TANESCO ofisi ya Nyakato Ilemela mbona mnakua wasanii sana,watu tumelipia umeme tokea mwaka Jana mwezi wa 10 huu ni mwezi wa 6 sasa hatujaunganishiwa umeme ,kazi kuomba rushwa ila huduma hamleti. Fisi maji nyie leteni umeme
 
Nyumbani kwangu kuna tatizo la mita yaani unit zipo lakini umeme hauwaki nikiongeza unit zinaingia vizuri tuu nikiangalia unit zinaoonyesha vizuri lakini umeme ndani hauwaki kwenye rimont yake inawaka taa moja nyekundu na pia kuna mshale umenyanyuka juu badala ya kunyooka nimetoa taarifa nikarekebishiwa lakini linajirudia tena mwanzoni ulikuwa unakata kwangu tuu baada ya muda unarudi na imekuwa hivyo mara nyingi sana ila mara hii ndio imekata mazima tatizo ni nini?

pili mimi matumizi yangu kwa mwenzi yapo chini ya unit 56 mbona meter yangu ni tarif 1?

umeme wa sh.10000 napata unit 28 kwanini na mimi niko chini ya unit 75za tanesko kama vigezo vyao nifanye aje ili nipate haki ya kupata tarif 4 ?
 
Wakuu naomba namba ya simu call centre nina shida ya umeme
 
TANESCO kariakoo baadhi ya mitaa na nyumba hazina umeme tangu jana
Umati wa watu na sikukuu hizi mtafanya watu wazimie law joto
 
Mvua zinanyesha, mabwawa yamejaa, umeme ndo kwanza unakatika hovyo hovyo.

Kipindi cha kiangazi mnasingizia maji kupungua. Haya sasa tafuteni sababu.

RIP Magufuli
 
Naomba kutoa malalamiko kidogo kuhusiana na Tanesco igunga, uchunguze ufanyike inaonekana Tanesco igunga inanuka sana rushwa na baadhi ya viongozi wake wanakata umeme kwa itikadi ya ushabiki wa mpira kwa makusudi kabisa.
TAKE CARE ON IT📌
 
Nilishalipa gharama za kuingiziwa umeme tangu 11.03.2022 lakini mpaka leo kimyaa. Gharama zilikua 515,000/= huwa kuna utaratibu gani wa kuwasiliana na mteja ili ajue tatizo ni nn maana naamini kama hamko ktk nafasi nzuri ya kuwekea umeme pia msingeendelea kuwapa namba za kulipia
 
Namba yangu ya simu ni 0784856865. Nzega mjini
 
Nimelipia Luku Mita no.37212755179 kupitia CRDB SIM banking lakini mpaka SASA sijapata Token msaada Tafadhali.
 

Naomba kuondolewa kwenye matumizi makubwa, nitumie utaratibu gani?
Asante!
 
Jaman jaman TANESCO Tarakea rombo
Mnanini mwez wa pili huu unaisha cjafungiwa
Umeme kwanini Lakin wateja hamtuthamin
[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Kwa izi mvua kidogo umeme unakata iyo tren ya umeme mlisha handaa sehemu zakulala porini
 
Mwezi wa 5 mwaka jana nilichukua fomu, mwezi 8 mpimaji akaja, mwezi 10 nikalipia ila Mpaka leo sijapata umeme.

Kama kuna konekisheni inahitajika tujuzane tu. Maana hakuna namna.
 
Acheni siasa fisi maji nyie TANESCO kuna nyumba huku mtaani nimezishuhudia kuanzia msingi hadi inaisha na wamefungiwa umeme sie wengine huu unaenda mwezi wa 7 hatujapata huduma ya kufungiwa na tumeshalipia muda mrefu sana ,na ukiwauliza wa TANESCO ofisi ya Nyakato wanatoa sound za uongo uongo na kuomba rushwa
 
Naona kukatika kwa umeme kumeanza kuwa kawaida.

Leo niko Mbezi juu, umeme haupo tangu Asubuhi.

Ijuamaa nilikuwa Masaki umeme ulikuwa unakatika Mara kwa Mara.


Jumatatu nilishindwa kuprint report zangu kwa mda nilioupanga pale mitaa ya mwenge.

Ijuamaa ya Tarehe 29 April 2022 nilikuwa Kariakoo Umeme ulikatika nikashindwa kufanya kazi zangu.

Wahusika Embu fanyeni jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…