Fomu ikishatolewa kupitia mfumo inakuwa kwenye mfumo muda wote
Mwenye makosa ni mteja au ni watoa fomu?? Lakini huu sio mjadala wakuendelea kujadili mm ninachokiomba ni kujua tu miundo mbinu itanifikia ln lkn kunambia misubiri hapo ndo inakuwa kasheshe kwan kusubiri ni kusubiri tu pengine lbd hadi 2025
 
Ninaomba majibu yenu TANESCO

Katika mkoa wa Songwe,wilaya ya Mbozi,Mji wa Vwawa kata ya Hasanga kuna mitaa haijapata umeme mpaka leo.

Mitaa hii ni:Iyela, London,mtakuja na Hasanga.
Katika mtaa wa Mtakuja watu kadhaa waliandika barua na kujaza form kwaajili ya kuomba kuwekewa nguzo,kuanzia mwaka 2018, lakini mpaka leo hakuna majibu.Nataka kujua yafuatayo
1.Mitaa hii ipo ktk mfumo wa REA?
2.Kama haipo ktk mfumo wa REA ni kwanini?
3.Ni kwanin mpaka leo Umeme haujasambazwa ilhali maeneo haya yapo sehemu ya makao makuu ya mkoa?

NB:kuwapatia Umeme watu ni kuongezea idadi ya wateja kwenu.Naomba majibu please.
 
Hili shirika majibu yake tu inaonyesha hawako tyr kuhudumia wananchi haiwezekani mtu anajibiwa etinanatakiwa kusubiri miundo mbinu imfikie maana yake hakuna muda sahh wa hyo miundo mbinu kufika ifike mahala muwe serious na majibu yenu
 
Tafadhali onyesha namba ya simu kwa mrejesho zaidi
 
Naingiza namba za Luku kwenye mita lakini inaandika Error - 77,nifanyeje
JINSI YA KUONDOA ERROR 77 KWENYE MITA ZINAZOANZA NA NAMBA 2421...

ERROR 77

Hii ni error ambayo inapatikana kwenye mita tengano maarufu kama mita za rimoti au CIU ambazo zinafungwa juu ya nguzo na zinaanza na namba ya mita 2421.....

NINI KINASABABISHA ERROR 77

Error 77 inamaanisha kuwa mita yako ya kwenye nguzo na rimoti yako hazina mawasiliano hivyo umeme hauwezi kuingia. Mara nyingi inatokea unapotaka kuweka umeme baada ya kuisha unit.

JINSI YA KUTATUA ENDAPO ITATOKEA

Unatakiwa kuhakikisha kuwa umeme kwenye mtaa wako upo na kama nyumba yako haina umeme yaani unit zimeisha weka betri zenye nguvu kwenye rimoti yako na kisha fata taratibu zifuatazob

[emoji841]Zima switch zote za nyumba yako, hakikisha zote zimezimwa

[emoji841]Washa switch moja tu ya ukutani na chomeka hiyo rimoti kisha bonyeza zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako alafu tena zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako kisha bonyeza ok au enter..

Mfano mita namba yako ni 241234567 Utafanya ifuatavyo *024212345670241234567ENTER

[emoji841]Baada ya kubonyeza ok itaakuandikia GOOD apo sasa weka umeme wako kama kawaida na utapata umeme.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA ZA TANESCO

RUKSA KUSHARE NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI
 
Tafadhali naomba kufahamishwa juu ya nini chanzo cha umeme kukatakata mara kwa tena kwa mda mrefu hasa siku za hivi karibuni.
Je ni ukanda huu tu au Nchi nzima hii hali ipo??








Nauliza kwasababu nategemea umeme huu kuweza kulisha familia,sasa mnapokata bila taarifa maanake mnataka nife njaa au.??
Tafadhali naomba ufafanuzi

Location:Kahama Mjini
 
Nawaheshimu TANESCO makao makuu. Kupitia hii thread nimepata msaada wa namba ya malipo ambayo nilikuwa nikizungushwa Sana na watu wa wilayani zaidi ya nusu Mwaka, lakini baada ya kulalamika hapa, mlinisaidia kuwasiliana nao na mwanzoni mwa mwezi huu nimepata msaada wa namba ya malipo na nimeweza kulipia siku hiyo hiyo! Kwa Sasa BADO nasubiri waje wanifungie umeme.

