Ni wiki ya pili sasa hatuna umeme,BUSEGWE BUTIAMA transformer yenu iliharibika baada ya nyie kutoifanyia maintenance kwa miaka. Kila mkija mnazunguka zunguka na lori lenu mnaangalia transformer kisha mnaondoka.
Simu hampokei na mkipokea mmekuwa waongo mno. Hapa kuna taasisi zaidi ya tatu zinazotegemea umeme kupump maji, hivi tutaishi vipi bila maji?
Swala la nyie kuja na kuunganisha transformer ya karibu ikasambaza umeme mnashindwaje?
Mita zingine mmeweka juu ya nguzo na umeme ukiisha zinajilock hadi mje mpande juu ya nguzo ndo mzifungue. Mkiitwa makaa siku mbili ndo mje, mara ooh hakuna usafii MUNGU ANAWAONA
Ukitaka kuungiwa umeme ndo usiseme, mnataka mbebelezwe miezi miwili.
TANESCO KERO NA MATESO YAMEZIDI HAYAVUMIIKI