"Maintanance na wewe kukosa huduma havieleweki kabisa"'hasa ukizingatia umeme umenunua upo nyumbani wa kutosha, bahati mbaya wabongo akili tunazo ila vitendo vya kutekeleza maarifa ya akili zetu ndio hatuna that's why tunachezewa.
 
Kuweni wapole tuu kama makao makuu ya tanesco wamewasha generator ije kuwa nyinyi? Kila nikijarabu kumsahau jiwe Tanesco wananitonesha tena
 
Ratiba ya Mgao inaonyesha mtaani kwangu Leo ilikua siku ya mgao yaani Umeme hautokuepo ila upo Mpka mda huu.!
 
Katika suala la kukata Kodi halijakaa vizuri Nyumba niliyopanga kila mpangaji anatumia LUKU yake inakuaje wote tukatwe kodi ya Nyumba rekebisheni hili
 
Katika suala la kukata Kodi halijakaa vizuri Nyumba niliyopanga kila mpangaji anatumia LUKU yake inakuaje wote tukatwe kodi ya Nyumba rekebisheni hili
Hii anashauriwa kutoa taarifa TRA kwa uhakiki ili uhalali wa kulipia au kutolipia ufahamike
 
TANESCO WILAYA YA TEMEKE kuweni serious kidogo.

Mmetukatia umeme toka asubuhi saa 3 na mpak sasa hamjarudisha

Mgao gani huo?????

Eneo mlilokata ni lote kuanzia KTM mbagala , mbagala sabasaba,kipati,kizuiani na mbagala rangi 3.

Hebu fanyeni kuwasha.
 
Kiongozi tangazo Lao si linasema watarudisha saa sita usiku,au hukuliona?
 
Shikamoo tanesco saa sita juu ya alama,mmeturudishia umeme, mbagala, tumepamba na joto pamoja na mbu.
 
Ukiangalia matangazo ya mgao inaonyesha kwamba ikiwa zamu ya kukatika basi watakata saa mbili asubuhi na kurudisha saa sita usiku hapo ni upige pasi nguo za ofisini, uniform za watoto, upashe misosi Kama unatumia umeme uweke breakfast kabisa na kuchaji simu mapema.

Balaa na nusu wacha tuwavumilie kwa hizi siku kumi halafu tuone kama umeme hautatengemaa watakuja na kisingizio gani la sivyo tunang'oa transformer zote wasituchukulie poa.
 
Ratiba inasema hadi siku ya jumatatu tarehe 7,ina maana kadhia hii ya siku 10,siku mbili mbagala.
 
Nikitoa kitu kidogo mnaweza mkaniwekea hapa ratiba ya mgao wa umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…