Tanesco kiukweli kama Taifa bado mpo chini sana kasi yenu ya kuhudumia wananchi haiendani na kasi ya serikali ya awamu ya tano, huwa ninakuja hapa ninaeleza tatizo langu lakini hamlitatui,
Kwa majina naitwa OSCAR MKANDYA JOHN mkazi wa BUCHOSA-SENGEREMA
Mtaa wa Iseni kata ya Nyanzenda, nilishaomba kupatiwa miundo mbinu ya umeme toka mwezi April 2020 sasa ni mwisho wa mwaka hakuna nilichokiona ni vyema mtu mkamueleza kama hawezi kupatiwa huduma akalitambua hilo mapema ni nini afanye, kama miundo mbinu mnasema itamfikia mwananchi pasipo gharama yeyote inakuwa vipi wananchi tunahitaji miundo mbinu hamtupi??? Pengine mseme ni wapi tunaweza kwenda kununua nguzo ili iwe rahisi kwa mwananchi kupata huduma kama zilivyo idara zingine kama maji n.k ninaomba kuwasilisha
 
Naandika kutoka PWANI MKURANGA VIKINDU KILONGONI tumepewa umeme kupitia mradi wa REA ni mwezi mmoja sasa umepita umeme tuliwashiwa na kupewa unit 10 lakini baada ya unit hizo kuisha ajabu ni kuwa kila tukitaka kununua umeme wanasema mita haijasajiliwa nimeenda tanesco mkuranga wamasema watakuja wenyewe kutupa sereal au siri ( sijui hasa inavoandikwa) kisha watusajili ili tuweze kununua umeme na kutumia kama kawaida siku nyingi zmepita kuja hawaji sijui tatizo n nini hasa na baadh ya nyumba mbili tatu za wenye uwezo wameshasajiliwa tayar maana umeme wao uliisha saiv unawaka lkn sie makapuku tusio na kitu wanatupiga tarehe your help plz
 
ULIZO KWA WATU WA TANESCO

Nimejenga nyumba ina Sebule/chumba master viwe mara nne,nimefanya wiring ya kujitegemea katika Kila Sebule/chumba master yake,Lengo la hiyo Nyumba ni kwaajili ya Kupangisha,

SWALI: je naweza kupata meter nne za Luku?
 
Asante sana tumepokea taarifa kw ufatiliaji na hatua zaidi
 
Tafadhali onyesha namba ya simu na namba ya mita
 
Tafadhali onyesha namba ya simu
 
Shirika lilipewa dhamana ya kuhudumia wananchi lkn kilichoasisiwa na uhalisia ni tofauti kabisa kama mnatoa huduma kwa upendeleo ni bora kuweka wazi kila mara ninakuja hapa kulalamika na ninaweka taarifa zangu zote lkn hakuna ufatiliaji, tunalalamika kuwa wananchi hawawapendi watumishi wa umma lkn tunasahau kuwa hatutendi haki kwa watumishi wa umma yaani nguzo mbili zinachukua takribani nusu mwaka kiukweli hii hali inaboa sana ,, nipo buchosa sengerema mtaa wa Iseni mawasiliano ni 0768145634 niliomba kupatiwa huduma ya miundo mbinu toka april lkn mpaka leo ni janja janja tu inatumika
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi
 
ULIZO KWA WATU WA TANESCO

Nimejenga nyumba ina Sebule/chumba master viwe mara nne,nimefanya wiring ya kujitegemea katika Kila Sebule/chumba master yake,Lengo la hiyo Nyumba ni kwaajili ya Kupangisha,

SWALI: je naweza kupata meter nne za Luku?
Mpaka uombe tuje kukagua na kujiridhisha
 
Kwanini mnazuia meter za three phase kuhama nazo wakati biashara kuna mda unahamia sehemu kwa kutafuta Sokoni kubwa zaidi na mkijua mnaziuza bei ghali
 
Kwanini mnazuia meter za three phase kuhama nazo wakati biashara kuna mda unahamia sehemu kwa kutafuta Sokoni kubwa zaidi na mkijua mnaziuza bei ghali
ELIMIKA NA TANESCO

MWONGOZO KUHUSU KUHAMISHA MITA KUTOKA ENEO MOJA KWENDA ENEO JINGINE

Je mteja anaweza kuhamisha mita kutoka eneo moja kwenda eneo lingine?

Jibu la TANESCO

[emoji3578]Mita ni kifaa kinachotumika kupima matumizi ya mteja kadiri ya matumizi yake.

[emoji3578] Mteja halipii wala kununua mita bali analipia gharama halisi ya kufungiwa umeme (Service line connection fee).

[emoji3578]Mita inaendelea kuwa mali ya TANESCO wakati wote mteja anaotumia umeme.

[emoji3578]Mita ya umeme ikiharibika au kupata hitilafu yeyote ambayo haitokani na uzembe au matumizi mabaya ya mteja, TANESCO inabadilisha mita hiyo kwa gharama zake kwa kuwa ni kifaa chake.

[emoji3578] Wajibu wa mteja wa TANESCO unaanzia baada ya mita kuingia ndani ndio maana mteja au fundi (mkandarasi) haruhusiwi kufanya matengenezo yoyote kwenye mita ya TANESCO, wala kuifungua.

[emoji3578] Mita ya umeme ikishafungwa haiwezi kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa ndani ya ploti / kiwanja husika na inafanywa na TANESCO kupitia maombi kwa maandishi ya mteja.

[emoji3578] Unapoona hitilafu yeyote kwenye mita au kifaa chochote cha umeme kuanzia kwenye mita kwenda nje toa taarifa TANESCO mara moja na sisi tutaifanyia kazi bila gharama yeyote.

Toa taarifa kupitia [emoji116]

[emoji3578] TANESCO APP

[emoji3578]Facebook/twitter/tanesco yetu

[emoji3578]Instagram:tanesco_official page

[emoji3578]Tovuti: www.tanesco.co.tz

[emoji3578] Barua pepe: Customer.service@tanesco.co.tz

[emoji3578] Huduma kwa wateja
0768 985 100/ 022 219 4400

TANESCO Tunayaangaza Maisha yako
 
Tunaomba kujulishwa tumerud kwenye umeme wa mgao au vip haiwezekan kwa siku umeme unakatika Mara 5
 

Ni week sasa tangu niandike hapa kuhusu hili jambo, nilijibiwa kuwa tumepokea taarifa yako tunafanyia kazi (kama wajibiwavyo watu wote humu)
Napenda kuuliza nitajuaje kama jambo langu linafanyiwa kazi? Mnaomba namba za simu lakini hamzibigi atleast kuwaweka wahanga karibu,

Tafadhali tupeni hata moyo basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…