SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
*TAARIFA YA KATIZO LA UMEME LAINI YA VIWANDA*
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga linawataarifu Wateja wake wa Shinyanga kuwa, Umeme utazimwa siku ya Alhamisi tarehe 24/08/2017 kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.
*SABABU*
Kupisha kazi ya kubadili nguzo zilizooza, kunyoosha nguzo zilizolala, na kukata miti iliyosogelea laini.
*MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA NI*
Maeneo yote ya NBC, Ibinzamata, Mwanakapaya, Ndala Masekelo, Ndala Upongoji, Mwawaza, Kizumbi, Keshini, Nhelegani, na Chuo Cha Muccobs.
*TAHADHARI*
Tafadhali usiguse wala kukanyaga nyaya zilizokatika,Kama kuna tatizo lolote la huduma tafadhali tupigie tuelezee, tutakusikiliza na kukufikia.
Namba zetu:
0754 251 070, 0783 521 070 na 028 2762 120
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100
Tovuti:
www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Shinyanga
TANESCO "Tunayaangaza maisha"