Ndugu Mtejawewe TANESCO jana tu ulitulia,leo mmekata tena umeme saa tisa usiku na saa hizi saa tisa mchana mmekata tena.Mna shida gani nini nyinyi?!mimi niko Kimara huku bado umeme unasumbua ila inaonekana sio sisi tu maana nimemsoma Habib Hanga kule twitter nae analalamika kuna mgao wa kimya kimya sehemu nyingi.
Hivi kuna nini?si mseme ukweli?!
Hoja ni kuwa nini mnashindwa kutoa huduma kwa wakati?Tunakusii uache kupotosha uma kwa kuwa hauna taarifa kamili na sahihi
Ndugu Mteja , Tunashukuru kwa taarifa tumeipokea kwa hatua zaidi, tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa mawasiliano zaidiTANESCO Hapa Manzese karibu na serikali ya mtaa Mvuleni kuna transformer ambayo mara kwa mara hubutuka na kuwaka moto, hatari ni mbili
Kwanza wenye mashine za kusaga mahindi wamenunua fire extinguisher na hulimwagia kila linapowaka
Pili chini ya hiyo transformer kuna vibanda viwili vya kuuzia pombe na chakula kuna siku watu watafia hapo kwa nini hamuagizi viondolewe?
Rekebisheni hali hii na hii ni mara ya pili natoa taarifa
0683686908 TANESCONdugu Mteja , Tunashukuru kwa taarifa tumeipokea kwa hatua zaidi, tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa mawasiliano zaidi
Ndugu Mteja!swali langu mimi nipo ilala meter yangu inasumbuwa kuweke luku katika remote nimewapigia offisini emergency wakaja kuniwekea kwa kutoa seald kwenye meter nakuingiza namba yangu ya vocha halafu seald hawakurudisha wanasema ukipata tatizo tena lakuingiza token nipande juu niweke bila kitumia remote swali je tanesco hawawezi kuja nisumbua siku za baadae kuwa hakuna seal kwenye meter nani katoa maana sina ushahidi wa maandishi je nifanye nini?
Tanesco mbona hamnijibu?Nimejiunnganisha kwenye huduma ya niconect nimefikia hatua hiyo hapo je kinachofuata ni Nini?View attachment 2294801
Wazee wa umeme kiukweli inasikitisha sana kwa sasa umeme unakatika na hakuna taarifa yoyote yaani hapa Arusha imekuwa kama vile swala na simba ,hujui saa ngapi mnakata na lini na kwasababu gani? Dar nako yale yale unakuta usiku mpo giza tuuu nini kinawasibu?Tafadhali hakikisheni mnapata magari makubwa yakazi maana huku kwetu tmk yombo tanesco walikuwa wanashida sana ya magari mpk kifikia mafundi sometime kutembea kwa miguu mpk wananchi tunawaonea huruma tunawakodia bajaji, mara wakaletewa gari ya green lkn ni kadogo kwa ajili ya meneja tuu hakafai kitu mara tena likaja lingine jeupe nalo ni dogo halifai kitu.
Hebu kuweni serious mnajua shirika ni la kazi mnaleta vigari vidogo seriously?
Waambieni viongozi wenu wawe serious hayo magari mabovu muyauze mnunue pamba mpya, igeni hata kenya.