Tanesco embu mtusaidie namna ya kupata huduma ya umeme.
Utaratibu wenu kama ndo huo, basi wengine tutaishi bila umeme kabisa.
Nilijaza fomu ya maombi ya kupewa huduma almost karibu sasa miaka mitatu.
Surveyor wakaja na kudai wanatengeneza ramani.
Tulisubiri kuona hatua ambayo ingefuata lakini ajabu tulishangaa kuona nguzo zinachimbiwa maeneo mengine na wakapewa umeme.
Baada ya kufuatilia Tanesco, tuligundua kwamba ile fomu yeti ilikuwa blank na hakukuwa na chochote ambacho Tanesco walifanya. Hakukuwa hata na hiyo ramani ambayo surveyor walidai kuifanya .
Baada ya malalamiko walitumwa surveyor wengine na kufanya Tena hicho kinachoitwa ramani.
Ajabu Sasa, baada ya hapo tulidhani tutapewa huduma hii mara nguzo zitakaoopatikana maaba hili ndo lilikuwa excuse ya Tanesco/ Rea kwa eneo letu.
Nguzo zimekuja nyingi sana, lakini tumerukwa Tena na hata ukifuatilia ni siasa tu.
Tunaambiwa Ili kupata nguzo ni Lazima tujiongeze.
Nimeshuhudia umeme ukipindwa kuroka hata eneo jingine na mtu anawekewa eti katoa sh 50000.
Nguzo zinasafirishwa usiku kwenye maeneo ambayo watu wanatoa chochote.
Kuna watu ambao tunao mtaa mmoja kwa maana ya barabara moja Wana umeme walioipata kutoka mtaa wa nyuma yetu. It
Umeme unavutwa kwa nyuma na mtu anapewa sababu katoa pesa.
Ukiwaambia Tanesco utasikia wanaweka lawama kwa mkandarasi na wakati mwingine wanasema ni Ramani yao ndo inaonesha waweke wapi umemw na waache wapi.
Kwa eneo letu ukuja utashangaa maana kwingine kote umeme umesambaa ni eneo letu TU ndp halina umeme. Tumezungukwa na umeme pande zote kasoro eneo letu tu.
Mimi nimekataa kutoa rushwa maana dhamiri yangu hainitumi kufanya hivyo
Sasa je tufanyeje site ambao hatuko kwenye category ya kutoa 50,000.
Siku mkija nitawaonyesha umeme ulivyofungwa kimagumashi kwa watu waliotoa chochote.
Kama ni sera ya kuwahonga wanaoitwa wakandarasi, twambieni pia.
Vinginevyo tufanyeje????
.