[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Imebidi tu nicheke $#&&$&£¥₩€&%!
 
acha ujinga jamaa
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Nimejaza form ya kuomba kuunganishiwa umeme hii ni week ya tatu sasa sijapata control number naambiwa kuna network problem. Pia nimeambiwa hata nikilipiwa itanichukuwa zaid ya miezi sita kuunganishiwa umeme kwa sababu mita hazipo ni kweli
 
Naomba kujuzwa, je kisheria/kwa utaratibu wa TANESCO mteja baada ya kulipia huduma ya mteja mpya kwa control no anatakiwa kupatiwa huduma ya umeme ndani ya kipindi kisichopungua wiki/miezi mingapi kama site inahitaji nguzo?

Tanesco mkitupa huo muongozo hatutakua wasumbufu tutasubiri kwa amani.

Binafsi nimelipia tar 03/09/2021 naendelea kusubiri kama nilivyoambiwa kila namba ngeni ikiita najua tanesco kupokea tofuti
 
Kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja mteja aliyepo ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo itakayomuunganishia umeme anapaswa kufungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi, mita zaidi ya 30 hadi 100 ndani ya siku 60 za kazi na zaidi ya mita 100 ni ndani ya siku 90 za kazi
 
Asante sana kwa muongozo. Kwangu ni kama mita 40 so itakua ndani ya miezi miwili maana panahitaji nguzo mbili.

Inaumiza sana una hela mfukoni halafu unalala gizani, hela ipo, fridg ipo lakini inaliwa na panya hakika kwa utaratibu huu TANESCO mmetuweza
 
Tunaposema ndani ya siku kadhaa haina maana mpaka zifike hii ni kuruhusu waliolipa mbele yako kupatiwa huduma ndio tukufikie wewe
 
Mimi kwangu surveyor alikuja 4/7/2021, baada ya kulalamika hapa na kutoa taarifa ndio nikapewa control no tar 3/9/2021 so nikijumlisha miezi miwili ya kisubiri mchakato huu utakua umetumia kama miezi mitano hadi kupatiwa huduma.

Mnaanza kuhesabu siku niliyopata control no au siku surveyor aliyopima? Maana kuna foleni mbili hapo
 
Muda wa kufingiwa unazingatia muda uliofanya malipo
 
Muda wa kufingiwa unazingatia muda uliofanya malipo
Sawa mkuu asante sana kwa muongozo, naiheshimu mno jf maana baada ya kuripot hapa ndio nilipatiwa control no bila hivyo bado ningekua nasota.

Nitarejea tena kwako kama mpka muda tajwa ntakua sijapatiwa huduma mkuu
 
Sawa mkuu asante sana kwa muongozo, naiheshimu mno jf maana baada ya kuripot hapa ndio nilipatiwa control no bila hivyo bado ningekua nasota. Nitarejea tena kwako kama mpka muda tajwa ntakua sijapatiwa huduma mkuu
Usiwe na shaka tutakuangazia maisha yako hivi punde kaa mkao wa kufurahia maisha na umeme
 

Naona umejibu kwa kujiamini kabisa wakati mimi nimelipa toka april..baada ya kulalamika kuna dada anaitwa Lucy akanipigia,akaniahid July itakuwa tayar, sasa hiv nikimpigia simu hapokei...nikituma text hajibu
 
Naona umejibu kwa kujiamini kabisa wakati mimi nimelipa toka april..baada ya kulalamika kuna dada anaitwa Lucy akanipigia,akaniahid July itakuwa tayar, sasa hiv nikimpigia simu hapokei...nikituma text hajibu
Tafadhali tupatie taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Umelipia lini
 
Hizi mbwembwe zidumu huku maana watanzania kutiririka matatizo ndo kwao .msikumbie next year niwakute humu
 
Tanesco embu mtusaidie namna ya kupata huduma ya umeme.

Utaratibu wenu kama ndo huo, basi wengine tutaishi bila umeme kabisa.

Nilijaza fomu ya maombi ya kupewa huduma almost karibu sasa miaka mitatu.

Surveyor wakaja na kudai wanatengeneza ramani.

Tulisubiri kuona hatua ambayo ingefuata lakini ajabu tulishangaa kuona nguzo zinachimbiwa maeneo mengine na wakapewa umeme.

Baada ya kufuatilia Tanesco, tuligundua kwamba ile fomu yeti ilikuwa blank na hakukuwa na chochote ambacho Tanesco walifanya. Hakukuwa hata na hiyo ramani ambayo surveyor walidai kuifanya .

Baada ya malalamiko walitumwa surveyor wengine na kufanya Tena hicho kinachoitwa ramani.

Ajabu Sasa, baada ya hapo tulidhani tutapewa huduma hii mara nguzo zitakaoopatikana maaba hili ndo lilikuwa excuse ya Tanesco/ Rea kwa eneo letu.


Nguzo zimekuja nyingi sana, lakini tumerukwa Tena na hata ukifuatilia ni siasa tu.

Tunaambiwa Ili kupata nguzo ni Lazima tujiongeze.

Nimeshuhudia umeme ukipindwa kuroka hata eneo jingine na mtu anawekewa eti katoa sh 50000.

Nguzo zinasafirishwa usiku kwenye maeneo ambayo watu wanatoa chochote.

Kuna watu ambao tunao mtaa mmoja kwa maana ya barabara moja Wana umeme walioipata kutoka mtaa wa nyuma yetu. It

Umeme unavutwa kwa nyuma na mtu anapewa sababu katoa pesa.

Ukiwaambia Tanesco utasikia wanaweka lawama kwa mkandarasi na wakati mwingine wanasema ni Ramani yao ndo inaonesha waweke wapi umemw na waache wapi.

Kwa eneo letu ukuja utashangaa maana kwingine kote umeme umesambaa ni eneo letu TU ndp halina umeme. Tumezungukwa na umeme pande zote kasoro eneo letu tu.

Mimi nimekataa kutoa rushwa maana dhamiri yangu hainitumi kufanya hivyo

Sasa je tufanyeje site ambao hatuko kwenye category ya kutoa 50,000.

Siku mkija nitawaonyesha umeme ulivyofungwa kimagumashi kwa watu waliotoa chochote.


Kama ni sera ya kuwahonga wanaoitwa wakandarasi, twambieni pia.

Vinginevyo tufanyeje????




.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Tanesco mnafanya kazi nzuri ongezeni ufanisi kwenye kila kitu tutafika nchi ya ahadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…