Mimi nilishalipia umeme wa 27,000 x2 kwaajili ya nyumba zangu mbili kijijini huko kigoma lakini siishi huko nimekuwa nikizungushwa na fundi aliyejifanya ni fundi wa REA bila mafanikio nikawasiliana na tanesco kigoma wakasema hawamjui huyo fundi baadae fundi huyo kishoka wa REA akanipigia kuwa anazo mita za nyumba zangu ila wire wa kuingizia moto ndiyo hamna hivyo nimtumie hela 50,000/= ili mkandarasi wa REA aje nao,nikatuma hiyo hela lakini hakuna kilichofanyika hadi leo.

Baadae nikapata namba ya mkandarasi wa REA nikamueleza kila kitu kuwa kuna fundi umeme anadai ni wa REA ana mita zangu na nimeshampa hela ya waya mkubwa 50,000/= kama ulivyodai lakini sijaingiziwa huo umeme na mita anazo inakuwaje?

Mkandarasi huyo wa REA alinifokea sana na kunitukana kuwa naleta ujuaji hivyo sitafungiwa umeme kamwe hata kama nimelipia.

Napenda kujua swala hili nalifikisha wapi kwa usumbufu na je ni sawa kinachofanyika?

Napia huyu kishoka alipataje hizo mita zangu?
 
Nyumban kwangu kila umeme unapokua mdogo umeme unakata wakati kwa majirani unawaka
Niliita fundi kuangalia lakini ameniambia wiring haina tatizo

Mimi natumia mita ndefu za tanesco zenye kutoa alarm majirani wanatumia vile vi box vidogo
Naomba ufafanuz
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Je umewahi kuitolea taarifa? Kama ndio tafadhali onesha namba ya taarifa kwa hatua zaidi
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
TANESCO Tunauliza tena Vifaa hasa Mita za Luku zinafika lini? Watu tumelipia tokea Mwaka Jana mwezi wa 10 na 11 lakini Leo tunaenda mwezi wa 6 Bila kuunganishiwa Huduma ya umeme.

Kila tunapofatilia katika ofisi za Ilemela Mwanza tunaambiwa Vifaa hakuna hivo tuendelee kusubiria... Wale wote tuliokua tumelipia mwaka Jana walitutukia SMS kua tutapatiwa huduma kabla ya tarehe 30/03/2022 lakini Leo ni April na hatujatumiwa SMS tena ili kama tuendelee kusubiri hadi lini?

Apa nafanya mpango wakupata No ya Waziri wa Nishati My January Makamba ili labda yeye ndo atatupa jibu sahihi kua inawezekanaje mteja asubirie zaidi ya miaezi 6 au mpaka tutoe Rushwa???
 
Msaada nimenunua umeme mara mbili ndani ya mwezi mmoja kimakosa ,nikatolewa KWENYE MATUMIZI ya kawaida!!
 
TANESCO hivi Wananchi wakiamua kuwafungulia kesi dhidi ya ucheleweshaji mnaoufanya makusudi wa kutokuwaunganishia wateja umeme ndani ya siku 14 mtapona kweli? Ngoja nimtafute wakili msomi level za Kibatala anipigie mahesabu tokea October last year to date napaswa kulipwa shilingi ngapi? Huenda nikalipwa ela ndefu kwakukiuka mkataba wenu... Kongole kwake CAG kwakututoa shimoni
 
 
MIMI NILIAMBIWA INACHUKUA SIKU 60 NILIPOENDA KUCHUKUA CONTROL NO. SASA NAJIULIZA HIVI KWELI NI FAIR? NAOMBENI TANESCO MBORESHE HUDUMA ZENU MAANA NIMECHOKA KUSUBIRI SABABU NIMESHALIPIA GHARAMA ZA KUUNGANISHIWA UMEME ZAIDI YA MWEZI SASA.
 
Hivi nyie tanesco mna roho ya uchawi ndani yake? Maana mtu anaehatarisha maisha ni kama mchawi.

Kwa nini mnapewa taarifa za hatari afu mnazichukulia kimasihara au furaha yenu mpaka muone maisha na Mali za watu zimepotea?