Nilichokuja kufahamu katika hili, TANESCO makao makuu mpo serious Sana katika utendaji wenu kuhakikisha mnafanikia strategic plan ya serikali kuhusu nishati ya umeme. Kinachowapunguzia kasi ni utendaji legevu wa TANESCO ngazi za chini.

Nashauri katika mfumo wa uongozi wa TANESCO, kuwe na monitoring and evaluation experts ambao watapima na kuratibu utendaji kazi wa watumishi wenu hususani ngazi za chini na ku report kila wiki makao makuu. Mfano, customer care wa TANESCO wamekuwa na kauli na majibu ya kikatili kwa wateja wao, Jambo linalopelekea si tu maudhi na kupungua kwa kasi ya kuenea kwa Huduma ya shirika, Bali pia kupungua kwa Uhusiano mwema Kati yenu na jamii. Mfano, sisi tukipiga simu kuulizia mchakato wa Huduma ulipofikia mnatujibu-jibu Kama mnavyotaka nyie alafu mtarajie tukiona watu wanaohujumu miundombinu ya shirika tutoe taarifa kwenu,Hapana! Lakini kungekuwa na wataalam wanaofuatilia maongezi ya customer care ngazi za chini na wateja na kuyaratibu wangekuwa wanachunga kauli zao
 
wanakuja
 
Tunashukuru sana kwa ushauri tunaendelea kuboresha huduma zetu
 
Yaaani watu wa Moshi tunateseka sana na hili shirika. Kila siku umeme unakatika masaa 12 usipokata mchana unakata usiku. Kwa nini mnatuonea na kama kuna mgao si muwe wazi mseme ili tujipange?
 
Tanesco mkoa wa Tabora kuna shida gani.Maanake umeme mkikatani masaa 10 yanapita mkierudisha ni saa 1 moja mnakata tena kuna tatizo gani?! Tumejaribu kuulizia majibu tunayopewa ni zaidi yanyodo.

Mara wakujibu sisi wenyewe hatujui kama umeme unakatika au mara chimba bwawa lako uzalishe na wewe umeme majibu ni mengi na michafu ya kutosha.tulitegemea kwamba baada ya kupata ushindi wa kishindo na kuwa sisi wenyewe kwenye serikali baada ya kukwamisha na wapinzani miaka 59 kama walikuwepo.

Sasa hivi tutapata maendeleo.Miongoni mwa maendeleo ni kuwa na umeme wa uhakika.Sasa siku hizi imekuwa kazi umeme lisaa li1unakatika masaa 12 sasa hya maendeleo tunayapataje kwa mtindo huu.Mbowe na wapinzani mbona hamuongei au ndo mmeamua mtuache huyu jamaaa atumalize
 
Yaaani watu wa Moshi tunateseka sana na hili shirika. Kila siku umeme unakatika masaa 12 usipokata mchana unakata usiku. Kwa nini mnatuonea na kama kuna mgao si muwe wazi mseme ili tujipange?
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

DESEMBA 17, 2020

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanescoyetu

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu


Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Sikuizi mnakata umeme kila mara wakati mwingine hauna nguvu mnaunguza taa zetu kama kuna mgao mseme tujue tununue solar ma generator. Hata saizi umekatika hapa vikindu mkuranga
 
Bila ushahidi kuwa umejibiwa hivyo, na watu Tanesco, basi mleta mada hii unafanya hila na njama za kutia watu matatani kwa sababu za roho mbaya!
 
Mimi NIMELIPIA umeme tarehe 16/9/2020
Lakini Hadi leo hii Ni tarehe 22/12/2020 umeme SIJAUNGANISHIWA kila nikiwapigia simu WANANIPA kiswahil TU
NIMELIPIA 320,000.wanasema INAHITAJIKA nguzo moja tapping pole.
Wenzangu mtaan wanasema walilipia baada ya mwez mmoja umeme uliwaka.
TANESCO KISARAWE mmezid aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…