Nawaheshimu TANESCO makao makuu. Kupitia hii thread nimepata msaada wa namba ya malipo ambayo nilikuwa nikizungushwa Sana na watu wa wilayani zaidi ya nusu Mwaka, lakini baada ya kulalamika hapa, mlinisaidia kuwasiliana nao na mwanzoni mwa mwezi huu nimepata msaada wa namba ya malipo na nimeweza kulipia siku hiyo hiyo! Kwa Sasa BADO nasubiri waje wanifungie umeme.
Nilichokuja kufahamu katika hili, TANESCO makao makuu mpo serious Sana katika utendaji wenu kuhakikisha mnafanikia strategic plan ya serikali kuhusu nishati ya umeme. Kinachowapunguzia kasi ni utendaji legevu wa TANESCO ngazi za chini.
Nashauri katika mfumo wa uongozi wa TANESCO, kuwe na monitoring and evaluation experts ambao watapima na kuratibu utendaji kazi wa watumishi wenu hususani ngazi za chini na ku report kila wiki makao makuu. Mfano, customer care wa TANESCO wamekuwa na kauli na majibu ya kikatili kwa wateja wao, Jambo linalopelekea si tu maudhi na kupungua kwa kasi ya kuenea kwa Huduma ya shirika, Bali pia kupungua kwa Uhusiano mwema Kati yenu na jamii. Mfano, sisi tukipiga simu kuulizia mchakato wa Huduma ulipofikia mnatujibu-jibu Kama mnavyotaka nyie alafu mtarajie tukiona watu wanaohujumu miundombinu ya shirika tutoe taarifa kwenu,Hapana! Lakini kungekuwa na wataalam wanaofuatilia maongezi ya customer care ngazi za chini na wateja na kuyaratibu wangekuwa wanachunga kauli zao