Ilitolewa taarufa juu ya nguzo kuoza na kubend ikiwa karibu na nyumba, mbaya zaidi nguzo ipo kwenye kimwinuko ikiface nyumba na wataalam wenu walikuja kuhakikisha na kwenye taarifa yenu wameeleza jinsi nguzo inavohatarisha maisha ya wakazi katika nyumba husika lakini siku mnaishia kupromice mnakuja mnakuja kuanzia kutolewa kwa taarifa April 1 na mafundi kufika within 2days kushuhudia na kuiandikia taarifa.

Namba ya taarifa ni 0135 nyumba ipo eneo la mbezi kibanda cha mkaa. Jaribuni kutofautisha taarifa za kuzuia hatari na taarifa za marekebisho and prioritize them. Na mvua hizi ni risk zaidi
 
Huduma bora kwa Tanesco ya Tanzania au ya nchi gani?
Napenda kuwapa pongezi kwa huduma zenu bora , namaswali mawili kwenu (1) ningependa kujuwa viwango vya malipo ya umeme vinakwaje mfano mimi natumia unit 65 kwa mwezi na anae tumia unit 80 wote ni sawa.
 
Hongereni Tanesco kwa kuanzisha mfumo mpya wa kufanya maombi ya umeme mtandaoni.

Lakini rekebisheni kwenye kipengele Cha kuulizana majina ya kati ya mama na taarifa nyingine binasfi.

Kingine kama huna kitambulisho Cha taifa/NIDA uwezi homba umeme, si Kila mtanzania ana namba ya NIDA.

Rekebisheni hapo Kila mtu ilimradi ana kitambulisho chochote halali awezi kupatiwa huduma ya umeme.
 
Mimi niwape pongezi kidogo. Huku mitaa ya kigamboni toangoma mmejitahidi hajmakata kipindi cha mvua hizi za uchwara. HONGERENI SANA.
 
Ibrahim Juma nipo Wilaya ya Newala, namba ya cm 0719496951.

Kuna tatizo kweny nyumba yangu, umeme mdogo taa zote na vifaa ningine havifanyi kazi, jirani zangu wote umeme upo vizuri.

Pia mita inatoa mwanga wa bluu then inazima, haiwaki taa ile nyekundu.
 
Ibrahim Juma nipo Wilaya ya Newala, namba ya cm 0719496951.

Kuna tatizo kweny nyumba yangu, umeme mdogo taa zote na vifaa ningine havifanyi kazi, jirani zangu wote umeme upo vizuri.

Pia mita inatoa mwanga wa bluu then inazima, haiwak taa ile nyekundu.
#TANESCO
 
Nyie jamaa majiendeshaje kibiashara wakati watu wanalipia umeme wenu kwa zaidi ya miezi miwili na hamuwafungii umeme? kungekua na mshindani mngefanya hivyo? imagine watu wamelipa hela zao tena wamelipa kwa gharama mpya wanambwela mbwela miezi kadhaa no service na wala hawahitaji nguzo wengi wao
 
TANESCO DODOMA JIJI MNAHUJUMIWA NA KISHOKA MWENYE NAMBA HII 0785675861..ameisajili kwa jina la mwanamke ila yuko na watu nyuma wasio waaminifu ambao humtuma kuunganisha umeme pasipo fuata taratibu,kuunga kuunga waya vipande vipande kwenye nguzo ambao hatari kwa nyumba za watu..Nguzo kuwekwa hovyo hovyo

pia watu wengi wametapeliwa baada ya kuwaletea nguzo kinyume na taratibu na kusababisha watu hao kushindwa kuunganishiwa umeme wanapoenda kulipa gharama za mita..(maana huwachangisha fedha na pia huwashawishi kwamba wataungiwa mapema huduma) kawaliza wengi kata ya chidachi,mkonze na mpunguzi
inaonekana kuna kikundi kipo nyuma yake
MKIMWEKEA TEGO MTAMKAMATA MAPEMA MNO SABABU ANAPENDA SANA HELA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…