Pugu eneo gani haswa na namba yako ya simu tafadhali
 
Naona umeme unastua kidogo huku halafu unakata. Inawezekana mmeufanyia kazi ujumbe wangu japo umeme haujawaka
 
Upo umbali kitaalamu unapaswa kuachwa kutoka kwenye miundombinu ya umeme

Nahisi wewe ndio mpungufu wa ubunifu, unatafuta njia fupi ya kutatua tatizo badala yakufikiria mbinu mbadala ya kutandaza nyaya za umeme, huko ndio kunakoitwa akili mgando, dunia inakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na vitendo vya watu kama nyie halafu unaleta majibu mgando!!
 
Mabadiliko ni gharama na muda hivyo tunaomba utuelewe kwa sasa ili kupunguza makatizo ya umeme lazima kuprun miti iliyokaribu na miundombinu
 
Mabadiliko ni gharama na muda hivyo tunaomba utuelewe kwa sasa ili kupunguza makatizo ya umeme lazima kuprun miti iliyokaribu na miundombinu

Ingekuwa mna proon sawa sasa oysterbay masaki MITI imekatwa hadi chini, MITI iliyopandwa Mika 50 iliyopita, hii ni sahihi? Huyo contractor mlimpa terms of reference za kazi zake, au umepata muda kupitia utendaji wake unaoharibu mazingira kwa kiwango cha kutisha!
 
Asante sana TANESCO kwa rapid response
yenu, tayari umeme umerudi na tunayaangaza maisha sasa pamoja nanyi
 
TAARIFA YA KUOMBA RADHI KATIZO LA UMEME .

Shirika la umeme TANESCO Mkoa wa Morogoro linaomba radhi kwa katizo lililojitokeza Asubuhi ya leo kama ifuatvyo:

MUDA :11:35 Alfajiri.
Siku :Jumamosi
Tarehe :26/07/2020.
Sababu: ni hitilafu iliyojitokeza katika transfoma kubwa ya T4 katika kituo cha kupokea na kupooza umeme Msamvu.

Maeneo yaliyoathirika ni :Maeneo yote ya Wilaya ya MOROGORO, Mikese, Mvuha, Kisaki, Wilaya yote ya Kilosa, pamaoja na baadhi ya maeneo yanayotumia laini hizo .

JUHUDI zilizofanyika ni pamoja na :team ipo site kuhakikisha huduma inarejea kwa uharaka zaidi.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakao kuwa umejitokeza.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO - MAKAO MAKUU
DODOMA




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Tanesco makao makuu imulikeni Tanesco Kibaha ( Mkoa wa Pwani) kumejaa rushwa ambayo inaikosesha serikali mapato kwa kuchelewesha kwa makusdi kuwafanyia wateja survey. Muulizeni meneja ni wateja wa ngapi wameunganishiwa umeme kwenye mradi uliokamilika wa nguzo za zege? Na ni kwa nini wateja wengi waliomba kuunganishiwa umeme hawajapatiwa huduma hiyo, isipokuwa wale wachache waliokubali kutoa rushwa ya shilingi laki moja mpaka laki mbili na nusu.
Mradi uko kata ya viziwa ziwa unaanzia palijengwa chuo cha Siasa kuelekea eneo linalojulikana kama Shana Town.
 
Asante kwa taarifa ndugu mteja, tutaomba namba yako ya mawasiliano kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…