Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Huku haujakata hata sekunde tokea jana asubuhi hadi naandika hapaVip huko ulipo
Tunashukuru sana mpendwa mteja wetu, Kwa wateja wanaotoa taarifa kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii tunawasihi kutoa taarifa kamili ili zituwezeshe kuwahudumia.MREJESHO/SHUKRANI
Kwa dhati ya moyo wangu niwashukuru jamiiforum kwa kuanzisha huu mtandao na TANESCO kwa kutatua kero zetu hapa kuhusu umeme.
Niliripoti hapa siku kadhaa nyuma kuwa surveyor amepima ila nina miezi miwili sijapata control no.
TANESCO hapa jukwaani waliomba namba yangu ya simu na mahali nilipo kwa ufuatiliaji.
Kesho yake tu nikapigiwa simu na branch yangu kuwa ndani ya siku mbili nitapatiwa control no na kweli leo hii nimepatiwa na kulipia 27, 000 tu.
Nawapongeza sana kwa namna mlivyofanyia kazi malalamiko yangu na nina amini kuwa ndani ya muda mfupi ujao nitapata huduma ya umeme.
Pamoja na kuwa sijajua muda maalumu wa kupatiwa huduma baada ya kulipia ila angalao kwa kupata control no nimepata amani
MUNGU AWABARIKI SANA SANA TANESCO MUENDELEE KUTUANGAZIA.
Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidiMorogoro mnakata umeme bila taarifa kila siku. Ustaarabu ni muhimu kazini ikiwa kweli mnamaanisha kulisogeza taifa mbele. Mkitoa taarifa mtasaidia watu kupanga budget zao vizuri na hivyo kuepuka gharama za ziada.
Mfano mtu kanunua nyama ya kutumia kwa wiki moja, anafika nyumbani na umeme mnakata- huyo mnakuwa tayari mmemsababishia hasara. Lakini mngemtaarifu asingenunua nyama nyingi kiasi hicho.
TUKIFANYA KAZI KWA MOYO NA USTAARABU - TAIFA LITAENDELEA HARAKA. Lakini tukiendeleza uenyeji huu, tusishangae wakoloni wakaja kutuendesha tena.
@TANESCO hawawezi kukujibu hapa.Hbr, shida yng ni hii ni hivi majuzi walikuja tanesco kubadilisha mita za zamani na kuweka mpya. Ss ntk nijue je mtarudisha unit zetu ambazo tulinunua kwny mita ile ya zamani au la????
Dah htr mana umeme tuliweka wa elfu 50 hlf tukatumia siku mbil wamebadilisha mita. Tumefstilia wamesema had wik mbl zipite mh yn naona kbs hii n dalili kua hatutarudishiwa.@TANESCO hawawezi kukujibu hapa.
Hesabuni maumivu tu.
Hapo jitahidi kumkumbusha na kumsumbua sumbua surveyor wako na kama ofisi zipo karibu uwe unaenda mara kwa mara kuulizia. Unaweza kaa hata miezi mitatu ndugu ndo upate control noUkishaja form ya kuomba kuunganishiwa umeme na surveyor ashakuja kuchek inachukua muda gani mpaka kuambiwa ukalipie
TANESCO leo jpili watu wako ibadani mmekata umeme Kimara mwisho!
Hivi haya malalamiko mengi nnayosoma humu hasa ya wakazi wa Dar hamuyaoni?
Niliwauliza kuwa kama hamuwezi kuihudumia Dar es salaam vizuri,legitimacy yenu kuitwa shirika la umeme Tanzania iko wapi then?maana huu ndio mji wa mfano.Huwezi kushindwa kuihudumia Dar ukatudanganya unaweza kuihudumia Kigoma.Hamna kitu hicho.
Ilipaswa kuwa kosa la jinai umeme kukatika Dar.Lakini soma malalamiko humu,majority ni sisi wakazi wa Dar!Ndio watumiaji wakubwa zaidi wa umeme,tena tunautumia kuzalisha mali,iwe jtano iwe jpili,lakini hamtuheshimu,mnakatakata umeme hovyo hovyo na mko consistent kwenye hilo!mko imara katika jambo lililo kinyume na kazi yenu.Huu ni uhalifu.
Mimi pekee soma post zangu kuhusu ukatikaji wa umeme kimara mwisho pekee,ni miaka na miaka nalalamika,lakini hadi leo nipo hapa bado natoa taarifa kila baada yamda mfupi.siwezi kukaa wiki mbili kabla ya kukerwa na umeme na kuja humu.Inashangaza sana.
Tumepokea taarifa wataalamu wetu wanaendelea kufanyia kazi tatizo lilitokea eneo la Mbezi na Kimara huduma itarejea.Tunawaomba radhi sana
Mlikata jpili iliyopita,mlikata jtano,leo jpili nyingine mfululizo mmekata umeme Kimara mwisho hivi ninavyoandika.Hii ilikuwa jpili.
Leo jtano kuna nini?
Ndugu mpendwa Mteja wetuMlikata jpili iliyopita,mlikata jtano,leo jpili nyingine mfululizo mmekata umeme Kimara mwisho hivi ninavyoandika.
TANESCO
Kwa hiyo nyie tanesco humu mnachagua watu wa kujibu??? Wengine tumeuliza maswal kimya ila wengine mnajibu. Ss kuna maana gn ya kuanzisha huu uzi si bora muufute tu sbb hamtatui hizo kero za wananchiHbr, shida yng ni hii ni hivi majuzi walikuja tanesco kubadilisha mita za zamani na kuweka mpya. Ss ntk nijue je mtarudisha unit zetu ambazo tulinunua kwny mita ile ya zamani au la????
Asante50333482180870220614