TANESCO mkoa wa Arusha mtaa wa Laizer mkandarasi wameweka nguzo sasa mwezi wa pili ushapita hatujui kinachoendelea tukienda tanesco ofisi ya mkoa hawatoi jibu la kueleweka je ni lini wataleta waya na wananchi kuunganishiwa umeme?

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Nimeshalipa kodi ya mejengo ya mwaka 2021/22 tangu mwezi wa Aprili mwaka huu. Je, nikinunua umeme Tanesco au TRA mtajuaje kuwa sitakiwi kukatwa tena kwa mwaka huu na ninaona nakatwa?
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Mkuu TANESCO hili ni tatizo la line nzima.
Umeme unazimwa huko Ubungo.
Kimara mwisho pana line kama tatu hivi.

Line inayosumbua ni hii inayoleta umeme Kimara Darajani, Kituo cha Polisi, Dawasco, Sokoni, Kanisa Katoliki, hospitali ya Kimara, Matangini, TRA, KAM College, Mavurunza, na mwisho wake ni Makaroni.

Ipo upande wa kulia wa barabara ya Morogoro kama unakwenda Mbezi.
Zamani Kimara ilikuwa na line moja yote.

Mkazitenganisha kulia na kushoto ili kusiwe na waya zinazovuka barabara.
Kwa hiyo ukiwa kama unakwenda Mbezi, upande wa kushoto kuna line kubwa inatoka Ubungo mpaka Mbezi huko.

Hii line haisumbui kabisa umeme.

Line inayosumbua ni ya upande wa kulia ambayo inatokea Ubungo inatembea na huo upande wa kulia hadi Kimara mwisho inaishia makaroni.
Hii ndio inasumbua mno kukatika ivyo umeme.

Post yangu hapo juu iwe tu mfano kwako uone kiwango cha ukatikaji umeme kilivyo. Nilikwambia jpili ya juzi mlikata, mkakata tena jtano, na jpili ya jana mkakata tena.

Sasa hivi nnavyokuandikia hii jtatu leo hakuna umeme tena ushakatwa.
Inasikitisha sana. Ni tatizo la muda mrefu.

Tangu October mwaka jana hali imekuwa hivi. Too much.
Ukiwapigia tanesco Mbezi hawaishi sababu mara tunakata miti, mara hitilafu, mara sijui nordic feeder imefanya nini, sasa sisi inatuhusu nini?

Sisi tunataka huduma endelevu ya umeme. Mbona wenzetu upande wa pili umeme umetulia watu wanakaa hata mwezi haujakatika?

Line yetu ina shida gani isiyotatulika?
Mnatuumiza sana. Huu umeme tunafanyia kazi za kupata kipato, hatuwashii taa usiku tuu wazee!
Badilisheni mindset zenu hizo.
 
Tanesco Kwa heshima na taadhima naomba kueleweshwa gharama za kupatiwa Umeme wa rea vijijini.

Gharama zote kuanzia surveyors, form Kama kweli inauzwa na gharama zingine Kama zipo maana duuh!
 
Tanesco Kwa heshima na taadhima naomba kueleweshwa gharama za kupatiwa Umeme wa rea vijijini.
Gharama zote kuanzia surveyors, form Kama kweli inauzwa na gharama zingine Kama zipo maana duuh!
Form hauzwi, na malipo yote yanafanywa kwa kupitia control number utakayapatiwa na ofisi za eneo lako.
 
Hawa waajiliwa wenu wanaboa Kila huduma mpaka utoe rushwa
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Jina Zahoro Kombo na Henry Lusoba

Eneo
Tegeta Boko
Wilaya
Kinondoni
Namba ya simu
0768590175
Tatizo
Tumelipia umeme toka mwezi wa 7 ila mpaka leo hatujafungiwa kila mara tunaambiwa wiki wiki hii mara waya zimeisha mara mita zimeisha
Toka lini
Mwezi wa 7
 
Tarehe 7 mwezi wa ngapi Mkuu?
 
Tumaona mwezi tunaifatulia tafadhali
 
Je uliandika namba gani kwenye form ta maombi ya umeme hii haipo
 
Mi naomba kufahamishwa tu, je kuna muda maalum wa mtu akishafanyiwa survey hadi kupata control no?

Na je ni ndani ya muda gani unatakiwa tangu kupata control no hadi kuotiwa huduma ya umeme kama panahitaji nguzo mbili?

TANESCO mkitupatia huu muongozo mtakua mmetusaidia sana na kutufanya tusiwe walalamishi hadi muda husika utakapokua umeptia.

Maan mwingine analipia leo kuanzia kesho anaanza kulalamika
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Nilichoomba ni muongozo tu mkuu. Maana ni wiki ilopita 3/9 ndio nimepata control no na kulipia. Je natakiwa kusubiri kwa muda usiozidi wiki/miezi ili kupatiwa huduma.

Ili muda tajwa ukipita nianze ufuatiliaji wa karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…