TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Upo utaratibu sahihi wa kuweka wateja kwenye makundi yanaendana na matumizi yao, hivyo haupaswi kuwa na hofu kwa kuwa manunuzi yako yanaonekana kwenye mfumo, Weka namba yako ya mita na swali kuhusu mita yako tafadhali
Unaelimu gani afsa habari mpya!?
 
Basi nitaenda kuomba huduma hii jirani na ofisi za tanesco nikijibiwa tofauti nitarudi kwenye ukurasa huu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Tafadhali tambua wateja wa vijijini ndio wanaokedhi kundi la matumizi ya D1 yaani chini ua unit 75 kwa mwezi kwa mujibu wa taratibu na muongozo uliopo,
 
Naomba kuuliza, nimeunganishiwa umeme single phase.

Ninataka kuunganishiwa/ nibadili kuwa three phase kwa akiji ya mashine ya kusaga, wire za three phase zipo umbali wa nguzo 10, 1:malipo/makadirio ya gharama yatakuwaje
2:Taratibu za kubadili Single phase kwenda three phase zikoje
 
Naomba kuuliza, nimeunganishiwa umeme single phase.
Ninataka kuunganishiwa/ nibadili kuwa three phase kwa akiji ya mashine ya kusaga, wire za three phase zipo umbali wa nguzo 10, 1:malipo/makadirio ya gharama yatakuwaje
2:Taratibu za kubadili Single phase kwenda three phase zikoje
Tafadhali fika ofisi za eneo ambalo nyumba husika ipo, omba kufanyiwa Phase upgrading, utapatiwa form ya maombi ya umeme kama kawaida, utaweka mchoro kupitia kwa mkandarasi wako wa umeme kisha utairudisha tutakupimia na kukupatia gharama za kulipia, ukishalipia tutaondoa mita ya njia moja ( Single Phase) na kufunga na njia tatu ( Three phase)
 
Mgao wa umeme upo tokea Makamba awe waziri!

Ila nauliza kwa sisi watu wa Temeke jana tokea asubuhi umeme haukuwepo maeneo mengi ya Temeke wakarudishwa jioni baada ya saa kama moja wakakata tena!

Sasa nauliza huu mgao rasmi uliotangazwa na MAHARAGE ndio huu umeshaanza sasa au utakaoanza Februari mosi?

Maana wasiwasi wangu kweli siku kumi zitatosha? Maana waziri Makamba amekuwa hasimamii kauli zake! Visingizio kibao mara mitambo chakavu, mara maji hayatoshi mara kitengo cha habari hakilitetei shirika la TENESCO!

Naomba kujua!
 
Najiuliza kama siku za hivi karibuni tulikuwa tunakosa umeme kwa zaidi ya masaa 48, tukidhani ni mgao wa umeme; sasa mgao orijino wa umeme uliotangazwa na viongozi utakuwa wa namna gani?
 
Uzalendo haununuliwi kwa pesa. Hawa watu hawana uzalendo na taifa hili na watu wake zaidi ya kuiba.
 
Back
Top Bottom