Mgao wa umeme upo tokea Makamba awe waziri!
Ila nauliza kwa sisi watu wa Temeke jana tokea asubuhi umeme haukuwepo maeneo mengi ya Temeke wakarudishwa jioni baada ya saa kama moja wakakata tena!
Sasa nauliza huu mgao rasmi uliotangazwa na MAHARAGE ndio huu umeshaanza sasa au utakaoanza Februari mosi?
Maana wasiwasi wangu kweli siku kumi zitatosha? Maana waziri Makamba amekuwa hasimamii kauli zake! Visingizio kibao mara mitambo chakavu, mara maji hayatoshi mara kitengo cha habari hakilitetei shirika la TENESCO!
Naomba kujua!