimara,TRA ...hilo eneo lote linalishwa na line moja na halina umeme leo na ndio utaratibu ulivyo every weekend.Lazima tukatiwe umeme.hapa hakuna umeme tangu saa tatu na dk 40 asubuhi.
Sio tatizo langu binafsi ni tatizo la eneo lote nililolitaja hapo na lina historia ya zaidi ya miezi miwili sasa.Hebu fuatilia mkuu ujaribu kuwauliza huko kuna shida gani na weekends zetu huku kimara?hii laini ilitulia sana mwaka jana,sijui sasa hivi kuna nini.
Kwa ujumla tuna matatizo ya kukatika umeme sana Kimara yote tu mwaka huu.Tusaidieni umeme utulie.Mnatuumiza sana sisi wajasiriamali.nna magunia ya kukoboa hapa nawasubiri nyinyi muwashe umeme.
nna saluni zangu leo watu weekend ndio wananyoa sana,mmekata umeme.bora saluni ntawasha generator je,hizi mashine za kusaga natumia nini zaidi ya umeme wenu?na mimi ni mtanzania mmoja tu kati ya wakazi maelfu wa Kimara.mmeathiri shughuli ngapi kwa ujumla?every week we have two to three days za kununa.dah!not fair!
 
Habari Tanesco,

Ni mwaka umepita tangu muweke nguzo na nyaya eneo la Saccos--Mabwepande,tukifatilia kutaka kuwekewa umeme tunaambiwa mradi bado haujakamilika,umeme unatoka kinondo wameweka nguzo za kuweka transformer ambalo ndio lita supply wakazi wa saccos ni miezi mitatu imepita tangu waziweke hizo nguzo na chuma za kuweka transformer.

Tunaomba kujua ni kitu gani kinachelewesha kutuletea hilo transformer? Mnaweka nguzo mwaka mzima zinakaa tu maana yake nini?

Kama mmeshindwa ni bora mtuambie wananchi tujichange tununue transformer letu tuwakabidhi ili mliweke.
Tanesco ijumaa alikuja mtu wenu huku saccos Mabwepande na baadae wakaja mafundi wenu wakaweka vikombe na kushusha nyaya tatu za kuunga kwenye transformer wakaondoka.

Jumamosi hawajaja labda ni kwasababu sio siku ya kazi(benefit of doubt ),we hope kesho mtaendelea na process mtufungie transformer wakazi wa saccos tupate umeme ili tuendeleze juhudi za Mh Rais za kuendeleza viwanda.

Nguzo ziliwekwa July 2019 hadi leo September 2020 umeme hauwaki wakati wenzao Dawasa walianza kuchimba na kusambaza mabomba Nov 2019 baada ya muda mfupi tu tayari tunapata maji ya dawasa.

Tanesco fanyeni kazi kuhudumia wananchi,watu wanahitaji huduma lakini hawapati ,najua mnafanya haya coz mme_monopolize soko ,hakuna ushindani....Issue kama hizi sio mpaka Mh Raisi aje ndio mfanye,Mh ana mambo mengi amewaweka nyie mumsaidie kutimiza malengo yake ya kutupatia umeme vijiji vyote.

Tunawaomba Tanesco mzidishe speed ya kazi yenu kabla mvua za mwezi wa 10 kuanza maana njia za kwetu ni changamoto kipindi cha mvua msije kuleta sababu kwamba hatuwezi kupitisha transfomer kwasababu ya njia mbovu.
 
Karibu sana
Bado sijapata msaada wiki sasa. Jina kwenye system yenu hamukuwahi kubadilisha, kwa hiyo linasomeka kama John C. Sivalon. Details zangu ni kama nilivyokupatia kenye Persona message. Sivalon alishahama kwenye nyumba hiyo karibia miaka 20 sasa
 
Usiku mwema
IMG_20200922_232105_856.jpg
 
Kwakweli sasa linakua tatizo sugu mitaa ya Makumbusho mpaka akachube huku Umeme unakatika mara nyingi sana. Na mbaya zaidi unakatika asubuhi unarudi jioni wakati siku imeisha. Ingekua inatokea kwa dharura tungejua ni matatizo ya kawaida ila sasa hii si dharura tena maana tangu mwaka jana hili tatizo linajirudia.

Nini shida nyie TANESCO? Mbona mnaturudisha nyuma? Wiki hii tu ni mara ya pili mmekata umeme asubuhi na mpaka mchana huu haujarudi. Mnajua hasara mnayotusababishia?

Tunaomba mtatue tatizo once and for all sio kubabaisha kila mara tatizo linajirudia. Hali ni ngumu na mzee baba mnajua hajaajiri mpaka leo halafu tukikomaa kivingine mnatuwekea vigingi
 
Habari,Mimi mkazi wa kata ya Nyanga Bukoba manispaa.Eneo kubwa la mtaa wetu wa nyanga zahanati hatujafikiwa na huduma umeme.Sababu kubwa ni kuwa Huu mji umeanzishwa hivi karibuni na kwa sasa una takribani nyumba 107 ambazo watu wanaishi na ujenzi bado unaendelea. Tumefanya juhudi mbalimbali za kuomba kusogezewa nguzo ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua Tanesco iliyosainiwa na wakazi waishio mtaani pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa na kata mwaka 2019 tunashukuru alikuja surveyor na akapima Eneo letu na akatuambia tunatakiwa tupate transforma.Tunawaomba Tanesco Mspeed up zoezi la kutuletea nguzo na transforma nasi tupate umeme.By the way hongereni kwa kazi mzuri mnazozifanya.
 
Back
Top Bottom